Search This Blog

Sunday, 22 January 2017

MAANDALIZI YA UFUNDISHAJI-1

MAANDALIZI YA UFUNDISHAJI
Kabla ya kufundisha unahitaji maandalizi ya kutosha, Ipo miongozo maalumu iliyoandaliwa ya kutuongoza kutengeneza azimio la kazi na andalio la somo la Kiswahili kwa shule za msingi. Mitazamo hii inabadilika kutokana na nadharia na mahitaji ya elimu nchini. Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya mtazamo wa ufundishaji, mkazo umekuwa kwenye ujenzi wa maana hivyo msisitizo umekuwa kwenye kujenga ujuzi.
AZIMIO LA KAZI
Ni mpangilio au utaratibu unaomwezesha mwalimu kuchanganua muhtasari wa somo na kupanga mada na jinsi atakavyozifundisha katika kipindi cha wiki , mwezi, na muhula.Ni mpango wa ufundishaji kwa kipindi fulani.
Umuhimu wa azimio la kazi
Humsaidia mwalimu kwenda na mtiririko mzuri wa mada.
Humwonyesha mwalimu muda wa kufundisha kila mada.
Huonyesha zana/vifaa/njia ya kumsaidia mwalimu katika ufundishaji wake.
Kuonyesha malengo ya ufundishaji wa somo hilo katika muda aliopanga.
Wakati wa kuandaa andalio la somo kuna mambo ambayo yanatakiwa kuzingatiwa,
Kuangalia kalenda au ratiba ya shule ambayo itakuongoza katika kuandaa azimio lako la kazi kwa kigezo cha muda.
Kusoma kwa makini muhtasari wa somo la kiswahili na kuweza kubaini mada, malengo , zana, na ujuzi ambao utatakiwa wanafunzi wako waupate katika mada husika.
Kuhakikisha kwamba vifaa vya muhtasari, vipo na vinatosheleza mfano, vitabu vya kiada, vitabu vya ziada, kiongozi cha mwalimu, kitabu cha mwalimu, na kitabu cha mwanafunzi.
VIPENGELE VYA AZIMIO LA KAZI
Ujuzi ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
Katika kusoma ujuzi uliopo katika muhtasari wa somo la kiswahili , inakupasa kujua ujuzi ni upi, na maudhui ni yapi, kwani ujuzi huohuo huweza kujengwa na maudhui mengine.
Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi. Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji ambao ni ujuzi.
Malengo mahsusi lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua, kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha n.k. Viwango vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
Sifa za malengo mahsusi : – Ni lazima libebe kitendo kinachopimika wakati unapofundisha.
– Malengo yahusiane na kiwango cha uwezo wa mwanafunzi.
– Muda wa malengo utajwe waziwazi
– Kiwango cha kufikia kila lengo kiwezeshwe.
– Kipindi kimoja kisiwe na malengo mengi.
Mwezi na Wiki Katika kugawa muda unatakiwa kuzingatia idadi ya vitendo vitakavyofanyika ili mwanafunzi ajenge ujuzi. Kuna baadhi ya vitendo vinahitaji muda mrefu na vingine vinahitaji muda mfupi kukamilika.
Vipindi Idadi ya vipindi itazingatia na uzito na wigi wa vitendo katika mada husika. Jiulize vitendo vya kiwango cha juu vina uzito sawa na vitendo vya kuchunguza? Katika muhtasari umepewa muda wa idadi ya ya jumla ya vipindi kwa mada kuu, hakikisha kuwa umevigawa kwa uwiano sawa kulingana na vitendo.
Vitendo vya Ufundishaji Kumbuka unapoandika vitendo vya ujifunzaji wewe ni mwezeshaji/wewe ni msaada kwa mwanafunzi wako katika utendaji wake. Katika kuandika vitendo nya ufundishaji unatakiwa kuonyesha yale matendo yote utakayoyafanya mwalimu pamoja na mifano katika uwezeshaji wako.
Vitendo vya ujifunzaji Unapoandika vitendo vya ujifunzaji unatakiwa uvichukue ndivyo vitendo vya msingi vitakavyoleta kujengwa ujuzi. Lugha itakayotumika ionyeshe kuwa mtendaji mkuu ni mwanafunzi. Mfano Wanafunzi, kuchora, kueleza,Kujibu maswali ya mwalimu, kujadiliana,kutafsiri,kueleza, kusoma, kujadili, kufupisha n.k
Vifaa/zana Matumizi ya zana katika kujifunzia na kufundishia ni nyenzo muhimu sana kwa sababu inatumika katika ujenzi wa maana kwa kile mwanafunzi atakachojifunza. Vilevile zana humsaidia mwalimu katika kumrahisishia kazi yake ya kufundisha.
Rejea, Mwalimu atapaswa kuonesha vitabu vya rejea katika mada atakayoifundisha, Kumbuka rejea siyo vitabu tu, bali inahusisha vitu vingine kama majarida, magazeti,vipeperushi, vipindi vya redio, kanda za video, chati na makala mbalimbali na intaneti.
Upimaji, katika upimaji tunaangalia ufanisi wa ujifunzaji na ufundishaji uliofanyika katika malengo mahsusi. Upimaji huu unahusu vitendo hivyo vimefanyika kwa kiasi gani kuleta ujuzi. Mfano, mwalimu anaangalia ni jinsi gani vitendo vya ufundishaji na ujifunzaji vimefanikiwa.
Maoni, Inahusu hatua au ushauri utakaouchukua baada ya kufanya upimaji.
Mfano wa muundo wa azimio la kazi
Jina la mwalimu :………………. Mwaka:………………………..
Shule: …………….. Muhula:…………………………
Somo: ……………… Darasa:……………………………..
Ujuzi
Malengo
mwezi
wiki
Mada kuu
Mada ndogo
vipindi
v/ufundishaji
v/ufundishaji
vifaa/zana
rejea
Upimaji
maoni
Andalio la somo: Ni utaratibu au mpangilio wa hatua za kufundishia unaotayarishwa na mwalimu kwa kipindi husika kwa darasa fulani./ ni dira ya kumwongoza mwalimu wakati wa kufundisha.
Umuhimu wa andalio la somo.
Huonyesha wazi malengo ambayo mwalimu anatarajia yafikiwe na mwanafunziwake wakati wa kipindi.
Humwongoza mwakimu kufundisha kwa hatua anapokuwa darasani.
Humwonyeshab mwalimu vitendo vya kufanya wakati wa ujifunzaji na ufundishaji.
Vipengele vya andalio la somo
Chati itakayoonyesha taarifa za awali , Tarehe, darasa, kipindi/somo, muda,idadi ya wanafunzi waliopo na wasiopo.
Ujuzi : ni uwezo wa kufikiri, na kutenda anaoyarajiwa aujenge mwanafunzi kwa kupitia mada/maudhui kwa ushirikiano wa mwalimu na mwanafunzi, mwanafunzi na mwalimu, mwanafunzi na mazingira yake.
Ujuzi hujengwa kwa vitendo vinavyojitokeza katika malengo mahsusi. Vitendo vya malengo mahsusi ndivyo vinavyoleta matokeo ya ufundishaji na ujifunzaji ambao ni ujuzi.
Mada na mada mada ndogo : Hizi ni mada kuu na mada ndogo ambazo zimeonyeshwa kwenye muhtasati wa somo.
Lengo kuu: Ni lengo la jumla ambalo mwalimu anatarajia wanafunzi wake kulifikia katika ufundishajina ujifunzaji.
Malengo mahsusi: lengo ni lazima libebe kitendo kitakachowezesha ujuzi kutokea. Mada ndogo inaweza ikawa na malengo mengi yakibeba vitendo mbalimbali vitakavyotumika kujenga ujuzi.
Katika kuunda malengo ni vizuri ukazingatia vitendo vya kiwango cha juu vya kufikiri na kutenda kama , kueleza,kuchambua, kuunda,kuchanganua, kutofautisha, kutathmini, kubuni , kubainisha,kuhusianisha n.k. Viwango vya chini vya kufikiri na kutenda ni kutaja,kuorothesha,kuonyesha n.k kwa hiyo kazi ya mwalimu ni kumsaidia mwanafunzi kuinua kiwango chake cha kuunda vigezo vya kufikiri na kutenda.
Jedwali linaonyesha hatua za ufundishaji.
– utangulizi: Utangulizi ndio hatua ya kwanza ya somo, mada unayotaka kufundisha haipo mbali sana na maisha ya mwanafunzi, ni vema kama mwalimu ukaanza mada yako kwa kutafuta maarifa ya awali aliyonayo mwanafunzi.
Ni vema kufahamu wanafunzi wana maarifa na uzoefu gani kuhusu kile utakachokwenda kukifundisha.Lengo ni kuanza kwa kile wanachokifahamu wanafunzi kisha kuelekea kile kipya, Kwa hiyo kile kile wanachokifahamu kitakuwa ni msingi mzuri ambao kile kipya watakachojifunza kitaleta ujuzi. Mfano unaweza ukatumia njia ya bungua bongo, maswali na majibu au changanya kete kutafuta maarifa ya awali kwa mwanafunzi.
– Ujuzi mpya: Katika hatua hii Mwalimu anahitaji kufikiri kwa kina kuhusu stadi na maarifa atakayotumia mwanafunzi katika kujenga ujuzi unaotarajiwa. i.e Kuwaongoza wanafunzi kufanya
vitendo mbalimbali vilivyopo kwenye vitendo vya ujifunzaji ili kuweza kujenga maarifa mapya.
-Kuimarisha maarifa: Katika hatua hii inampasa mwalimu kuwashirikisha wanafunzi katika kuunganisha maarifa waliyojifunza ili kuwe na mshikamano wa dhana husika.
– Tafakuri : Mwalimu uwaongoze wanafunzi wako kutafakari jinsi maarifa waliojifunza yanavyohusiana na maisha yao na ujuzi wanaotarajiwa kuujenga. Vilevile kupima ufanisi au udhaifu wa ujifunzaji na ufundishaji.
-Hitimisho: Mwalimu tafuta njia mbalimbali za kuhitimisha somo lako, mfano kutumia maswali yanayohitaji majibu mafupimafuipi kwa kile walichojifunza, kumhitaji kila mwanafunzi kubainisha dhana muhimu alizojifunza.
– Vitendo vya upimaji, Ni tendo linalifanyika mfululizo toka mwanzo hadi mwisho wa somo. Ni ukweli kwamba utakuwa umeandaa vitendo vya kupima kila hatua ya mada yako. Lakini kuna uwezekano wa kubadili vitendo vya upimaji kulingana na jinsi somo linavyoendelea.
-Tathmini: Tathmini inahusu ufanisi wa somo unaotokana na matokeo ya vitendo vya upimaji katika mfululizo wa hatua nzote za somo. Tathmini ya mwanafunzi inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ujifunzaji Mfano mwalimu anaweza kuwauliza wanafunzi maswali yafuatayo , ni mambo gani mmeyapenda katika hii mada, mambo gani hamkuyapenda, na uwaagize watoe sababu kwa majibu waliyoyatoa, mnahitaji msaada gani ili muelewe zaidi? Au wagawie vikaratasi waandike maoni yao kuhusu mada iliyofundishwa na tathmini ya mwalimu inatoa picha ya ufanisi wa vitendo vya ufundishaji, Tafakari ya matokeo ya upimaji uliofanya katika hatua zote za somo na matokeo ya tathmini ya mwanafunzi.
-Maoni: Maoni yanatolewa baada ya tathmini, Mwalimu atabainisha mambo yatakayowezesha kuboresha ujifunzaji wa somo. Mfano, kwa wale ambao hawakuweza kufikia ujuzi uliotarajiwa utatumia mbinu gani kuwasaidia, au maoni /ushauri kuhusu namna ya kuboresha ufundishaji na ujifunzaji wako.
Muundo wa andalio la somo.
TAREHE
DARASA
KIPINDI
MUDA
IDADI YA WANAFUNZI
IDADI YA WANAFUNZI
IDADIWALIOHUDHURIA
IDADI YA WALIOANDIKISHWA
ME
KE
JML
ME
KE
JML
Ujuzi…………………………
Mada kuu………………………………………
Mada ndogo…………………………………..
Lengo kuu……………………………………….
Lengo mahsusi……………………………..
Zana/vifaa:…………………………………………..
Rejea:…………………………………………….
Hatua za somo
Tarehe
Vitendo vya ufundishaji
Vitendo ufundishaji
Vitendo ujifunzaji
utangulizi
Ujuzi mpya
Kuimarisha maarifa
Tafakuri
Hitimisho
Tathmini ta wanafunzi…………………………………………..
Tathmini ya mwalimu…………………………………………….
Maoni………………………………………………………………
KUMBUKUMBU ZA SOMO/SHAJARA LA SOMO.
Ni muhtasari unaotayarishwa na mwalimu wa somo kuonyesha mada kuu na mada ndogo alizofundisha,wakati alipofundisha, na jina au sahihi yake. Pamoja na kumbukumbu hii, mwalimu ana kumbukumbu zingine zinazotumika kama rejea za kazi alizofanya. Mfano nukuu za somo, andalio la somo, azimio la kazi.
Umuhimu wa kumbukumbu za somo.
Huonyesha mambo yaliyofundishwa na wakati yalipofundishwa.
Mwalimu huweza kupima kiasi cha mada alizokwisha kufundisha kwa kulinganisha na azimio la kazi.
Humwelekeza mwalimu mpya mahali pa kuanzia.
Huweza kupima muda uliotumika katika ufundishaji wa mada ukilinganisha na azimio la kazi.
MUUNDO WA SHAJARA LA SOMO
MWEZI
Wiki
MADA KUU
MADA NDOGO
TAREHE
KUANZA
TAREHE
KUMALIZA
MADA ZILIZOFUNDISHWA
SAHIHI NA MAONI YA MWALIMU WA SOMO
SAHIHI NA MAONI YA MKUU WA IDARA.
SAHIIHI NA MAONI YA MKUU WA SHULE
Jan
1,2
Fasihi
Fasihi simulizi
1/1/2012
15/1/2012
-maana ya fasihi
-dhima ya fasihi simulizi
– vipengele vya fasihi simulizi

No comments:

Post a Comment