Search This Blog
Sunday, 22 January 2017
SUNDAY, JANUARY 22, 2017 Wabunge waliosimamishwa waweka mikakati
Kwa ufupi
Wabunge watano kati ya hao waliopigiwa simu wamesisitiza kwamba wataendelea kubainisha jinsi bajeti iliyotengwa na Serikali wakati wanasimamishwa ilivyo na changamoto za utekelezwaji wake.
ADVERTISEMENT
By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Wabunge wanane waliokuwa wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda na makosa tofauti wanatarajiwa kurejea kwenye chombo hicho cha kutunga sheria mwisho wa mwezi huu baada ya kumaliza kutumikia adhabu zao huku baadhi yao wakiahidi kuendeleza moto wa bajeti.
Wabunge watano kati ya hao waliopigiwa simu wamesisitiza kwamba wataendelea kubainisha jinsi bajeti iliyotengwa na Serikali wakati wanasimamishwa ilivyo na changamoto za utekelezwaji wake.
Mei, 2016 Bunge kupitia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipitisha azimio la kuwasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliodaiwa kufanya vitendo vya vurugu ndani ya ukumbi na kudharau mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.
Wabunge hao ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), John Heche (Tarime), Halima Mdee (Kawe), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Pauline Gekul (Babati), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Ester Bulaya (Bunda) ambao adhabu yao ilitokana na kitendo chao cha kupinga msimamo wa Spika kuhusu Bunge kuonyeshwa ‘live’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment