Search This Blog

Tuesday, 24 January 2017

MBINU YAKUFANYA WASOMAJI WAKO WAVUTIWE NA HABARI ZAKO

“Je! Unaandika post lakini hazivutii wasomaji kuzisoma? Tazama mambo ya kuzingatia ili itie mshawasha” 

Wateja wa blog yako hawasomi post zako kwa sababu tu zina ujumbe mzuri, la hasha! Ila pia kwa kuwa zinavutia machoni na zinawafanya wajihisi wepesi kuanza kuzisoma. Kama post yako itakuwa ni maneno tu yamejaa kurasa yote humfanya msomaji ahisi kuwa atachukua muda mrefu kusoma na kuchanganua kilichoandikwa. Lakini kama itakuwa imepangiliwa vizuri basi hatoona wingi wa maneno na ataanza kuelewa kinachozungumziwa kabla hajamaliza kusoma.

Vifuatavyo ni vitu vitakavyomtamanisha msomaji asome post yako

1. Vichwa vya habari vya chapisho

Kazi iliyopangiliwa kwa kuwa na vichwa vya habari vinavyotambulisha kila wazo katika post yako humfanya msomaji aelewe anachokisoma baada tu ya kuona kichwa hicho. Mfano ukiandika post kisha baada ya kichwa cha post yakajaa maelezo tu hadi mwisho itamlazimu msomaji aisome kazi yote ndio apate picha ya kinachozungumziwa. Lakini kama baada ya kichwa cha habari kikuu ukaandika aya moja kisha kikafata kichwa cha habari kidogo kisha maelezo yake, kisha vivyo hivyo mpaka mwisho, kutamfanya msomaji aelewe habari nzima kwa kusoma vichwa vya habari tu na hivyo huwa mwepesi kuisoma kazi nzima. 

2. Picha katika blog

Picha hutoa ujumbe kwa wepesi zaidi kuliko maneno elfu moja. Matumizi ya picha hupunguza mlundikano wa maneno pamoja na humpa msomaji kitu cha kujiburudisha akiwa katika post yako. Humfanya msomaji apate ujumbe wa kinachozungumziwa na kukumbuka kwa wepesi zaidi ujumbe ule. Picha inaweza ikawa ni ya kupiga kwa kamera, mchoro, chati ama jedwali. Ni muhimu tu kuzingatia masuala ya haki miliki unapotumia picha.

3. Listi/orodha katika blog

Kutumia listi ni kujaribu kuyapanga mawazo yako katika mtiriliko ambao utakuwa na vichwa vya habari na namba ama nukta. Listi hufanya post ionekane nyepesi na yenye kusomeka. Jitahidi kutumia listi katika post zako ambazo zinaruhusu listi. Post hii ni mfano mzuri wa matumizi ya list.

4. Rangi za blog

Si kila post itakuwa na rangi yake, la hasha! Ila mpangilio mzuri wa rangi katika post zako hupendezesha post na kuonekana ni za maana hata kama yaliyomo hayafikii kiwango hicho cha umaana. Jaribu kutumia rangi tofauti katika kichwa cha habari kikuu, vichwa vidogo, linki na maneno yaliyobaki. Kwa kawaida kuseti rangi huwa kunafanyika wakati wa kudizaini blog yako.

5. Video katika blog

Video zina faida kama ilivyo picha ila kwa video ni zaidi. Kuna aina ya watu ambao huwa wanauwezo mkubwa wa kujifunza kwa kusikia kuliko kusoma hivyo kwa video na sauti watavutiwa zaidi na blog yako. Zipo tovuti ambazo unaweza kuweka video zako bure kisha ukaziunganisha katika blog yako.

No comments:

Post a Comment