Search This Blog
Sunday, 22 January 2017
UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ?
MAKALA hii nimeiandika maalumu kwa watanzania na wadau wangu wote , wanafunzi wa SHULE ZA MSINGI , SEKONDARI, na VYUO wanaopenda kujifunza LUGHA YA KIINGEREZA na lugha nyingne ngeni lengo ni kuweza KUANDIKA na KUONGEA kwa UFASAHA na UMAHIRI.
Limekuwa ni tatizo kubwa kwa Watanzania wengi na wanafunzi wetu kuanzia ELIMU AWALI, MSINGI,SEKONDARI , VYUO kutoweza kuongea KIINGEREZA kwa ufasaha na umahiri.Hata Lugha ya KISWAHILI ingawa ni lugha yetu ya taifa bado ni tatizo kwa watanzania wengi na wanafunzi kuongea kwa ufasaha na umahiri ! TATIZO NI NINI ? UTAKUZAJE UWEZO WAKO WA LUGHA ? Kujifunza LUGHA yoyote ni suala ENDELEVU {long and permanent term } na siyo suala la KUJIFUNZA LUGHA KWA WIKI TATU TU, AU MIEZI MITATU TU ,AU MIEZI SITA TU ! KAMA MATANGAZO YA BIASHARA YANAVYOJITANGAZA . “ JIFUNZE LUGHA YA KIINGEREZA KWA WIKI TATU “ hii si kweli ndugu yangu.
LUGHA ni mtaji , inaweza kukufanikisha mambo yako katika maisha ! Ndugu yangu MTANZANIA kama wewe ni mbumbumbu wa Lugha ya KISWAHILI au KIINGEREZA utachina au utakwama katika masuala yako yanayohitaji UMAHIRI katika lugha hizo mbili . Kuna umuhimu sana kwa ndugu yangu MTANZANIA kuwa MAHIRI katika kutumia KISWAHILI au KIINGEREZA kwa ufasaha na umahiri .
SIRI ZA KUIKUZA LUGHA YA KIINGEREZA
---Huwezi kuimiliki lugha yoyote kama huitumii.Mtu anaweza kujidai kuwa kwa vile ni mswahili na amezaliwa katika lugha hii basi anaijua lugha. Hii si kweli kabisa ndugu yangu .Kama ingekuwa hivyo basi wote tungeweza kutumia na kuielewa MISAMIATI na MISEMO yote ambayo iko katika lugha yako.Kwanini basi wengine wakiitumia MISEMO na MISAMIATI hito wewe unatoka kappa , ni kwa sababu huitumii.Kwa hiyo jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa unaitumia lugha.
----Kwa wale wanaojifunza lugha ya kigeni , jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa unaitumia ili uweze kupata uzoefu na hatimaye kuitumia kadri unavyotaka.
-----KUITUMIA LUGHA MAANA YAKE NINI ? Izungumze au itumie katika MAANDISHI ; kama ni lugha ngeni kwako.Kadri unavyoendelea kuitumia katika mazungumzo au katika kuiandika basi unakuwa na uwezo wa kuielewa na utahitajika kupata misamiati mipya.
----Hudhuria katika mikutano na uhakikishe unatafuta nafasi ya kuzungumza. Unapozungumza katika matukio kama hayo maana yake utapaswa kuchagua MANENO/ MISAMIATI na kuyapanga ili uonekane unajieleza kwa ufasaha na kile kinachokusudiwa. UWEZO WA LUGHA UTAHITAJIKA.
-----Makongamano , au hata ubishi wa kawaida mitaani ni nafasi nzuri kwako wewe kuitumia ili uweze kukuza uwezo wako wa lugha. Na wewe uingie katika ubishi halafu uangalie , fanya tathmini , baadaye , kwa nini ulishindwa au kushinda, kwa nguvu ya hoja au kwa hoja ya nguvu.Kama unamiliki lugha unaweza KUSHINDA kila KONGAMANO.
-----Jifunze kutunga HADITHI au kuzisoma , KUTUNGA MASHAIRI.Haya ni mambo pekee yanayoweza kukufanya uhitaji uwezo mkubwa wa lugha na hazina kubwa ya MISAMIATI.
UTATUNGAJE MASHAIRI KAMA MISAMIATI YAKO NI MICHACHE ?
Aidha ukitunga MASHAIRI au HADITHI utajikuta nyakati zote unatafuta KAMUSI au VITABU vya MISEMO na lugha ili uweze kupata MANENO yanayofaa katika utunzi wako kwa ajili hii LUGHA yako inakua kwa haraka sana.
Lakini zuri sana hapa ni kuwa kadri unavyoendelea kujihusisha na utunzi wa MASHAIRI au HADITHI UNATUMIA MUDA MWINGI KUFIKIRI , na jinsi unavyoendelea kushughulika na mambo hayo, uwezo wako wa KUFIKIRI NA KUTAFAKARI nao huongezeka. Ongezeko la uwezo wako wa KUFIKIRI ni matokeo ya kuwa na UWEZO MKUBWA WA LUGHA.
----SIKILIZA , Wengine hudhani KUSIKILIZA sio sehemu ya kutumia / kujifunza LUGHA.
-----FUNGULIA REDIO, utasikiliza MISEMO na MISAMIATI mbalimbali ambayo utahitajika kuielewa ili uweze kufuatilia kinachoelezwa .Kwa hiyo basi kadri unvyoendelea kuisikiliza ndivyo unavyoweza kuielewa vizuri zaidi. Kwanza unapoisikiliza lugha ikizungumza na wenyewe , kwa mfano , unajifunza MATAMSHI SAHIHI , unajifunza MISEMO ambayo huwezi kuipata katika matukio mengine.
Unatakiwa kuwa mwangalifu katika kuchagua vipindi , kama unachagua redio au televisheni ; kuna TAARIFA YA HABARI ambayo , hutumia LUGHA RASMI ili uweze KUJIFUNZA MANENO YANAYOTUMIKA KATIKA REJISTA MBALIMBALI ZA LUGHA. Lakini chagua vipindi vya DRAMA , yaani MICHEZO YA KUIGIZA. Utajifunza LUGHA ikizungumzwa katika mazingira yake halisi--- NATURAL SETTING. Matamshi , mwitiko na uteuzi wa lugha unaondana na mazingira.SIKILIZA VIPINDI VYA DINI , SHULE , SAYANSI , UCHAMBUZI na kadhalika ili uweze kupata MISAMIATI MBALIMBALI KWA AJILI YA KUKUSAIDIA.
HITIMISHO
----Kama unajifunza LUGHA YA KIGENI , fanya marudio , mazoezi mengi na soma vitabu vingi vya hadithi vya lugha hiyo.
-----Soma ukiwa na KAMUSI na tafuta maana ya neno usilolijua.
----Jizoeze KUSIKILIZA na KUONGEA ukiwaiga wajuao ujifunzapo lugha ya kigeni.
-----Sikiliza MIHADHARA na REDIO ili ujifunze kwa wengine wanavyotamka maneno.
-------Jikumbushe MANENO magumu kila siku.
------Kila nafasi unayoipata itumie kwa kusoma.
------Pambana na SARUFI za LUGHA YA KIGENI kikamilifu.
------Jifunze lugha ya kigeni kwa kuongea mara kwa mara.
Asante sana wadau wangu hasa WANAFUNZI wangu kwa kusoma makala hii nzuri sana kama utaweza mwonyeshe mwenzako naye asome apate kuelewa jinsi ya kukuza lugha ya kiingereza na lugha nyingine.
Makala hii imeandikwa na MWL PRUDENCE KAIJANANTE , GEITA , TANZANIA ,AFRIKA YA MASHARIKI anapatikana kwa namba +255 755840352 , EMAIL: prudencekaijanante@yahoo.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment