Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

TARATIBU ZA UHAMISHO WA MTUMISHI

TAARIFA YA UHAMISHO WA WATUMISHI WALIOOMBA KUHAMA KWA
KIPINDI CHA JANUARI JUNI KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA
MITAA, TANZANIA BARA
1.0 Utangulizi
i. Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002
ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003
Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi
Ya RaisMenejimenti
ya Utumishi wa Umma na
ii. Kwa maelekezo ya Ofisi ya RaisMenejimenti
ya Utumishi Wa Umma kwa
barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na.
C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika
Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
yamekasimiwa kwa;
a. Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kwa watumishi
wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
b. Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka
Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;
c. Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja
kwenda kingine ndani ya Halmashauri.
OWMTAMISEMI,
imeendelea na utaratibu wake wa kushughulikia maombi ya
Uhamisho kwa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mwezi Juni na
Desemba kila mwaka. Maombi yanapokelewa kuanzia mwezi Januari mpaka Juni
hushughulikiwa mwezi Juni na maombi yaliyopokelewa kati ya Julai mpaka Desemba
hushughulikiwa mwezi Disemba.
Ukurasa wa 1 kati ya 2
2.0 Vigezo vya Kuzingatia
Ili maombi ya Uhamisho yaweze kukubaliwa, mtumishi hupaswa kutimiza vigezo
vifuatavyo;
a. Kupatikana kwa Nafasi Wazi
Mwombaji aandike barua ya maombi na kujibiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri
yenye nafasi ya kumpokea. Aidha, Wakurugenzi wataeleza nafasi wazi ya Uhamisho
ilivyopatikana (mfano, Mtumishi aliyestaafu/kufariki kwa Jina na ‘Check Number’
yake, au watumishi walioomba kubadilishana vituovya kazi, nk)
b. Kupata Ridhaa ya Mamlaka ya Ajira
Maombi yaliopitishwa na Mkuu wa Idara/Taasisi (mfano Mkuu wa Shule pamoja na
Afisa Elimu, au Mkuu wa Idara za Afya, Maendeleo ya Jamii, Ardhi Maliasili na
Mazingira, nk) yatawasilishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambayo
mtumishi/mwombaji anataka kuhama ili kupata ridhaa yake. Barua ya uhamisho
inatakiwa kusainiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri mwenyewe.
c. Kuomba Kibali cha Katibu Mkuu OWMTAMISEMI
Barua za uhamisho zinapaswa kuwasilishwa OWMTAMISEMI
na Makatibu Tawala
wa Mikoa kwa maandishi katika vipindi viwili tarehe 30 Septemba na tarehe 15
Desemba kwa uhamisho wa mwezi Desemba na tarehe 30 Machi na tarehe 15 Juni
kwa uhamisho wa mwezi Juni. Barua za ridhaa ya Mkurugenzi wa Halmashauri
anayotaka kuhama na barua ya Mkurugenzi wa Halmashauri itakayompokea
zitawasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa. Ni muhimu mtumishi ataje cheo chake
wakati anawasilisha maombi yake.
d. Viambatanisho Muhimu
Watumishi wote walioomba kuhama, wanatakiwa kuambatisha, nakala ya
kitambulisho cha kazi, Check Namba, anuani ya barua pepe ya mwombaji
kama ipo, sanduku la posta la Ofisi au binafsi pamoja na namba ya simu ya
mkononi.
Ukurasa wa 2 kati ya 2
3.0 Namna ya Kupata Majibu toka OWM TAMISEMI
Vibali vya Uhamisho kwa watumishi walioomba uhamisho na kukidhi vigezo (kama
ilivyooneshwa kwenye orodha) kwa kipindi cha kati ya Juni mpaka Disemba kila
mwaka watapewa Vibali vya Uhamisho kupitia Ofisi za Wakurugenzi wa
Halmashauri wanakohama. Aidha, maombi ambayo hayakukidhi vigezo, pia
yatajibiwa kupitia ofisi za Wakurugenzi hao.
4.0 Uhamisho wa Juni, 2013
Katika kipindi kinachoishia Juni 2013, maombi kadhaa hayakuzingatia utaratibu
ulioelekezwa pamoja na kughushi barua na hivyo kuchelewesha zoezi la uhamisho
kwa watumishi. Barua zote ambazo hazikufuata utaratibu ulioelekezwa zilirudishwa
kwa Wakurugenzi kupitia kwa Makatibu Tawala wa Mikoa. Barua
zilizoshughulikiwa katika kipindi hiki ni zile tu ambazo zimerejeshwa kwa kuzingatia
utaratibu ulielekezwa. Barua zote ambazo ziliwasilishwa baada ya tarehe 30 Juni
2013, zitajumuishwa katika barua zitakazopokelewa kati ya Julai – Disemba 2013 na
kushughulikiwa mwezi Disemba 2013.
5.0 Muda wa Kufuatilia Majibu
Waombaji wanashauriwa kufuatilia majibu ya maombi yao, kupitia ofisi za
Wakurugenzi wao kuanzia wiki ya pili ya mwezi Julai, 2013.
OWMTAMISEMI
imetuma barua zote za waliokidhi vigezo kwa waajiri. Kwa
Matokeo zaidi ya Maombi ya Uhamisho, tafadhali tizama tovuti ya OWMTAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz
OWM TAMISEMI INAWASHUKURU WATEJA WOTE KWA USHIRIKIANO
ORODHAYA WATUMISHI WALIOKIDHI NA WASIOKIDHI VIGEZO VYA
UHAMISHO WATUMISHI WOTE WALIOOMBA KUHAMIA MAMLAKA
MBALIMBALI ZA SERIKALI ZA MITAA JUNI,
2013
Ukurasa wa 3 kati ya 2

No comments:

Post a Comment