Search This Blog
Sunday, 22 January 2017
Mambo matano ya kuepukwa wakati wa usaili wa kazi
Watu tulio wengi tunakuwa na hofu sana wakati wa kufanyiwa usaili. Tunakwenda katika usaili bila kuwa na maandalizi yoyote. Muda mwingi tunautumia katika kuwaza na kuwa na wasi wasi mkubwa juu ya "Maswali mtego" na aina gani ya nguo tunayotakiwa kuvaa wakati wa kufanyiwa usaili, badala ya kufanya vile vitu ambavyo ni muhimu kuambatana na usaili. Zaidi ya yote, tunaamini kwamba usaili unakusudia kwetu kujibu maswali ambayo wasaili hutuuliza. Nasema haya kwa kuwa mimi ni mmoja miongoni mwa wengi waliojihusisha na usali nikiwa katika pande mbili za meza moja: nikiwa kama mmoja wa watu waliofanyiwa usaili, pia nikiwa kama mmoja wa watu waliowafanyia watu wengine usaili. Lakini mbali na hayo yote, bado una nafasi ya kujiweka vizuri katika mchakato mzima wa usaili, unaweza kupata kazi katika makampuni makubwa na kuwashinda washiriki wengine ambao wamekuwa na uzoefu wa miaka mingi kukuzidi. Katika ulimwengu wa uchumi wa sasa, kujua namna ya kusaili, ni vizuri sana. Yafuatayo ni mambo 5 ambayo hutakiwi kufanya wakati wa usaili. 1. "Nilikuwa na... na kisha... na kama... na uh... yeah." Kama utababaika, utapoteza. Kwanza, unatakiwa ukumbuke mara ya mwisho kukutana na mtu na kumuuliza swali rahisi ("Hivyo, umewahi kufanya nini ulipokuwa mwandishi wa habari, au wakati unajifunza hapo chuoni, ni jambo gali ulipenda kulifanya zaidi?"), kusikia ndani ya dakika sita pekee juu ya maelezo yanayohusiana. unajisikiaje? Sasa chukulia kwamba hii inatokea katika usaili wa kazi. Wasaili hawatathmini mbinu zako katika kujibu maswali yako. Wanatumia mfumo wa maswali ya uwanja wa ndege wakijiuliza wao wenyewe. Kubali ama kataa kuwa, tunatathiminiwa kutokana na muonekano wetu, pia kutokana na uwezo wetu ama ujuzi wetu. Na kama hutoweza kutoa majibu mazuri na mafupi yenye kueleweka katika usaili, wanaokufanyia usaili watastaajabu endapo utakuwa na uwezo wa kufanya kile unachoombea kazi. 2. "Yeah, nimesaidiwa na Yule lakini sikuwa mimi." Ghilba ni jambo zuri, lakini kwenda tofauti na njia yako kwa lengo la kuwa bora zaidi katika usaili ni kufanya usaili kuishia usipotegemea. Unatakiwa kuwa muwazi kuhusu mambo yako, lakini wanaokufanyia usaili hawatojali kuhusu mambo yako katika maisha au namna unavyowasiliana na watu. Wanahitaji kujua zaidi ulichokifanya. Wanahitaji kujua unavyofikiri; wanahitaji kujua zaidi kuhusu wewe. Kama utaamua kucheza na mambo uliyoyakamilisha, namna ambavyo meneja wako alivyokuthamini kwa lengo la kukuweka juu? Ni sawa kujivuna kwa kazi uliyoifanya. Ni vema pia kujiamini. Jaribu: jitahidi kusema kwa mfano, "Nashukuru umeniuliza juu ya mradi huo. Najivunia matokeo tuliyoyapata, pamoja na ongezeko la pato kwa 13% ndani ya miezi 6." Angalia ni kwa namna gani hii itakuweka katika hisia za mafanikio. Je, itakufanya usijikie sawa kwa mara ya kwanza? Bila shaka. Hatujazowea kusema kuhusu makamilisho yetu bila kujihusisha nayo. Lakini kwa mara ya tano unatakiwa kujaribu majibu yako kwa kujiamini, itakufanya ujisikie vema. 3. "Niliacha kazi ya kwanza kwa sababu sikuwezana na boss wangu." Sote tuna mabosi ama tumewahikuwa na mabosi, lakini katika usaili hapatakiwi kuleta habari za kivita ama ugomvi. Wengi wamekuwa wanaingia katika mitego midogo ya namna hii wanapoulizwa pengine kwa nini ameacha kazi ya kwanza. Hapa unatakiwa kuwa makini katika kujibu swali kama hili. Nenda katika njia sahihi: unapoulizwa swali la namna hii jaribu mathalani kujibu "Nilifurahia kwa hakika kufanya kazi katika kampuni ile. Moja ya mambo niliyoyakubali ni kuwa huru kukuza ujuzi wangu katika sehemu niliyopangiwa kutekeleza majukumu yangu, lakini sasa niko tayari kuutumia ujuzi wangu katika hadhi ya juu kabisa. Ndiyo maana nikasukumwa kufanya kazi nanyi..." 4. "Nilifanya kazi kwa bidii sana." Kwa hivi, nini mapungufu yako makubwa? Watu wanaofanya usaili, hupenda sana kuuliza swali la namna hii kwa sababu hutenga watendaji wa juu kutoka katika wafanyakazi wa kiwango cha kati. Jibu hasa la swali hilo ambalo limezoeleka kwa kila mtu—jibu baya lisilofaa – mwitikio wake hujulikana: "Nilifanya kazi kwa idii sana" au "Nina matatizo kusema hapana katika kutekeleza majukumu." Waajiri siyo wajinga kiasi hicho. Wanaweza kuona ukweli kupitia mwitiko wa namna hii. Hivyo jibu sahihi ni lini katika swali kuhusu udhaifu wako mkubwa ama mapungufu yako? Angalia "swali nyuma ya swali." Wanachokitaka wasaili katika kuuliza swali hili ni kujua kwamba, unajitambua kwa kiwango gani na namna gani unaweza kubainisha mapungufu yako hasa katika kupata msaada wa kuyatatua – kila mtu ana matatizo yake – lakini zaidi ni kama umechukua hatua kuhakikisha unasahihisha mapungufu yako. Hivyo badala ya majibu mafupi yasiyo na ufumbuzi wa matatizo yako, unatakiwa kueleza nini hasa mapungufu yako na namna ulivyopigana ama unavyopambana kuyamaliza. Jaribu kuelezea mapungufu yako kinaubaga. Hoja hapa ni kuonesha pia mikutano kadha uliyohudhuria ama kazi mradi ulizofanya. Hivyo ndivyo wanavyojibu swali kuhusu udhaifu ama mapungufu hasa katika usaili. 5. "Nimetengeneza 40% ya faida katika kazi ya awali, hivyo nahitaji kazi ambayo itanifanya nitengeneze faida kubwa pengine kama 50% au zaidi. Lakini unajua...nitapenda hata 45%." Watu wanaokufanyia usaili daima watataka kujua ni kwa kiwango gani umezalisha faida katika kazi yako ya awali. Lakini siyo jukumu lako kuwaambia. Unapowaambia kuhusu kiwango cha faida ulichopata katika kazi ya awali, unajiweka wewe mwenyewe katika kundi la kutokuwa na thamani endapo utafanya hivyo na kutambua kiwango cha mshahara wako. mathalan, kama utawaeleza kuwa, unapokea 500,000 kwa mwezi, na mwajiri wako mpya alipanga kukupa ofa ya 600,000, ni wazi kuwa utapoteza 100,000 katika sentensi yako moja tu. Hata katika uchumi huu, makampuni machache yatakukataa kwa sababu tu ya kutojibu swali linalohusiana na mshahara. Hii kutokana na sababu kuwa, inagharimu maelfu ya shilingi kuajiri watu wa kiwango cha kati. Kama wanakutaka hasa, watakupa ofa, na mkaweza kuzungumza. Kwa nini wanakuuliza juu ya mshahara wako, hii ni mbinu ya kuitumia kujibu swali la namna hiyo: "Nina hakika kuwa, tunaweza kujadili kuhusu mshahara muda utakapofika, lakini kwa sasa nahitaji kuona kama kuna makubaliano baina yangu na wewe." Majadiliano yanaweza kuwa magumu, lakini yanaweza kuwa na thamani ya maelfu ya shilingi kwako. Sasa naamini kuwa utakuwa umejifunza namna ya kukabiliana na wasaili – hizo njia 5 za kushinda katika usaili. Epuka mambo haya matano na angalia mbele zaidi kwa lengo la kushinda katika usaili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment