Search This Blog

Sunday, 22 January 2017

Wanawake hukamatwa kirahisi wanaposaliti kuliko wanaume

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3782828/highRes/1541961/-/maxw/600/-/eajpn5/-/
Kwa ufupi
Lakini mtihani unabaki kati ya mke na mume nani anaweza kuwa kwenye uhusiano nje ya ndoa na mwenzi wake asijue?

Kwa mujibu wa uchunguzi mdogo uliofanywa na gazeti hili umebainika kuwa kati ya mwanamke na mwanaume, anayebainika haraka anapomsaliti mwenzake kuwa ni mwanamke.

ADVERTISEMENT
By Kalunde Jamal, Mwananchi
Tofauti na ilivyoeleka na kusikia wanawake wengi wakiwalalamikia waume zao kutoka nje ya ndoa, wapo wanawake wanaolalamikiwa pia kufanya hivyo.

Lakini mtihani unabaki kati ya mke na mume nani anaweza kuwa kwenye uhusiano nje ya ndoa na mwenzi wake asijue?

Kwa mujibu wa uchunguzi mdogo uliofanywa na gazeti hili umebainika kuwa kati ya mwanamke na mwanaume, anayebainika haraka anapomsaliti mwenzake kuwa ni mwanamke.

Wanaume kadhaa wakizungumzia suala hilo walisema kutokana na maumbile, utamaduni, hisia za mwanamke anapokuwa na uhusiano nje ya ndoa ni rahisi kufahamu tofauti na mwanaume anayeweza kufanya hivyo miaka kadhaa bila kubainika.

Matheo Matete alisema mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke, wanawake kwa miaka mingi bila kubainika na mkewe kutokana na kujiamini na kuona hilo suala ni la kawaida na ni haki yake kufanya.

Alisema mwanaume anaweza akatembea na marafiki wote wa mkewe na asibainike kutokana na kumudu kukaa kimya, kutobadilika akimuona mwanamke husika, lakini kwa mwanamke ni tofauti kwani hata akimuona huyo mwanaume hubadilika na urafiki na mwenzake utaisha na ipo siku atatoa hiyo siri.

“Wanawake wazuri kuficha baadhi ya siri kama udhaifu wa waume zao, siri za familia kwa ujumla, ingawa wakikasirika pia ni rahisi kuzitoa, lakini za mapenzi hawawezi wana mhemko, kiherere, wakati mwingine hata kiburi.

“Hawawezi kufanya jambo hilo bila kushirikisha marafiki zao, ambao wakiwaudhi kidogo husema, ”alisema Matete.

Dori Gasper alisema mara kwa kawaida mwanamke hawezi kuficha kutokana na kuzidiwa akili na wanaume ambao wanazijua mbinu mbalimbali za wanawake wanaotoka nje ya ndoa kwa sababu wana uzowefu wa kuwa nao.

Alisema jambo lingine wanawake wana majukumu mengi, hivyo wakiingia kwenye uhusiano nje ya ndoa ni rahisi kubainika kwa sababu nyumbani mambo yatakuwa hayako sawa.

“Inawezekana kuna wafanyakazi, lakini mwanamke mwenye nyumba nafasi yake ipo pale pale, kama hapo awali hakuwa na nyendo akianza tofauti itaonekana wazi, hivyo kumstua mumewe na hata ndugu wa karibu, ”alisema Gasper.

Hoja ya Gasper inaungwa mkono na Juma Kingole aliyesema mwanamke akiwa na uhusiano nje ya ndoa hujulikana mapema kutokana na kubadilika ikiwamo kuwa na dharau.

Alisema wengi wao wakipata mwanaume wa nje huona huko wanapata mapenzi matamu kuliko ndani na kuwa na kiranga kinachosababisha kuonekana wanafanya hivyo.

“Mwanaume tu anaweza kuwa na uhusiano kwa miaka mingi nje ya ndoa bila kubainika, lakini mwanamke tena kama ni mkeo rahisi sana kubaini.

“Hawajifichi nakuambia, wana mapenzi ya ajabu na wakiingia sehemu huingia mwili mzima, utaona tu mara anachelewa kurudi, ukimuuliza kitu anajibu huku anaondoka zake, hakuuliza mbona umechelewa, hujaoga, hujala yeye ana hamsini zake, ”alisema Kingole.

Kingole alifafanua kuwa mbali na hayo bado hatakuwa na muda wa kukutana faragha na mumewe na kila akiambiwa anaona kama ametukanwa au kubughudhiwa.

“Mapambo, mavazi, miondoko, hubadilika, visafari visivyo rasmi kama mama wa nyumbani huongezeka, watoto, familia kwa ujumla itajiendesha bila uangalizi wake, ”alisema.

Hoja ya wanawake kuwa wa kwanza kubainika kuwa wanatoka nje ya ndoa imepingwa na Muntali Abrahman alisema mwanamke na mwanaume haraka kugundulika na kukamatwa kama ana uhusiano na mwanaume kwa sababu hajali na haoni kama amefanya kosa.

Alisema wanaume huwa wanaamini kuwa na nyumba ndogo ni haki yao hivyo hata kujificha ni nadra , tofauti na wanawake ambao huamini wanafanya dhambi na siyo desturi.

“Mimi naamini kabisa mwanamke akitaka jambo lake anafanya na hakuna atakayejua, tena jambo lenyewe hilo la kutoka nje ya ndoa, siyo rahisi kulianika.

“Nafahamu kuwa wanapenda sana , tofauti na wanaume ambao wanaweza kutembea na mwanamke na isiathiri maisha yao, lakini bado wao wana uwezo mkubwa wa kuficha siri, ndiyo maana kuna kesi za wanaume kubambikiwa watoto, ”alisema Abrahman.

Nuru Salum anaunga mkono hoja ya Abrahman kwa kusema mwanamke ana uwezo wa kuficha siri siyo tu ya kuwa na uhusiano bali hata kuzaa na mwanaume mingine ilihali ameolewa.

Alisema kama anaweza kuzaa nje ya ndoa, bila shaka ni mtaalamu wa kuficha uhusiano wake wa nje ndiyo maana hajabainika hadi amezaa.

Alifafanua kuwa wanaume wakifanya hivyo hawana kificho na hata ujumbe wakitumiwa kwenye simu hawafuti utaukuta na wakati mwingine hurudi wakinukia manukato.

“Usiende mbali mimi mume wangu alinifunza hilo alikuwa na uhusiano na mwanamke shangingi kila siku alikuwa anarudi na poda kwenye shati za rangi tofauti, ananukia manukato mengine, hali chakula, harudi kwa wakati na nilipoivizia simu yake nilibaini kutokana na ujumbe waliokuwa wakitumiana.

“Yupo jirani nafahamu kama kaolewa na anatembea na shemeji si jana si juzi na hadi leo mwanamke hajastukiwa ila mke wa shemeji yangu ndiyo ananihisi mimi na huyo rafiki yangu, ”alisema Salum.

Alisema hata kuhisi huko kulitokana na ndugu yao kuwasikia wakizungumza , lakini hakuelewa vizuri ni nani kati yao anatoka nae.

Nae Maria Faustine alisema inategemea wanandoa hao wanachukulianaje ingawa haamini kama mwanamke kwa mazingira yake anaweza kuwa na uhusiano kwa muda mrefu bila kugundulika.

Alisema wanaume siyo rahisi kugundulika kwa sababu hakuna anayewapangia muda wa kurudi, wazungumze na nani na wala waende wapi, lakini mwanamke anapangiwa yote hayo.

Alisema wanawake hujishtukia na anakuwa mkali akiulizwa, simu inakuwa na namba za siri lukuki na akibanwa na maswali atalia kujitetea, lakini mwanaume makini ataujua ukweli.

No comments:

Post a Comment