Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

LIKIZO YA UZAZI:WATUMISHI WA KIKE

61.-(1) Mtumishi wa umma anapojifungua atastahiki likizo ya uzazi ya miezi mitatu kwa siku za kalenda. Likizo ya Uzazi. 87 (2) Likizo ya uzazi ya miezi mitatu itatolewa mara moja kila baada ya miaka miwili na miezi tisa kwa watumishi wanawake waliojifungua ambao wamo katika masharti ya kudumu. Likizo hiyo haitaathiri likizo ya kawaida ya mwaka ya mtumishi. (3) Pindipo mtumishi wa kike atajifungua kabla ya kutimiza muda uliotajwa chini ya kanuni ndogo (2) ya Kanuni hii, atastahiki kupata mapumziko ya wiki sita za kalenda. (4) Taarifa ya uzazi itatolewa na Mtumishi aliyejifungua au mtu wake wa karibu kwa Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kwa ajili ya kustahiki likizo ya uzazi ya mtumishi huyo, taarifa hiyo lazima iambatanishwe na kitambulisho cha kuzaliwa kwa mtoto kitakachotolewa hospitali, Sheha au Kiongozi wa Mtaa au Kijiji. (5) Itakapotokea mtumishi amejifungua mapacha kipindi cha likizo kitaongezwa mpaka siku mia moja. (6) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi, itakapotokea kuharibika kwa mimba au kufa kwa mtoto, mtumishi huyo atapewa likizo ya wiki sita kutoka tarehe ya kujifungua au kuharibika kwa mimba. (7) Mtumishi ambaye likizo yake imekatishwa kwa sababu ya kifo cha mtoto mchanga, akipata ujauzito kabla ya kutimiza miaka miwili na miezi tisa kuanzia tarehe ya kujifungua au kuharibika kwa mimba, mtumishi huyo atastahiki likizo kama ilivyoelezwa katika kanuni ndogo (1) ya kanuni hii. (8) Hakuna mtumishi atakayefukuzwa, kuhamishwa au kuachishwa kazi kwasababu za ujauzito au kujifungua. 88 (9) Mtumishi atakayejifungua atapewa saa moja ya kunyonyesha kwa kila siku kwa kipindi cha miaka miwili. Mtumishi huyo atachagua aidha kuitumia nafasi hiyo asubuhi kabla ya kuja kazini au mchana saa moja kabla ya muda wa kuondoka kazini. (10) Mtumishi wa kike mjamzito na aliyejifungua atahudhuria kliniki kwa mujibu wa maelekezo ya Daktari wa Serikali na mahudhurio hayo hayatoathiri malipo yake ya mshahara na stahiki nyengine. (11) Mtumishi wa umma atakaejifungua katika muda wa majaribio hatostahiki likizo iliyoelezwa katika kanuni ndogo (1) ya kanuni hii, isipokuwa atastahiki kupata mapumziko ya wiki sita za kalenda.

No comments:

Post a Comment