Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

LIKIZO YA MTUMISHI WA UMMA

58.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni yoyote ya Kanuni hizi. (a) Mtumishi wa umma atastahiki kupewa likizo la siku ishirini na nane za kazi ndani ya miezi kumi na mbili na atastahiki posho la likizo kila baada ya miaka mitatu au kama itakavyofafanuliwa katika matoleo kutoka Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma. (b) Mtumishi wa umma, atakaetumia likizo yake pahala ambapo sipo penye maskani yake ya kawaida atapaswa kutoa anuani ya pahala hapo kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi yake kabla ya kuanza likizo yake. Mabadiliko yoyote ya hapo baadae lazima ayaeleze. (c) Siruhusa kwa mtumishi wa umma kuakhirisha likizo yake ya mwaka kwa madhumuni ya kulimbikiza siku zake za likizo ili achanganye na za mwaka mwengine, isipokuwa kwa dharura maalum iliyokubalika na kwamba kwa vyovyote vile hakuna likizo itakayolimbikizwa kwa njia ya kuaghirisha zaidi ya miaka miwili. Likizo itakayozidi miaka miwili itakuwa imepotea. Likizo la mwaka. 83 (d) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anaweza kumzuilia mtumishi wa umma kwenda likizo kwa maandishi na kwa dharura maalumu kwa muda usiozidi miezi sita. (e) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anaweza kumruhusu mtumishi wa umma aliezuiliwa likizo lake kwa mujibu wa kanuni ndogo (d) ya kanuni hii, kwenda likizo wakati wowote dharura hiyo itakapomalizika na kama miezi sita imepita tokea mtumishi huyo azuiliwe likizo lake na udhuru aliozuiliwa likizo hilo bado unaendelea, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anaweza kuinunua likizo hilo la mtumishi huyo kwa thamani ya mshahara wa mwezi mmoja bila ya posho. (f) Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi anaweza kukatisha likizo la mtumishi wa umma yeyote wakati wowote ikitokea haja ya kufanya hivyo na mtumishi huyo atawajibika kurudi kazini katika tarehe aliyopangiwa na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi. Isipokuwa kwamba, mtumishi aliyekatishwa likizo lake chini ya kijifungu hiki anaweza kukubaliana na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kuendelea na likizo yake udhuru huo utakapomalizika. (2) Mtumishi wa umma aliyekuwepo masomoni kwa mafunzo ya miezi tisa na kuendelea hatochuma likizo lolote katika kipindi atakachokuwa masomoni. 84 (3) Mtumishi wa umma ambaye atasimamishwa kazi na kulipwa nusu mshahara kwa mujibu wa kifungu 84 cha Sheria hatochuma likizo lolote katika kipindi alichosimamishwa kazi. (4) Kwa madhumuni ya kanuni hii, hesabu ya likizo itaanzia pale mtumishi wa umma atakaporipoti kazi baada ya kumaliza likizo lake.

No comments:

Post a Comment