Donald Trump alishinda urais baada ya kusema kuwa atafanya mabadiliko makubwa kuhusu mahusiano ya nchi yake na nchi nyingine duniani. Je kuingia kwake katika ikulu ya White House kuna maana gani kwa nchi tofauti za Afrika ?
Afrika Kusini- na Pumza Fihlani
Afrika kusini imeweza kujiweka katika hali ya nchi ambayo haihitaji misaada bali mshirika mwenye uwezo na anayejiamini kibiashara . Lakini mazungumzo magumu na Marekani kuhusu makataba wa fursa ya ukuaji wa kiuchumi wa Afrika (AGOA) mwishoni mwa mwaka jana huenda yalikuwa ukumbusho kwa nchi zinazoendelea kuhusu mahala halisi zilipowekwa kiuchumi na Marekani.
Baaadhi ya wakosoaji wa Mapatano ya AGOA wanasema Afrika kusini, kama mataifa mengi ya Afrika, ilikuwa ngao thabiti katika kukubali masharti ambayo hayainufaishi kwa minajili tu ya kupata mshirika thabiti.
Bwana Trump ana sifa ya kuwa mfanyabiashara maarufu, na huku haijawa wazi ni sera gani aliyo nayo kwa Afrika kusini, baadhi nchini humo wana hofu kuwa huenda uhusiano mzuri iliyokuwa nayo nchi yao na Marekani ukavunjika. Wanasema utawala wa mfanyabiashara huyo huenda ukaitaka Afrika Kusini kuonnyesha ni kwa nini inafaa kuwa katika kikosi cha Bwana Trump.
Nigeria - na Naziru Mikailu
Tangu kuchaguliwa kwa rais Muhammadu Buhari mwaka jana , Nigeria imeboresha uhusiano na Marekani uliotiwa dosari kubwa na shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya jeshi la Nigeria, hususan katika vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram . Jeshi la Nigeria lilipata mafunzo na zana kutoka kwa utawala wa Obama na bila shaka itataka kuendeleza uhusuiano huu ulioboreka. Nigeria pia itataka uhusiano wa kibiashara na taifa lililoimarika zaidi kiuchumi duniani.
Kwa upande mwingine nchi hizi mbili zinaweza kujikuta katika uhasama ikiwa Bwana Trump ataamua kuwatambua waasi wanaotaka kujitenga wa Biafra. Pia inasemekana kuna raia wa Nigeria zaidi ya milioni moja wanaoishi nchini Marekani , na baadhi wanahofu kwamba sera za uhamiaji za Bwana Trump zinaweza kupelekea maelfu yao kurejeshwa nyumbani.
Uganda - na Catherine Byaruhanga
Serikali ya Marekani hutoa msaada wa dola milioni mia saba ($700m) kwa Uganda kila mwaka. Mingi kati ya misaada hiyo huelekezwa katika mipango ya kuboresha afya, hususan dawa utoaji wa dawa za bure za HIV/Aids kwa wale wanaozihitaji. Kiasi cha pesa kisichojulikana pia hutolewa kwa ajili ya msaada wa jeshi. Hakuna maelezo yanayotolewa lakini kutokana na kwamba Uganda imeongeza kikosi cha askari wake wa kulinda amani katika mataifa ya kigeni, ikiwemo Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, serikali ya Washington imekuwa mfadhili wake mkuu. Marekani pia imekuwa ikitoa msaada wa mafunzo kwa wanajeshi.
Katika barua ya hivi karibuni kwa Wizara ya Mashauri ya Kigeni, maafisa wa mpito wa Bwana Trump walihoji kuhusu shughuli hizi. Hofu ya Uganda ni kwamba utawala mpya utasitisha ama kupunguza msaada huu .Kwa upande mwingine baadhi ya wapinzani wamedai kuwa wafadhili wa kimataifa hawakuipatia serikali msaada unaofaa. Katika sekta ya afya , kupunguzwa kwa msaada kunaweza kuwaacha wengi mashakani.
Kenya and Somalia - na David Wafula
Takriban theluthi moja ya Wakenya 90,000 wanaoishi Marekani ni wahamiaji haramu, kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Pew . Hii inamaaninsha kuwa zaidi ya watu 30,000 wanaweza kurejeshwa nchini Kenya kama Donald Trump atatekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni ya kuwarejesha makwao wahamiaji haramu. Hii itaathiri kwa kiasi kikubwa kipato chao wanachotuma nyumbani kinachokadiriwa kuwa dola milioni sitini ($60m ) kutoka Marekani na Canada mwaka 2015.
Walipokuwa wakitathmini uhusiano baina ya Marekani na Kenya pamoja na Afrika kwa ujumla maafisa wa mpito wa Bwana Trump walielezea hofu yao kuhusu hali ya baadae ya ushirikiano huo. Walihoji ni kwanini Marekani imekuwa ikipigana na al-Shabab kwa muongo mzima bila kushinda vita hivyo. Na walihoji ikiwa pesa ambazo Washington inatoa kama msaada kwa nchi mbali mbali za Afrika zinatumiwa kwa kwa umakini.
Zimbabwe - na Shingai Nyoka
Serikali ya rais Robert Mugabe imesema inatumaini mabadiliko ya hali iliyowezoweleka yanaweza kuisasidia kurejesha uhusiano baina yake na Washington. Bwana Mugabe, baadhi ya maafisa wake na baadhi ya makampuni yanayomilikiwa na serikali yanakabiliwa na vikwazo vya kusafiri nchini Marekani na kiuchumi tangu wakati wa utawala wa rais George W Bush' kufuatia mnadai ya ukiukaji wa haki za binadamu. Bwana Mugabe anaamini vikwazo hivyo vinakiuka sheria. Hata hivyo bado Trump hajatoa tamko lolote kuhusu Zimbabwe ama Bwana Mugabe na hakuna ishara yoyote kwamba msimamo wake kwa Zimbabwe utatofautiana na ule waliokuwa nao watangulizi wake.
No comments:
Post a Comment