Search This Blog
Sunday, 22 January 2017
MBINU ZA KUSOMA NA KUFAULU MITIHANI
Kila mzazi angependelea mwanae afanikiwe katika masomo na kufaulu mitihani yake. Pia kila mwanafunzi anahitaji KUFAULU katika mitihani yake . Walimu nao hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika mitihani yao.
KUFAULU mtihani ni muhimu kwa malengo ya mwanafunzi , kwani anaposhinda mitihani humwezesha kuwa na mtazamo wa juu kielimu , kwa mfano KUPATA CHETI , DIPLOMA AU DIGRII, kitu ambacho humfanya afae kwenye KAZI. Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwa baadhi ya WANAFUNZI kumudu MASOMO na mitihani yao. WAKATI HUO HUO wapo baadhi yao ambao wao KUFAULU MITIHANI si tatizo.
Sasa mtu anaweza kujiuliza , kwa nini WANAFUNZI wengine WASHINDWE na wengine WAFAULU vizuri katika Masomo NA MITIHANI yao ? MAFANIKIO katika MASOMO na KUFAULU MITIHANI kunahitaji UWEZO WA ASILI , KUFANYA KAZI KWA BIDII na KUFUATA KANUNI NA MBINU ZA KUSOMA.
Wanafunzi wengine huona ugumu katika MASOMO na KUFAULU MITIHANI , si kwa sababu hawana akili , bali hawafuati MBINU na KANUNI fulani za KUSOMA na KUFAULU MITIHANI. WANAFUNZI wengi wana uwezo mzuri , kama watajifunza mbinu hizi.
Mbinu na kanuni hizi zinazweza kutumiwa na wanafunzi wa SHULE ZA MSINGI , SEKONDARI , VYUO na hata VYUO VIKUU.
KANUNI ZA KUSOMA
{1}. Weka LENGO maalumu la KUSOMA kila siku na litimize.
{2}. Jiandae kwa mtihani kila wakati , usingoje mwalimu atangaze kuwa ataleta mtihani ndipo usome. SOMA KILA SIKU.
{3}.Weka RATIBA ya kila somo na ifuate.
{4}.Tenga muda wa kutosha kwa kila somo.
{5}.Uwe na mahali maalumu pa kusomea.
{6}.Epuka kitu chochote kinachoweza kukufanya usisome vizuri.
{7}.Tafuta mahali pasipo na kelele za aina yoyote.
{8}.Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja.Kwa mfano , MAPENZI au ANASA ZA KIMWILI wakati ungali mwanafunzi.Hivyo ni vikwazo masomoni.
{9}.Jijengee tabia njema ya kujizuia katika tama za mwili.
{10}. Fanya MAZOEZI ya mwili mara kwa mara.
{11}.Jiwekee MUDA wa kutosha kila siku kwa ajili ya kazi za utoaji taarifa za MASOMO na PROJEKTI.
{12}.Ni jambo la busara kuwa na usiku mmoja wa kumpumzika katika juma ambayo si Jumapili au Jumamosi.
{13}.Ni muhimu kujihusisha na watu wengine , jambo hili litakufariji kimawazo.
WAKATI WA KUJISOMEA
{14}. Kabla hujaanza kujisomea , hakikisha kuwa zana zote muhimu kwa kusomea zipo.
{15}.Epuka vishawishi vinavyoewza kukufanya uairishe KUJISOMEA.
{16}.Tafuta mahali pasipo na kelele za aina yoyote.
{17}.Hakikisha kuwa mahali pa kusomea pana mwanga wa kutosha.
{18}.Usisome mambo mengi kwa wakati mmoja.
{19}.Epuka kusoma hadi usiku sana; utaharibu afya yako.
{20}.Jisomee katika MUDA unodhani unafaa zaidi.
{21}.Epuka KUSOMA ukiwa umejilaza kitandani.
{22}.Uwe na MUDA wa KUPUMZIKA kila unapochoka KUSOMA.
{23}.Uwe na muda mwingi wa KUJISOMEA kila siku , usipoteze MUDA kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile MAONGEZI.
UNAPOKUWA SHULENI / CHUONI / DARASANI FANYA YAFUATAYO
{24}. Fika darasani kwa wakati unaotakiwa ili usikose MAAGIZO.
{25}. Usikose kipindi bila sababu maalumu.
{26}.Wakati mwalimu hajafika darasani , pitia yale uliyojifunza kipindi kilichopita.Soma kazi zako zote za darasani kabla ya kuanza darasa.
{27}.Wakati Mwalimu anafundisha darasani SIKILIZA KWA MAKINI kile anachofundisha na mwangalie machoni mwalimu usiangalie pembeni .
{28}.Baada ya kipindi , pitia yale uliyojifunza.
{29}.Chunguza masomo yako ili ujue udhaifu wako uko wapi.
{30}.Jenga tabia ya UVUMILIVU na kamwe usikate tama wakati ugumu unapoibuka masomoni.
{31}.Jenga tabia ya kupania KUFAULU katika MASOMO yako. AMINI KUWA UTAFAULU.
{32}.Usiwe MWANAFUNZI wa kukaa tu darasani, ULIZA na JIBU MASWALI yanapoulizwa.
{33}.Epuka kukaa kimya na nyuma ya darasa , bali shiriki katika mazungumzo ya darasani na wenzako.
{34}.Ni vizuri pia kuwa na MWENZAKO wa kujadili naye.
{35}.Uwe MWANAFUNZI mdadisi wa mambo kwa walimu na hata kwa wanafunzi wenzako pia.
{36}. Wasilisha kazi za darasani kwa wakati wake.
{37}.Unapokuwa na matatizo kimasomo, mwone mwalimu , anayehusika.
{38}.Hudhuria shughuli zote za shule nje ya darasani.
{39}. Jenga uhusiano mzuri kwa walimu wako na kwa wanafunzi wenzako.Ukiwa na AMANI moyoni , utasoma na kuelewa. JISTAHI na KUWAPENDA walimu wako. Ukimpenda mwalimu utalielewa vzuri somo lake.
{40}.Epuka marafiki wabaya wenye nia ya kukupotosha.
{41}. Epuka POMBE , UVUTAJI WA SIGARA , BANGI na MADAWA YA KULEVYA.Huharibu ubongo na kudhoofisha afya.
KABLA YA MITIHANI FANYA HAYA
{42}.Kabla ya mtihani , SOMA KWA BIDII SANA usingoje mtihani umekaribia ndipo usome.
{43}.SOMA kwa mpangilio kila siku ili KUJIANDAA kikamilifu kwa MTIHANI.
{44}.USIKU unaofuatiwa na siku ya mtihani uwe na MUDA WA KUTOSHA WA KULALA.
KULALA.Usisome hadi usiku wa manane.
SIKU YA MITIHANI FANYA HAYA
{45}.Siku ya mtihani , usifikirie kushindwa bali uwe na IMANI kuwa utashinda.ONDOA WASIWASI NA MASHAKA.
{46}.Wahi kwenye chumba cha mtihani kwani kuchelewa huleta HOFU.
{47}.Chukua vifaa vyote muhimu katika mtihani kama vile kalamu, penseli na rula.
{48}.Soma MAAGIZO YA MTIHANI kwa uangalifu sana, na hakikisha uko makii kwa kile unchotakiwa kufanya kabla ya kujibu swali lolote
{49}. Kabla hujaanza kujibu maswali , angalia maswali ambayo ni rahisi kwako kujibu.
{50}.JIBU maswali rahisi kwanza na kwa haraka ili upate MUDA wa kutosha kujibu maswali magumu.
Asante sana wanafunzi wangu wa SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI, VYUO na VYUO VIKUU kwa kusoma makala hii nzuri sana. Mwandishi wa makala hii ni MWL JAPHET MASATU , anapatikana kwa + 255 716 924 136 , EMAIL, japhetmasatu@yahoo.com , DAR ES SALAAM, TANZANIA, AFRIKA YA MASHARIKI.
MUNGU AWABARIKI WOTE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment