Ukweli kuhusu Titanic

"Kama ilivyo punje moja ya mchanga mbele ya fukwe za bahari kuu za dunia, ndivyo ulivyo ufahamu wetu mbele ya tusiyoyajua duniani na ulimwenguni na mbele ya yale tunayodhani kuwa tunayajua". Hayo ni maneno ya mwandishi mwenzangu William Shao.
Na mimi pia naungana naye kwa kusema kwamba, jambo la kweli kuhusu uhalisi umekuwa ukifichwa mno kwani ukweli una tabia ya kuuma. Na badala yake binadamu wamekuwa wakipenda uongo mtamu uliokolezwa asali kiasi cha kuaminika kama kweli lakini kumbe ni uongo. Hata hivyo tukubaliane kimsingi kuwa kuamini uongo ni kuruhusu fikra zilizo huru kupumbazika na kuvaa ujinga katika imani.
Yapo matukio kadhaa yaliyowahi kutokea hapa duniani na kuwaacha binadamu kwa mshangao, kwa machungu au kwa raha, lakini kutokana na hulka yetu ya kuamini uongo mtamu tumejikuta tukiamini uongo kuhusu matukio hayo badala ya ukweli wenyewe.
Miongoni mwa matukio yasiyoweza kufutwa katika vitabu vya kumbukumbu ni pamoja na kushambuliwa vita kuu vya dunia, kushambuliwa kwa kituo cha biashara cha dunia, WTC ambayo hadi leo tumeaminishwa nasi tukasadiki kuwa ililipuliwa na magaidi wa Al-Qaeda linaloongozwa na bilionea wa Ki-Saudia, Osama mwana wa Laden.
Tatizo letu binadamu tulio wengi ni uvivu wa kutokutaka kusaka ukweli na badala yake kwa uvivu tu tunabaki kusadiki uongo ambao unalenga kuficha ukweli. Huo ni upumbavu na kujiruhusu kuwa juha. Kwa leo sitaki kuzungumzia ukweli kuhusu shambulio la WTC, nataka tuzungumzie kuzama kwa meli kubwa kuliko zote zilizowahi kutengenezwa na binadamu duniani, yani Titanic.
Hii ni meli ambayo iliaminiwa na waundaji wake kuwa kamwe haiwezi kuzama kutokana na uimara na usanifu uliotumika kuutengeneza kwa miaka mingi. Ndani ya Titanic kulikuwepo na mahitaji yote muhimu kwa maisha ya nyumbani. Uliweza kucheza soka ndani ya Titanic, uliweza kuogelea, kucheza disko, kununua bidhaa kutoka maduka mbali mbali ndani ya Titanic. Ungeweza kusoma ndani maktaba, baa, mahoteli ya kula na kulala, watu walioa na kuolewa ndani ya meli hii. Kifupi Titanic ilikuwa ni kijiji ndani ya bahari.
Lakini pamoja umaridadi wake, uimara wake, sifa zake, bado Titanic iliweza kuzamishwa ndani ya maji na majasusi wa kanisa la Roma maarufu kama Jesuits miaka mia moja zilizopita.
Kwa nini waliamua kuzamisha meli hii? Walifanyaje mipango yao kwa siri hadi isigundulike? Endelea kusoma maandiko haya.
Inajulikana kuwa mwanzoni mwa miaka ya 1830 Amerika bado ilikuwa haijawa na Benki Kuu wakati majasusi hawa wa Ki-Italiano walihitaji benki nyingine Amerika ambayo wangetumia kuchota fedha kwa ajili ya kufanikisha mipango yao ya vita na ajenda nyingine za siri duniani kote.
Mnamo mwaka 1910 karibu na pwani ya Georgia katika kisiwa cha Jekyll wanaume saba walikutana kwa lengo la kuanzisha benki hiyo ambayo ingeitwa Benki ya Akiba. Hapa ninawazungumzia Nelson Aldrich na Frank Vanderlip ambao waliwakilisha taasisi ya fedha ya tajiri Rockefeller; Henry Davison, Charles Norton na Benjamin Strong waliowakilisha kampuni ya J.P, wengine ni Morgan na Paul Warburg waliowakilisha benki ya Uropa ijulikanayo kama Rothschilds ambayo ilikuwa ni wakala wa Kipapa ikifanya kazi moja tu, nayo ni kulinda utajiri wa kanisa la Katoliki.
G. Edward Griffin katika kitabu chake, The Creature from Jekyll Island, anabainisha kuwa; "Ikumbukwe taasisi hizi; Rockfeller, Morgan na Rothschild zilikuwa (na bado) zinaendeshwa kwa usimamizi wa karibu wa Jesuits kuhakikisha kuwa utajiri wa kanisa usiweze kuporomoka lakini pia zitumike kusambaza imani ya kanisa duniani kote".
Jesuits wamefanya kazi kubwa wakitumia taasisi za fedha duniani kuhakikisha utawala na himaya ya Papa unaendelea kuwa na nguvu siku hadi siku. Wamehakikisha himaya ya Vatican unazidi kuhimarika na kuheshimiwa duniani kiasi cha kuifanya eneo dogo la Vatican kuwa nchi huru ndani nchi kubwa ya Italia. Hii ni kwa matumaini kuwa iko siku Upapa utatawala dunia kidini na kiserikali.
Ujenzi wa meli ya Titanic ulianza mnamo mwaka 1909 katika karakana ya kutengeneza meli ya Belfast, mji mkuu wa Ireland Kaskazini ukiwa na waumini wengi wa Kiprotestanti ambao walikuwa ni maadui wakubwa wa Jesuits katika harakati zao za kusimika Ukatoliki duniani.
Titanic iliundwa na kumilikiwa na kampuni ya kimataifa ya White Star Line ambayo licha ya Titanic pia ilikuwa na meli kubwa nchini Ujerumani pamoja na Uingereza.
Titanic iliundwa na watu mabilionea na maarufu ambao hawakujihusisha na uundwaji wa Benki ya Akiba na kwa jinsi hiyo J.P Morgan alilazimishwa na Jesuits kufadhili ujenzi wa meli hiyo kama maandalizi ya kaburi kwa ajili ya matajiri na watu hao mashuhuri ambao walikuwa wapinzani wa harakati za Jesuits. (The White Star Line-Ibid, uk.246)
Hii ilitokana na hofu kwa Jesuits kwamba watu hawa wangeweza kutumia umaarufu na utajiri wao kuzuia kuwepo kwa Benki ya Akiba. Na kwa kuwa hawa ni watu ambao walipenda starehe na kuponda raha, ni lazima wangependa kuishi ndani ya Titanic ambayo iliundwa maalumu kama kaburi lao bila kujua.
Matajiri, watu maarufu na wale wote ambao Jesuits walitaka wafe walialikwa kuingia ndani ya meli hii kubwa. Pamoja na watu hao maarufu, watu muhimu zaidi waliolengwa hasa ni matajiri watatu ambao ni Benjamin Guggeenhein, Isador Strauss pamoja na John Jacob Astor aliyeaminiwa kuwa tajiri namba moja duniani.
Hawa ni matajiri ambao fedha zao kwa pamoja kwa wakati huo ulikadiriwa kuwa dola za Kimarekani 500 milioni fedha ambayo kwa thamani ya sasa ni dola za Kimarekani 11bilioni. Jesuits walifanikiwa kuwashawishi matajiri wale watatu hadi kuingia ndani ya paradiso inayoelea.
Labda nimkumbushe msomaji, kuwa Jesuit si lazima kuwa padre au mhubiri injili, hapana. Mtu yeyote anaweza kuwa Jesuit na kukitumikia shirika hilo kutegemeana na taaluma yako. Hii inathibitishwa na Edward Smith ambaye alikuwa ni nahodha wa Titanic lakini akiwa ni Jesuit hodari.
Edward Smith amekuwa nahodha kwa miaka 26 akiwa na uzoefu wa kutosha na ruti za bahari ya Atlantiki. Amefanya kazi kwa miaka mingi akiwa ndani ya kampuni ya J.P. Morgan.
Hatimaye ilipofika tarehe 10 Aprili, 1912 Titanic iling'oa nanga chini ya nahodha Edward Smith kwa maelekezo ya mkuu wa shirika la Jesuits, Mtakatifu Baba Francis Browne ambaye naye alikuwepo ndani ya paradiso inayoelea.
Mwandishi Eric J. Phelps katika kitabu chake, Vatican Assassin anasema; "Francis Browne aliingia ndani ya Titanic tayari akiwa na kurunzi na kamera ya kupiga picha watakaokufa hasa walengwa".
Si Edward Smith tu, lakini kila Jesuit huamini kwa kiapo kuwa amri ya mkuu wao ni amri kutoka kwa Mungu kwani kila amri hupata baraka kutoka kwa Papa ambaye ni Bwana wa uhai na mauti. Kwa jinsi hiyo saa na dakika zilipowadia Edward Smith alipokea amri ya kuzamisha meli ya Titanic.
W.C.Brownlee katika kitabu Secret Instructions of the Jesuits, American and Foreign Christian Union uk.143 anaweka wazi kwa kusema; "Katika Jesuit, kuua watu wasio na hatia ni ruhusa kwani amri hiyo hutoka kwa Mungu (Papa) hivyo kutekeleza mauaji yoyote ni halali".
Naye R.W.Thomson katika kitabu The Footprints of the Jesuits, Hunt and Eaton uk.54 anaelezea kiapo cha kuwa mwanachama wa Jesuits kwa kusema; "Nitajiweka katika kundi la wafu siku zote. Nitakuwa tayari kuondoa uhai wa mtu yeyote hata wa kwangu maadamu tu nimepokea amri kutoka kwa Baba (mkuu wa Jesuits). Nitafanya kazi ya ujasusi kwa uaminifu na makini ya hali ya juu kueneza upapa kote duniani".
Pamoja na telegramu zaidi ya nane alizotumiwa Edward Smith kubadilisha mwelekeo wa meli, yeye aliendelea kuelekeza Titanic katika barafu iliyoganda chini ya bahari tena kwa kuchochea mwendo kwani alitii amri kutoka Vatican. Ndipo meli "isiyozama" ilipoivaa barafu na kuchanika vipande vipande na kuua wote waliokuwa wamelengwa isipokuwa mke wa John Jacob Astor aliyeokolewa na boya.
Haya yanahesabiwa kama mafanikio makubwa ya shirika hilo la kijasusi la Roma katika historia yao. Na ilipofika 1913 Benki ya Akiba iliweza kuanzishwa nchini Marekani na miezi minane mbele Jesuits waliweza kutumia fedha kuanzisha Vita Kuu ya kwanza ya dunia na kuua mamilioni ya watu.
Huo ndio ukweli nyuma ya pazia ya kuzama kwa meli maarufu ya Titanic ambayo ni simulizi inayowaliza wengi.
Labda msomaji anaweza kujiuliza je, hili shirika la Jesuits bado ipo duniani? Mwandishi Bill Hughes anatupa jibu katika kitabu The Secret Terrorists kwa kusema; "Hili ni shirika lililo hai jana, leo na kesho hadi pale utawala wa Kipapa utakaposimikwa duniani kote".
No comments:
Post a Comment