Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

LIKIZO BILA YA MALIPO

63.-(1) Likizo bila ya malipo zitaidhinishwa na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kwa kuzingatia mambo yafuatayo; kwa jambo ambalo halikuorodheshwa hapo chini; Tume ya Utumishi husika ndio itakayohusika na kuidhinisha likizo hiyo. (a) ikiwa Mtumishi wa umma atapata kazi katika Mashirika ya Kimataifa. (b) ikiwa mtumishi atamfuata mume au mke mbali na kituo chake cha kazi ama kwa likizo au kwa kupata uhamisho. (c) ikiwa mtumishi wa umma anataka kujihusisha na siasa. (d) ikiwa mtumishi anataka kuhudhuria maziko au maombolezo ya jamaa yake nje ya Zanzibar. (e) ikiwa mtumishi wa umma mwanawe, baba yake, mama yake au mtu anaemtegemea ni mgonjwa na mtumishi anataka kumshughulikia mgonjwa huyo. (f) ikiwa mtumishi wa umma anataka kumfuata mume au mke aliyepata nafasi ya masomo, nje ya nchi. (g) ikiwa mtumishi wa umma mwanamme au mwanamke ameoa au ameolewa na mume au mke anaeishi nje ya Zanzibar. Likizo bila ya malipo. 90 (h) Wake au waume wa Viongozi wa ngazi za juu (Rais na Makamu wa Rais) ambao ni watumishi wa umma wanaweza kuchukua likizo bila malipo. (i) ikiwa mtumishi atamfuata mume au mke aliyepewa uhamisho na Serikali au aliyeazimwa kwa kazi za nje ya nchi. (2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo (1) ya kanuni hii, muda wa likizo bila ya malipo hautopungua mwezi mmoja na hautozidi miaka mitatu isipokuwa kwamba likizo hiyo inaweza kuongezwa kwa kipindi cha pili ikitokezea haja ya kufanya hivyo. Baada ya kipindi cha pili kumalizika na akihitaji kuengezwa muda mtumishi huyo atalazimika kuacha kazi. Isipokuwa kwa mtumishi atakaejiunga na siasa. (3) Kipindi ambacho mtumishi wa umma atakuwa amechukua likizo bila malipo, hakitohesabiwa wakati wa matayarisho yake ya mafao ya uzeeni katika taasisi yake. (4) Mtumishi wa umma yeyote ambae ana mkopo na amechukuliwa dhamana na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi hatoruhusika kuchukuwa likizo bila ya malipo hadi hapo ataporejesha mkopo huo. (5) Mtumishi wa umma anapomaliza likizo bila ya malipo atalazimika kuripoti kazini na Taasisi ikiona inafaa inaweza kumuongezea muda mtumishi anaeomba kwa kipindi cha pili. (6) Mtumishi wa umma hatoruhusika kuchukua likizo bila ya malipo katika taasisi moja ya umma na kwenda kufanya kazi katika taasisi nyengine ya umma. 91 (7) Mtumishi wa umma aliyerudi likizo bila ya malipo atalipwa mshahara wake kwa mujibu wa muongozo utakaotolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma. 64.-(1) Mtumishi wa umma ambae hajaripoti kazini baada ya likizo bila ya malipo kumalizika, Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atalazimika: (a) kumkumbusha mtumishi anayehusika kuripoti kazini; (b) endapo mtumishi wa umma atashindwa kuripoti kazini hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria. (2) Mtumishi wa umma atakayechukua likizo bila ya malipo atalazimika kujaza fomu itakayopaswa kujazwa na mtumishi huyo atakaporejea kazini baada ya kumaliza likizo bila ya malipo pamoja na kujazwa na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi husika; muongozo wa fomu hiyo utatolewa na Afisi Kuu ya Utumishi wa Umma. (3) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi, mtumishi wa umma aliyejiunga na siasa akachukua likizo bila ya malipo atawajibika yeye mwenyewe kurudi kazini baada ya kumaliza shughuli za siasa bila ya kusubiri kukumbushwa kufanya hivyo na Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi wake. 65. Makubaliano ya pamoja yatakayofikiwa baina ya pande zote za vyama vya wafanyakazi na waajiri, yatalazimika kutekelezwa na kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment