Search This Blog

Sunday, 22 January 2017

MAANDALIZI YA UFUNDISHAJI -2

MAANDALIZI YA UFUNDISHAJI
UJUZI WA SOMO
Baada ya kozi ya miaka miwili mwalimu mwanafunzi awe na ujuzi wa:
 Kufundisha kwa njia shirikishi mada mbali mbali za somo la kiswahili kwa shule za msingi
 Kutambua na kutatua matatizo mbalimbali ya wanafunzi katika kujifunza lugha ya kiswahili
 Kutengeneza, kufaragua na kutumia zana za kufundishia na kujifunzia somo la kiswahili kwa kuzingatia mahitaji mbalimbali ya wanafunzi
 Kuwasaidia na kujali wanafunzi wenye mahitaji maalumu
MALENGO YA SOMO
Baada ya ya miaka miwili mwanachuo aweze
 Kutumia mbinu shirikishi za kufundishia na kujifunzia mada zote za muhtasari wa kiswahili katika shule za msingi
 Kutengeneza kufaragua na kutumia zana anuai za kufundishia na kujifunzia somo la kiswahili
 Kutumia matini zenye masuala mtambuko katika kufundishaia na kujifunzia somo la kiswahili.
 Kutambua matatizo mbalimbali ya wanafunzi katika kujifunza lugha ya kiswahili
 Kufundisha stadi za lugha ya kiswahili kwa wanafunzi pamoja na wenye mahitaji maalum.
NJIA ZA KUFUNDISHIA
Maana ya njia ya kufundishia
Huu ni utaratibu unaohusu uhusiano kati ya mwanafunzi,mwalimu,zana,mazingira, na mada katika tendo lakujifunza.Pia njia za kufundisha ni vitendo vyote vinavyofanywa na mwalimu na mwanafunzi katika kuleta ujuzi, maarifa, na stadi mbalimbali.
NJIA KUU MBILI ZA KUFUNDISHIA
 Njia shirikishi
 Njia isiyoshirikishi
Njia hizi zimegawanyika katika mbinu mbalimbali kama ifuatavyo:
NJIA SHIRIKISHI
 Majadiliano
 Ziara
 Maswali na majibu
 Nyimbo
 Mdahalo
 Hadithi
 Maigizo
 Mradi
 Vitendo
 Bunguabongo
 Kualika mgeni n.k
NJIA ISIYOSHIRIKISHI
 Mhadhara
 Hotuba
 Mahubiri
 Risala n.k
Kabla ya kufundisha unahitaji maandalizi ya kutosha, Ipo miongozo maalumu iliyoandaliwa ya kutuongoza kutengeneza azimio la kazi na andalio la somo la Kiswahili kwa shule za msingi. Mitazamo hii inabadilika kutokana na nadharia na mahitaji ya elimu nchini. Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya mtazamo wa ufundishaji, mkazo umekuwa kwenye ujenzi wa maana hivyo msisitizo umekuwa kwenye kujenga ujuzi.
MUHIMU: Matumizi ya NJIA au MBINU za kufundishia hayana budi kzingatia vionjo mbalimbali kama vile umri, viwango na hali za wanafunzi
SIFA BAINIFU ZA NJIA SHIRIKISHI
 Humshirikisha mwanafunzi
 Humfikirisha mwanafunzi
 Humuondolea mwanafunzi unyonge au uwoga
 Mwanafunzi huwa mbunifu
 Hutumia muda mwingi katika kujifunza na kufundisha somo
 Huchochea udadisi n.k

SIFA BAINIFU ZA NJIA ISIYOSHIRIKISHI
 Mwanafunzi ni msikilizaji tu
 Humfanya mwalimu kuonekana bingwa na kumdunisha mwanafunzi
 Vitendo ni vichache
 Badiliko la tabia huwa ni la muda tu
 Haichochei udadisi kwa mwanafunzi
 Mtu huwezi kufundisha mambo mengi kwa wakati mmoja n.k


FAIDA NA UPUNGUFU WA NJIA ZA KUFUNDISHIA
(a) Faida za njia shirikishi
 Humfikirisha mwanafunzi
 Mwanafunzi huwa mbunifu
 Wanafunzi wengi hushiriki
 Humuondolea mwanafunzi unyonge au uwoga
 Humsaidia mwanafunzi kuwa na kumbukumbu ya kudumu
 Haimchoshi mwanafunzi katika swala zima la kujifunza
 Huinua taaluma ya mwanafunzi
 Hujenga ushirikiano kati ya mwanafunzi na mwanafunzi,mwanafunzi na mwalimu.

(b)UPUNGUFU WA NJIA HII
 Hutumia muda mrefu
 Mambo machache hufundishwa na uwezekano wa kumaliza mada husika ni mdogo
 Huweza kujenga uhasama kati ya wanafunzi(wenye uwezo mkubwa na wenye uwezo mdogo)
 Hufanya wanafunzi wenye uwezo mdogo kutokulipenda somo
 Huweza kusababisha mahusiano mabaya kati ya wanafunzi na wanafunzi kama mwalimu hatasimamia makundi husika katika mambo wanayojadili
(a)Faida ya njia isiyoshirikishi
 Huokoa muda
 Mwalimu anaweza kufundisha mambo mengi kwa wakati mfupi
 Wanafunzi wengi huwekwa pamoja kwa wakati mmoja
 Haina gharama mfano ununuzi wa manila kadi,n.k.Humfanya mwl. Kupata muda wa ziada wa kufanya mambo mengine
 Huondoa matabaka kati ya wanafunzi
(b)UPUNGUFU WA NJIA HII
 Haimjengei mwanafunzi kumbukmbu ya kudumu
 Haimfikirishi mwanafunzi ili awe mbunifu
 Badiliko la tabia sio la kudumu
 Haileti ukombozi wa kifikra
 Hudumaza taaluma ya wanafunzi
 Humfanya mwalimu kushindwa kufanya tathimini ya uelewa wa mwanafunzi katika somo.
 Haichochei ubunifu kwa mwanafunzi
 Humfanya mwanafunzi kuwa tegemezi

MBINU ANUAI ZA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZIA SOMO LA KISWAHILI
Maana ya mbinu:
Ni namna mwalimu na mwanafunzi watakavyotumia njia mbalimbali katika zoezi zima la kufundishia na kujifunzia.Ni jumla ya ya vitendo vyote vinavyofanywa na mwalimu na mwanafunzi katika kuunganisha na kuleta pamoja ujuzi, maarifa,na stadi mbalimbali katika tendo zima la kufundisha na kujifunzia ili kufanikisha kusudi/madhumuni au malengo ya somo.
Ziko njia nyingi za kutengeneza mazingira ya mtoto ili aweze kujifunza pia ziko njia nyingi za kufundisha.Njia za kuweka mtoto katika mazingira yanayofaa ili ajifunze na mbinu mbalimbali za kujifunzia na kufundishia zinaambatana au kutokana na mazingira hayo.
Kutokana na mazingira (teaching situation) tunayomtengenezea mtoto ili aweze kujifunza ,mbinu za kufundiisha na kujifunzia pia hubadilika..
Katika zoezi zima la kujifunza ni vizuri mwanafunzi akawa mkiini au mtendaji mkuu katika harakati za kujifunza,pia mwanafunzi ashikrikishwe katika kusndaa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.vifaa hivi huweza kupatikana kwa kuokoteza ,kutengeneza au kufaragua zana husika.
TOFAUTI ILIYOPO KATI YA NJIA NA MBINU ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA
NJIA MBINU
1.Hutilia mkazo mwalimu kama kisima cha maarifa .
MBINU YA MAJADILIANO
Faida zake:
 Huchochea ushirikiano
 Kila mmoja huweza kutoa mchango wake na mawazo yake kwani watu ni wachache katika kundi
 Huleta ujuzi na uongozi
 Hupunguza kazi ya masahihisho kwa mwalimu
 Hujenga hali ya mashindano kati ya kikundi kimoja na kungine
 Mwanafunzi huwa mbunifu na kuchochea udadisi
 Hujenga kumbukumbu kwa mwanafunzi

HASARA /UPUNGUFU WAKE
 Wale wenye uwezo mdogo hutegemea zaidi wale wenye uwezo mkubwa
 Hujenga uhasama katiya kundi na kundi wanafunzi na wanafnzi
KAZI YA MWALIMU KATIKA MAJADILIANO
1. Maandalizi
2. Usimamizi
3. Hitimisho la majadiliano
4. Kufanya tathimini
5.
Muhimu;vikundi vyaweza kuwa vya kudumu au vya muda.mwi lazima ahakikishe kuna mchanganyiko kati ya wale wenye uwezo mkubwa darasani na wale wenye uwezo mdogo,Pia ahakikishe kuwa vikundi vina uongozi, yaani mwenyekiti, katibu ,mtunza muda ,waelekeze wajibu wao.mwalimu unaweza kuwapa wanafunzi kazi inayofanana naaukazi tofauti.
MBINU YA MHADHARA
Mhadhara ni maelezo yanayotolewa mbele ya watu hasa katika vyuo vya ya juu kwa ajili ya kufundisha.
Faida ya Mhadhara
 huokoa muda
 vitu vingi hufundishwa kwa wakati mfupi
 hutumika kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja
 humwezesha mwl, kukamilisha muhtasari

UPUNGUFU WAKE
1. Badiliko la tabia sio la kudumu
2. Vitendo ni vichache
3. humdunisha mwanafunzi
4. haileti ukombozi wa kifikra
5. hujenga hali ya woga na kutojiamini kwa mwanafunzi
6.
MBINU YA KAZI MRADI
 Humhusisha zaidi mwanafunzi na mazingira anamoishi
 humwezesha mwanafunzi kupata maudhui(maarifa,stadi,muelekeo)ili ayatumie katika jamii yake.
JAMII
MWANAFUNZI MADA
 Humfanya mwanafunzi azame aidi katika jambo

UPUNGUFU WAKE
 Hutumia mua mwingi sana kwa wanafunzi na hata fedha
 huhitaji marejeo ya kutosha yanayoelekeza jinsi ya kuanya mradi kwa kulinganisha mawazo mbalimbali
MBINU YA ZIARA
wanafunzi huhitaji kupewa matayarisho kabla ya kufanya ziara
Wanafunz wapewe maswali muhimu yanayolengwa kwenye somo lako ili wasije wakauliza maswali mengine nje ya somo au kuleta chuki kat yao na ahusika
Hatua zote za ziara zifanyike kabla ya kuanza ziara.MFANO
 Kuwepo matayarisho kabla ya ziara
 Kufika sehemu yenyewe kabla
 Idadi ya wanaunzi ijulikane
 Taratibu na sheria zijulikane
 Wanafunzi wawe na tahadhari
FAIDA YAKE
Huchochea udadisi kwa mwanafunzi
wanafunzi hulifurahiasoo
humwezesha mwanafunzi kuelewa mambo mbalimbali kwa kina au kwa mapana
UPUNGUFU WAKE
Ni gharama/unahitaj fedha
MBINU YA VITENDO
Faida zake
 huleta hali ya udadisi
 hujenga kumbukumbu
 hujenga au husababisha kutumia milango ya maarifa
 huleta tendo la kujifunza kikamilifu
 huondoa tendo la kukariri,vitisho,fimbo n.k
HASARA / MAPUNGUFU YAKE
 hutumia muda mwingi kwa mmambo machache kufundishwa
 wanafunzi wanaweza kwenda nje ya maudhui ya somo
 inafaaa kwa baadhi ya masomo fulani tu kwa mfano katika somo la sayansi
 hufaa kwa baadhi ya watu wa umri fulani tu.kwa mfano huwezi kuwapa vitendo vya kulowa maji watu wazima hii hufaakwa watoto.

MBINU YA BUNGUA BONGO
Hii ni mbinu inayohitaji wahusika kufikiri haraka na kutafuta majibu mengi kwa haraka.
FAIDA YAKE
UPUNGUFU WAKE
MBINU YA CHEMSHA BONGO
Hii ni mbinu inayohitaji wahusika kujibu papo kwa hapo bila kufikiri swali walilopewa.
FAIDA YAKE.
UPUNGUFU WAKE.
Mbinu nyingine zijadiliwe na wanachuokwa kina na mapana yake.
2.0 UCHAMBUZI WA VIFAA VYA MTAALA WA KISWAHILI.
Vifaa vya mtaala wa somo la kiswahili.
Dhana ya mtaala
Mtaala ni utaratibu mzima wa vitendo vya kielimu vilivyopangwa katika shule na vyuo vyenye malengo maalumu kwa wanafunzi.
Mtaala ni pamoja na muhtasari,vitabu na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia.
Mtaala huhusisha pia njia na mbinu mbalimbali za kufundishia na kujifunzia.
Mojawapo ya nguzo kuu za mtaala wowote ni muhtasari itakayotumika katika kutekeleza mtaala.
Mitaala inatokana na misingi ya kifalsafa,kisaikolojia,na kisosholojia.Mitaala lazimaitungwe kufuatana na matakwa,mila, na desturi za jamii inayohusika.
VIFAA VYA MTAALA
a)Muhtasari
b)kitabu cha kiada/kitabu cha mwalimu
c)kiongozi cha mwalimu
d)kitabu cha ziada
a)Maana ya muhtasari
Ni mwongozo unaotaja kwa kifupi tu mambo yote yanayotakiwa yafundishwe katika mwaka mzima katika darasa fulani.Hivyo muhtasasri huoneshani wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia.
UMUHIMU WA MUHTASARI
 Hutoa shabaha na makusudi ya kufundisha somo fulani
 Humsaidia mwalimu asipwayepwaye wakati anapofundisha au asichepuke nje ya muhtasari.
 Hutaja kifungu kwa kifungu mambo yanayotakiwa yafundishwe mwaka mzima.
 Hutoa mapendekezo ya vifaa na vitabu vinavyomsaidia mwalimu na mwanafunzi katika kutekeleza muhtasari.
 Huonesha wakati wa kutoa majaribio na kufanya marudio
 Humdokeza mwalimu mbinu zinazofaa kufundisha vifungu fulani fulani.
 Humwezesha mwl. Kufanya tathimini ya aina moja kwa wanafunzi wote, kwa sababu wanafunzi wote hufanya au kujifunza mada zinazofanana.

b)Vitabu vya kiada
Hiki ni kitabu kitumikacho na mwalimu na wanafunzi katika somo fulani ambapo mada zote zilizo kwenye muhtasari wa somo zimeelezwa kwa undani katika kitabu hicho pamoja na mbinu za kufundishia na mazoezi.kitabu hiki hufaanua mada zote za muhtasasri kwa ukamilifu.
UMUHIMU WA KITABU CHA KIADA
 Hutoa mpangilio na muundo wa mada
 Hufanya uchambuzi wa madazinazotumika kama msingi wa maudhui ya kozi na kutoa msisitizo kwa mada hizo.
 Hutoa mazoezi na ushauri juu ya mbinu na njia za ufundishaji.
Hutoa taarifa juu ya upatikanaji wa vitabu vya rejea,vyanzo vya taarifa za somo, zana za kufundishia n.k
SIFA ZA KITABU CHA KIADA
 Kiwe chenye lugha rahisi
 kiwe na mazoezi ya kutosha
 kiwe kinaendana na muhtasari
 kiwe na maandishi yanayosomeka
 kiwe kinalengakiasi cha elimu au kiwango cha elimu cha mwanafunzi.

c)KIONGOZI CHA MWALIMU
Hiki ni kitabu ambacho humsaidia mwl. Kufundisha somo lake kwa kumpatia maarifa na ujuzi juu ya kozi zote kwa ujumla,kikijadili vipengele vidogo vilivyomo nani ya somo lote.
Hubainisha malengo ya somo,dhana za ufundishwaji na uhusiano uliopo kati yake,kiasi cha ufundishwaji(depth of treatment),mbinu za kufundishia na kjifunzia kwa kuangalia au kulingana na aina ya wanafunzi,vifaa vya ufundishaji.
UMUHIMU WA KIONGOZI CHA MWALIMU
AZIMIO LA KAZI
Ni mpangilio au utaratibu unaomwezesha mwalimu kuchanganua muhtasari wa somo na kupanga mada na jinsi atakavyozifundisha katika kipindi cha wiki , mwezi, na muhula.Ni mpango wa ufundishaji kwa kipindi fulani.
Ni utaratibu maalum wa vipengele mbalilmbali vya muhtasari.utaratibu huu hugawa vichwa vya habari vya muhtasari katika sehemu ndogondogo zinazoweza kufundishika kwa muda wa wiki, wiki mbili, au mwezi mmoja.
Umuhimu wa azimio la kazi
 Humsaidia mwalimu kwenda na mtiririko mzuri wa mada.
 Humwonyesha mwalimu muda wa kufundisha kila mada.
 Huonyesha zana/vifaa/njia ya kumsaidia mwalimu katika ufundishaji wake.
 Kuonyesha malengo ya ufundishaji wa somo hilo katika muda aliopanga.
 Kuandaa mapema masomo akijua ni kipi atakachofundisha na lini.
 Kujipima ikiwa anafundisha haraka au polepole kuliko alivyokadiria.
 Humfuna mwl asitapetape ovyo katika ufundishaji wake na afundishe kwa uzito ulio sawa yote anayopaswa kufundisha.
 Endapo mwalimu ataugua au atahamishwa ni rahisi mwalimu mwingine kuendeleza kazi hiyo.

Wakati wa kuandaa andalio la somo kuna mambo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa,
1. Kusoma kwa makini muhtasari wa somo la kiswahili na kuweza kubaini mada, malengo , zana, na ujuzi ambao utatakiwa wanafunzi wako waupate katika mada husika.
2. Kuangalia kalenda au ratiba ya shule ambayo itakuongoza katika kuandaa azimio lako la kazi kwa kigezo cha muda.
3. Kuhakikisha kwamba vifaa vya muhtasari, vipo na vinatosheleza mfano, vitabu vya kiada, vitabu vya ziada, kiongozi cha mwalimu, kitabu cha mwalimu, na kitabu cha mwanafunzi.
4.
VIPENGELE VYA AZIMIO LA KAZI
 Ujuzi ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
 Katika kusoma ujuzi uliopo katika muhtasari wa somo la kiswahili , inakupasa kujua ujuzi ni upi, na maudhui ni yapi, kwani ujuzi huohuo huweza kujengwa na maudhui mengine.
 Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi. Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji ambao ni ujuzi.
 Malengo mahsusi lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua, kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha n.k. Viwango vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
Sifa za malengo mahsusi : – Ni lazima libebe kitendo kinachopimika wakati unapofundisha.
– Malengo yahusiane na kiwango cha uwezo wa mwanafunzi.
– Muda wa malengo utajwe waziwazi
– Kiwango cha kufikia kila lengo kiwezeshwe.
– Kipindi kimoja kisiwe na malengo mengi.
-Liwe mahususi
– Linapimika
– Linaweza kufikiwa
 Mwezi na Wiki Katika kugawa muda unatakiwa kuzingatia idadi ya vitendo vitakavyofanyika ili mwanafunzi ajenge ujuzi. Kuna baadhi ya vitendo vinahitaji muda mrefu na vingine vinahitaji muda mfupi kukamilika.
 Vipindi : Idadi ya vipindi itazingatia na uzito na wigi wa vitendo katika mada husika. Jiulize vitendo vya kiwango cha juu vina uzito sawa na vitendo vya kuchunguza? Katika muhtasari umepewa muda wa idadi ya ya jumla ya vipindi kwa mada kuu, hakikisha kuwa umevigawa kwa uwiano sawa kulingana na vitendo.
 Vitendo vya Ufundishaji :Kumbuka unapoandika vitendo vya ujifunzaji wewe ni mwezeshaji/wewe ni msaada kwa mwanafunzi wako katika utendaji wake. Katika kuandika vitendo nya ufundishaji unatakiwa kuonyesha yale matendo yote utakayoyafanya mwalimu pamoja na mifano katika uwezeshaji wako.
 Vitendo vya ujifunzaji :Unapoandika vitendo vya ujifunzaji unatakiwa uvichukue ndivyo vitendo vya msingi vitakavyoleta kujengwa ujuzi. Lugha itakayotumika ionyeshe kuwa mtendaji mkuu ni mwanafunzi. Mfano Wanafunzi, kuchora, kueleza,Kujibu maswali ya mwalimu, kujadiliana,kutafsiri,kueleza, kusoma, kujadili, kufupisha n.k
 Vifaa/zana :Matumizi ya zana katika kujifunzia na kufundishia ni nyenzo muhimu sana kwa sababu inatumika katika ujenzi wa maana kwa kile mwanafunzi atakachojifunza. Vilevile zana humsaidia mwalimu katika kumrahisishia kazi yake ya kufundisha.
Zanazitumike kulingana na lengo la somo.Aidha zitumike katika hatua yeyote ya somo kulingana na mpangilio wa mwalimu na lengo la zana husika. Zana zinazoshauriwa kutumika ni pamoja na ;
 Vitu halisi kama mawe ,simu ,redio,miti,darasa,saa,mizani,matunda n.k
 Vifani, mfanomwanasesesre,magari n.k
 Picha,
 Vielelezo,(picha,za kuchora n.k)
ZANA ZITAKAZOTUMIKA ZIWE NA SIFA ZIFUATAZO
 Ziwe na uhusiano na mada inayofundishwa
 ziwe na ukubwa wa kuonekana kwa darasa zima
 Ziwe nadhifu
 Ziwe na uhalisia
 Ziwe zinamfikirisha mwanafunzi
 Ziwe imara
 Ziwe zinavutia
 Zana izingatie ubunifu
 Zana isiwe ya kuumiza,mfano macho,masikio,n.k
 Rejea, Mwalimu atapaswa kuonesha vitabu vya rejea katika mada atakayoifundisha, Kumbuka rejea siyo vitabu tu, bali inahusisha vitu vingine kama majarida, magazeti,vipeperushi, vipindi vya redio, kanda za video, chati na makala mbalimbali na intaneti.
UANDISHI WA REJEA UZINGATIE UTARATIBU HUU WA ‘APA’
a) Jina la mwandishi-anza na jina la ukoo ,kisha kifupi cha jina la kwanza ikifuatiwa na vifipisho vya majina mengine. Kama yapo
b)Mwaka
c)Jina la kitabu(ukitumia herufi ndogo pigia mstari,ukitumia herufi kubwa usipigie mstari)
d)Mchapishaji
e)Mahali kilipochapishiwa
d)kurasa ambazo maudhui yanapatikana
 Upimaji, katika upimaji tunaangalia ufanisi wa ujifunzaji na ufundishaji uliofanyika katika malengo mahsusi. Upimaji huu unahusu vitendo hivyo vimefanyika kwa kiasi gani kuleta ujuzi. Mfano, mwalimu anaangalia ni jinsi gani vitendo vya ufundishaji na ujifunzaji vimefanikiwa.

 Maoni, Inahusu hatua au ushauri utakaouchukua baada ya kufanya upimaji.
Mfano wa muundo wa azimio la kazi
Jina la mwalimu :………………. Mwaka:………………………..
Shule: …………….. Muhula:…………………………
Somo: ……………… Darasa:……………………………..
Ujuzi Malengo mwezi wiki Mada kuu Mada ndogo vipindi v/ufundishaji v/ufundishaji vifaa/zana rejea Upimaji maoni
ANDALIO LA SOMO:
Ni utaratibu au mpangilio wa hatua za kufundishia unaotayarishwa na mwalimu kwa kipindi husika kwa darasa fulani./ ni dira ya kumwongoza mwalimu wakati wa kufundisha.
Pia andalio lasomo no mtiririko wa kimantiki anaoandaa mwalimu ili umwezeshe kujua wazwazi maarifa ya somo atakalofundisha katika kipindi.
Umuhimu wa andalio la somo.
 Huonyesha wazi malengo ambayo mwalimu anatarajia yafikiwe na mwanafunziwake wakati wa kipindi.
 Humwongoza mwakimu kufundisha kwa hatua anapokuwa darasani.
 Humwonyesha mwalimu vitendo vya kufanya wakati wa ujifunzaji na ufundishaji.
 Humwezesha mwalimu kujua ni kitu gani atakachofundisha katika kipindi
 Humsaidia mwalimu kujua ni vifaa gani atakavyotumia
 Humwongoza mwalimu kujua maswali atakayouliza
 Humsaidia mwalimu kutathmini na kutoa maoni juu ya somo alilofundisha
 Huokoa muda kulingana na mada katika muhtasari.
 Uwezo wa mwalimu hutambuliwa vyema
Vipengele vya andalio la somo
 Chati itakayoonyesha taarifa za awali /maelezo ya awali: Tarehe, darasa, kipindi/somo, muda,idadi ya wanafunzi waliopo na wasiopo.
 Ujuzi : ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi. Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji ambao ni ujuzi.
Maneno yanayoshauriwa ni kutumika ni;
 Kuwa na uwezo wa;………
 Kutambua,kufahamu,kubuni,kuchora,kuhesabu,…….n.k
 MADA KUU: andika kama ilivyo kwenye muhtasari

 MADA NDOGO: Andika kama ilivyo kwenye muhtasari au kama hakuna unaweza kuangalia malengo yanayofanana au kukaribiana ili uweze kutengeneza mada ndogo.
 Lengo kuu: Ni lengo la jumla ambalo mwalimu anatarajia wanafunzi wake kulifikia katika ufundishajina ujifunzaji. Inashauriwa liandikwe kwa kutumia maneno yafuatayo;Wanafunzi watambue,waelewe, wafahamu, wajue, wagundue n.k EPUKA KUTUMIA NENO WAWEZE.KATKASEHEMU HII.
 Malengo mahsusi: lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua, kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha ,n.k. Viwango vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
 Inashauriwa kuandika kama ifuatavyo; wakati na baada ya kipindi cha dakika 40 au 80 kila mwanafunzi aweze………….(tumia vitenzi vinavyopimika kama ifuatavyo;kutaja,kueleza,kufafanua,kutofautisha,kuimba,kucheza,kuchora,kubainisha, n.k
1…………………………………………………….
2………………………………………………………
 Jedwali linaloonyesha hatua za ufundishaji.

– utangulizi: Utangulizi ndio hatua ya kwanza ya somo, mada unayotaka kufundisha haipo mbali sana na maisha ya mwanafunzi, ni vema kama mwalimu ukaanza mada yako kwa kutafuta maarifa ya awali aliyonayo mwanafunzi.
Ni vema kufahamu wanafunzi wana maarifa na uzoefu gani kuhusu kile utakachokwenda kukifundisha.Lengo ni kuanza kwa kile wanachokifahamu wanafunzi kisha kuelekea kile kipya, Kwa hiyo kile kile wanachokifahamu kitakuwa ni msingi mzuri ambao kile kipya watakachojifunza kitaleta ujuzi. Mfano unaweza ukatumia njia ya bungua bongo, maswali na majibu au changanya kete kutafuta maarifa ya awali kwa mwanafunzi.
 Inashauriwa kuandika maswali yatakayoulizwa wakati wa utangulizi na majibu yake.Hatua hii inakisiwa kuchukuwa muda wa dakika 3-5 kwa kipindi cha dakika 40
– Ujuzi mpya/ Maarifa mapya: Katika hatua hii Mwalimu anahitaji kufikiri kwa kina kuhusu stadi na maarifa atakayotumia mwanafunzi katika kujenga ujuzi unaotarajiwa. i.e Kuwaongoza wanafunzi kufanya
vitendo mbalimbali vilivyopo kwenye vitendo vya ujifunzaji ili kuweza kujenga maarifa mapya.
 Katika hatua hii mwalimu huwasilisha somo hatua kwa hatua akitumia mbinu na zana mbalimbali ili kurahisisha tendo la kufundisha na kujifunza, mfano onesho mbinu, majadiliano,kufikiri kijozi,kuchanganya kete,vitendo,bungua bongo ,chemsha bongo , nyimbo,michezo ,n.k
 mwl ahakikishe wanafunzi wana shirikishwa kikamilifu katika hatuahii.Hatua hii inakisiwa kuchukua kutumia muda wa dakika 10-15 kwa kipindi cha dakika 40.
-Kuimarisha maarifa: Katika hatua hii mwalimu huandaa vitendo au zoezi litakalopima kiasi cha ujuzi walioupata wanafunzi kulingana na na lengo au malengo mahususi yaliyokusudiwa. Zoezi litakalotolewa lizingatie muda na uwezo wa wa wanafunzi.H atua hii inakisiwa kuchukua au kutumia muda wa dakika 10-15 kwa kipindi cha dakika 40
 Tafakuri : Mwalimu uwaongoze wanafunzi wako kutafakari jinsi maarifa waliojifunza yanavyohusiana na maisha yao na ujuzi wanaotarajiwa kuujenga. Vilevile kupima ufanisi au udhaifu wa ujifunzaji na ufundishaji.
 Mfano;andika au eleza ulilojifunza katika mada ya leo,jambo gani limekutatiza katika mada ya leo,jambo gani ungetaka kufahamu zaidi, kuhusiana na mada ya leo,maarifa uliyopata yatakusaidiaje katika maisha ya kila siku, n.k HATUA HII INA KISIWA KUCHUKUA MUDA WA DAKIKA 2-5 katika kipindi cha dakika 40.
-Hitimisho: katika hatua hii mwalimu huweza kufanya mambo yafuatayo;
Kusisitiza jambo muhimu ambalo mwl. Anataka kulitilia mkazo aidha limetokana na tafakuri au maarifa mapya,U toaji wa shughuli au zoezi litakaloendelea kjenga au kuimarisha ujuzi uliokusudiwa.zoezi linaweza kuwa maswali ya kujibu mmoja mmoja au katika kikundi au kuchunguza/kudadisi jambofulanimmoja mmoja au kivikundi.
 Vitendo vya upimaji, Ni tendo linalifanyika mfululizo toka mwanzo hadi mwisho wa somo. Ni ukweli kwamba utakuwa umeandaa vitendo vya kupima kila hatua ya mada yako. Lakini kuna uwezekano wa kubadili vitendo vya upimaji kulingana na jinsi somo linavyoendelea.
 Katika sehemu hii tumia vitenzi kama vile KUCHUNGUZA,KUONA, KUPIMA, KUBAINI N,K,USIANDIKE SWALI KWENYE SAFU WIMA HII.
-Tathmini: Tathmini inahusu ufanisi wa somo unaotokana na matokeo ya vitendo vya upimaji katika mfululizo wa hatua nzote za somo. Tathmini ya mwanafunzi inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ujifunzaji.
 Mfano mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali yafuatayo , ni mambo gani mmeyapenda katika hii mada, mambo gani hamkuyapenda, na uwaagize watoe sababu kwa majibu waliyoyatoa, mnahitaji msaada gani ili muelewe zaidi? Au wagawie vikaratasi waandike maoni yao kuhusu mada iliyofundishwa na tathmini ya mwalimu inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ufundishaji, Tafakari ya matokeo ya upimaji uliofanya katika hatua zote za somo na matokeo ya tathmini ya mwanafunzi.

a)TATHIMINI YA MWANAFUNZI: Hakikisha unaandika maoni ya wanafunzi kuhusu mada uliofundisha nasio mtazamo wako kuhusu mawazo yawanafunzi, mawazo haya utayapata katika hatua ya tafakuri kama umefuata hatua za somo ipasavyo.Chagua maoni chanya yenye kujenga na kuimarisha ujuzi wa somo au mada husika,mengine yachukuliwe kama changamoto hasa yale yanayogusa ufundishaji wako na mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
b)TATHIMINI YA MWALIMU: Ni mahali mwalimu anapoonesha tathimini yake baada ya kukamilsha ufundishaji na usahihishaji wa kazi za wanafunzi. Tathimini huweza kuandikwa kama ifuatavyo;
 Wanafunzi 25/30 wameweza (…………………….tazama lengo mahususi).ila wanafunzi 5 hawakuweza kufkia malengo kusudiwa ipasavyo kwasababu……………………………………………
-Maoni: Maoni yanatolewa baada ya tathmini, Mwalimu atabainisha mambo yatakayowezesha kuboresha ujifunzaji wa somo. Mfano, kwa wale ambao hawakuweza kufikia ujuzi uliotarajiwa utatumia mbinu gani kuwasaidia, au maoni /ushauri kuhusu namna ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wako.
MUUNDO WA ANDALIO LA SOMO:
TAREHE DARASA KIPINDI MUDA IDADI YA WANAFUNZI IDADI YA WANAFUNZI
IDADIYAWALIOANDIKISHWA
IDADI YA WALIOHUDHURIA
ME KE JML ME KE JML
Ujuzi…………………………
Mada kuu………………………………………
Mada ndogo…………………………………..
Lengo kuu……………………………………….
Lengo mahsusi……………………………..
Zana/vifaa:…………………………………………..
Rejea:…………………………………………….
Hatua za somo
Tarehe Vitendo vya ufundishaji Vitendo ujifunzaji Upimaji
utangulizi
Ujuzi mpya
Kuimarisha maarifa
Tafakuri
Hitimisho
Tathmini ta wanafunzi…………………………………………..
Tathmini ya mwalimu…………………………………………….
Maoni………………………………………………………………
SHAJARA YA SOMO.
 Ni muhtasari unaotayarishwa na mwalimu wa somo kuonyesha mada kuu na mada ndogo alizofundisha,wakati alipofundisha, na jina au sahihi yake. Pamoja na kumbukumbu hii, mwalimu ana kumbukumbu zingine zinazotumika kama rejea za kazi alizofanya. Mfano nukuu za somo, andalio la somo, azimio la kazi.
 Ni utaratibu katika kitabu au daftari maalumu katika kuweka au kutunza mada ambazo zimekwisha fundishwa katika somo kwa kipindi cha wiki,mwezi au hata muhula.
 Shajara ya somo huwa na uhusiano na Azimio la kazi pamoja na andalio la somo.
Umuhimu wa kumbukumbu za somo/shajara ya somo
 Huonyesha mambo yaliyofundishwa na wakati yalipofundishwa.
 Mwalimu huweza kupima kiasi cha mada alizokwisha kufundisha kwa kulinganisha na azimio la kazi.
 Humwelekeza mwalimu mpya mahali pa kuanzia.
 Huweza kupima muda uliotumika katika ufundishaji wa mada ukilinganisha na azimio la kazi.
 Endapo mwl wa somo amepata uhamisho ni rahisi kujua alikofikia ili kuwa na mtiririko mzuri wa ufundishaji.
 Kurahisisha kazi ya ukaguzi, wakaguzi wa shule wanapofika na kuona shajara ya somo hupata picha halisi juu ya utekelezaji wa mtaala hapo shuleni.
 Inamsaidia mwalimu wa somo kujitathimini mwenyewe baada ya juma ,moja amefanya nini?

MUUNDO WA SHAJARA LA SOMO
MWEZI Wiki MADA KUU MADA NDOGO TAREHE
KUANZA TAREHE
KUMALIZA MADA ZILIZOFUNDISHWA SAHIHI NA MAONI YA MWALIMU WA SOMO SAHIHI NA MAONI YA MKUU WA IDARA. SAHIIHI NA MAONI YA MKUU WA SHULE
Jan 1
na
2 Fasihi Fasihi simulizi 2/2/2012 15/2/2012 -maana ya fasihi
-dhima ya fasihi simulizi
– vipengele vya fasihi simulizi
Swali
1. Kama mwalimu ni changamoto gani unazokutana nazo katika kutumia njia shirikishi.Toa maoni yako namna ya kutatua matatizo yako.
2. Jadili nini kitatokea kama mwalimu ataingia darasani bila maandalizi ya kutosha?
3. Eleza umuhimu wa kuandaa andalio la somo.
4. Chagua mada yeyote ya somo la kiswahili, andaa andalio la somo la dakika 40.
5. Elezakwa kutoa mifano na taja sifa tano za malengo mahsusi.
ZANA /VIFAA VYA KUJIFUNZIA
MAANA NA UMUHIMU WA KUTUMIA ZANA
Zana za kufundishia na kujifunzia ni kitu chochote anachotumia mwalimu ambacho kitamsaidia kufundisha somo lake kwa ufanisi zaidi na kuwavutia wanafunzi wake katika zoezi zima la kujifunza.Zana zinafanya mada kueleweka kwa urahisi,ufundishaji unakuwa wa ukweli na wa uhakiki(real).
UMUHIMU WA KUTUMIA ZANA
 Mtoto anajifunza zaidi kwa kuona,kugusa,kuonja, kunusa, na kusikia
 Humpa mwanafunzi fursa ya kutumia milango mbalimbali ya kumpatia maarifa na ujuzi
 Humsaidia kubadilisha mazingira ya kupatia maarifa na ujuzi
 Humfurahisha mtoto na kumfanya ayapende yale anayojifunza
 Humsaidia kumpatia mwanafunzi maarifa na ujuzi kwa njia ya mkato,na ujuzi wa maarifa hayo huwa vigumu kusahaulika upesi
 Huleta ukweli katika somo kwa vile mtoto anaona vitu vya kweli au mifano yake.
 Husaidia kumfanya mtoto ajifunze kwa njia ya kutenda na si kwa kusikiliza tu.

MAANA NA UMUHIMU WA TATHIMINI
UMUHIMU WA TATHIMINI
 Kugundua matatizo walio nayo wanafunzi yanayoathiri kujifunza kwao
 Kuwapa wanafunzi matokeo na maendeleo yao ili waweze kutambua kama ni mazuri au siyo na hivyo kuwatia ari ya kuongeza bidii zaidi
 Kuwapatia walimu taarifa kuhusu ufanisi wa njia na vifaa vya kufundishia na kujifunziaili kuweza kurekebisha matatizo yaliyopo
 Kuwapatia wazazi au walezi maendeleo ya watoto wao shuleni
 Kutakla kujua ufanisi wa mpango wa elimu ili kuweza kurekebisha matatizo yaliyopo na kama ni mradi kuweza kuamua kuendelea au kutokuendelea
 Kupata taarifa zitakazosaidia katika kufanya maamuzi ya kuaminika kuhusu mipango ya elimu
 Kuhakikisha kwamba muda,nguvu,na jitihadazilizowekwa kwenye mpango wa elimu hazipotei au kutumika vibaya
AINA ZA TATHMINI
 Tathmini ya kupima uwezo wa kumudu somo
 Tathmini ya kuendelea
 Tathmini ya kudodosa
 Tathmini ya mwisho/tamati

No comments:

Post a Comment