Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

MTUMISHI: LIKIZO YA DHARULA

59.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Kanuni hizi, kila mtumishi wa umma atastahiki likizo la dharura ya muda mfupi kwa malipo kamili katika hali zifuatazo: (a) ikitokea kifo cha mume, mke atastahiki kupata likizo ya miezi minne na siku kumi; (b) ikitokea kifo cha mke, mume atastahiki kupata likizo la muda wa siku saba; (c) ikitokea kifo cha baba au mama au mtoto au dada au kaka, mtumishi atapata likizo la muda wa siku tatu; (d) ikitokea kifo cha baba au mama mkwe atastahiki kupata likizo la siku tatu. (2) Bila ya kuathiri kanuni yoyote katika Kanuni hizi, Mtumishi wa umma anaweza kuomba siku za ziada za likizo ya dharura iwapo atakuwa bado anahitaji kufanya hivyo, isipokuwa kwamba likizo hiyo isizidi siku ishirini na nane katika miezi kumi na mbili. (3) Likizo iliyotolewa katika kanuni ndogo (2) ya kanuni hii, Mtumishi atalazimika kukatwa likizo hilo katika likizo lake alilochuma la mwaka. Likizo ya dharura na ya Muda.

No comments:

Post a Comment