NAIBU waziri Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Selemani Jaffo ameshangazwa na baadhi ya watumishi pamoja na wakuu wa idara katika Halmashauri ya mji wa Geita kutumia fedha zinazoletwa kwa ajili ya Miradi kwa kujenga majengo makubwa Mkoani Mwanza baada ya kuzitumia kwa miradi ya maendeleo.
Ametoa kauli hiyo kwenye ziara yake ya siku moja Mkoani humo ilikuwa na lengo la kukagua Shuguli za maendeleoa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Jaffo akionekana kukerwa na watumishi na baadhi ya wakuu wa idara Halimashauli hiyo amesema Fedha zinazoletwa na kukusanywa ndani ya Halmashauri hiyo zinafanya kazi binafusi za kujenga magorofa Mkoani Mwanza.
Joffo ameongeza kuwa Ofisi yake imefanya uchunguzi wa awali katika Halimashauli hiyo na kukuta fedha za miradi zimetumiwa kinyume na utaratibu wa kisheria.
Joffo ameongeza kuwa Ofisi yake imefanya uchunguzi wa awali katika Halimashauli hiyo na kukuta fedha za miradi zimetumiwa kinyume na utaratibu wa kisheria.
Hivi kalibuni wakati wa ziara yake Mkoani humo Waziri Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa George Sembachawene aliuagiza uongozi wa Mkoa wa Geita kuchunguza na kuwakamata watumishi waliotafuna milioni 200 kati ya Bilioni 2.5 zilizoletwa kwa ajiri ya kujenga Halimashauli ya mji.
Mkoa wa Geita umeletewa kiasi cha bilioni 1.8 kwa ajili ya kujenga Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo jambo ambalo mpaka sasa hata kiwanja bado.
No comments:
Post a Comment