Utengenezaji wa sabuni za gharama nafuu ni teknologia mpya ya kutengeneza sabuni bila ya kutumia kemikali ya aina yeyote, na utengenezaji wake hauhitaji mtaji mkubwa kama sabuni zinazotengenezwa viwandani na sabuni za magadi,zinazotumia malighafi nyingi na kemikali kali zinazo changia uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa,pia huleta madhara makubwa kama tahadhari hazito chukuliwa wakati wa utengenezaji wake. Sabuni hizo hutengenezwa kwa kutumia migomba iliyovunwa kwa kukata mikungu ya ndizi, na mafuta ya mawese/mise/pamba n.k.
Gharama za uzalishaji wa sabuni hizi rahisi kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo,kutokana na aina ya malighafi zinazotumika kutengeneza sabuni hizo hasa kwa wanaotengeneza/kuzalisha katika maeneo ambayo mafuta yanapatikana kwa urahisi(Kigoma,Mara,Mwanza,Morogoro na Mbeya).Na nguvu kazi(rasilimali watu) kidogo hutumika, pia uzalishaji wa sabuni hizi ni rafiki wa mazingira.
Namna ya utengenezaji/uzalishaji:
Chukua mgomba ulio vunwa ukate vipande vidogo vidogo kasha vianike hadi vikauke.Baada ya kukauka kusanya vpande vyote na uvichome moto,baada ya majivu kupoa yakusanye, kasha yaweke kwenye ndoo ya lita 20 yakiwa na ujazo wa lita/kilo 10 na uyaloweke kwa saa 24(siku moja),andaa mafuta yako pamoja na box la kutengenezea sabuni,ikiwa upo katika mchakato wa kutengeneza/kuzalisha hakikisha umeandaa ndoo ya ziada.
Kanuni(form)
Chukua majivu yaliyo lowekwa lita 1 na mafuta lita 1, lakini pia unaweza kuchanganya kiasi kikubwa(chochote) kwa uwiano huo kwa mfano majivu yaliyo lowekwa lita 20 na mafuta lita 20, changanya kwenye chombo kimoja anza kukoroga mpaka majivu na mafuta yachanganyike vizuri, kasha mimina kwenye box la kutengenezea sabuni baada ya saa 24 sabuni itakuwa tayari kukatwa, baada ya kukata anika sabuni kwenye sehemu yenye ubaridi isiyofikiwa na mwanga wa jua anika kwa muda wa siku 5-7 baada ya siku hizo sabuni yako itakuwa tayari kwa kutumika.
Pia unaweza kuweka rangi/manukato/virutubisho kama sabuni za viwandani na za magadi
No comments:
Post a Comment