Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

MUDA WA ZIADA KAZINI

SEHEMU YA SABA VIWANGO VYA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI 57.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma muajiri hatomtaka au kumruhusu mtumishi wa umma kufanya kazi katika muda wa ziada na itakapobidi muda wa ziada hautozidi saa tatu kwa siku. (2) Kazi itakayolazimika kufanywa katika muda wa saa za ziada na ikapelekea kulipwa posho la kufanya kazi hiyo lazima ipatikane idhini ya Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kabla ya kazi hiyo kufanyika. (3) Kiwango cha masaa ya kazi kilichowekwa chini ya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii, kinaweza kuongezwa iwapo kutatokezea dharura au haja ya kufanya hivyo. (4) Pale saa za kazi za ziada zitapofanywa mtumishi atastahiki malipo ya muda wa ziada kama ifuatavyo. (a) kwa siku za kazi za kawaida mtumishi wa umma atalipwa mara mbili ya kiwango anacholipwa kwa saa katika siku ya kawaida ya kazi (mshahara wa mwezi x saa za ziada x 2/22 igaiwe kwa 8). (b) kwa siku za mapumziko na mapumziko ya kitaifa. Mtumishi wa umma atalipwa mara mbili na nusu ya kiwango anacholipwa kwa saa kwa kufaya kazi katika siku isiyokuwa ya mapumziko ya kitaifa, ila malipo haya yatakuwa ni kwa saa nane (mshahara wa mwezi x saa za ziada x 2.5 /22 igaiwe kwa 8). Muda wa ziada katika kazi . 82 (5) Kwa madhumuni ya kifungu hiki watumishi wa ngazi ya uteuzi wa Rais na wale watumishi watakaoainishwa katika muongozo utakaotolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma,hawatostahiki kupata malipo baada ya saa za kazi kwa kuzingatia kwamba shughuli za kikazi baada ya saa za kazi, ni moja kati ya majukumu yake ya kazi.

No comments:

Post a Comment