Search This Blog

Thursday, 12 January 2017

MTUMISHI:LIKIZO YA MARADHI.

60.-(1) Taasisi italazimika kutafuta taarifa za mtumishi aliyekuwa hajahudhuria kazini siku tano mfululizo na ikigundua kuwa mtumishi huyo ni mgonjwa taasisi ifanye utaratibu wa kumpatia matibabu. (2) Mtumishi wa umma atakapopata maradhi atastahiki likizo ya maradhi baada ya kupata idhini ya Daktari wa Serikali kwa muda usiozidi siku 60 za kazi kwa mwaka mmoja kwa malipo ya mshahara kamili bila ya kuathiri likizo ya kawaida ya mtumishi huyo. (3) Iwapo baada ya siku 60 kumalizika itaonekana bado mtumishi anahitaji muda zaidi wa kupumzika kutokana na hali mbaya ya afya yake, Daktari wa Serikali anaweza kuidhinisha kwamba mtumishi anayehusika apewe mapumziko mengine ya muda usiozidi siku 60 kwa malipo ya mshahara kamili ambapo zitakatwa katika likizo yake ya kawaida. (4) Ikiwa baada ya kutolewa siku 120 za mapumziko kutokana na maradhi kwa mujibu wa kanuni ndogo (2) ya kanuni hii, mtumishi atakuwa bado hajapata nafuu ya kumuwezesha kuendelea na kazi, atastahiki kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na Bodi ya Uchunguzi wa Afya za Watumishi, kufuatana na mapendekezo ya Bodi hiyo, mtumishi atapewa likizo ndefu ya maradhi ambayo haitopindukia siku 180 kwa malipo ya mshahara kamili. Likizo hii itolewe pale itakapoonekana kuwa upo uwezekano wa mtumishi anayehusika kupata nafuu katika muda huo, na kwamba nusu ya likizo ndefu ya siku 180 za mwanzo italipwa kutokana na likizo yake ya kawaida. (5) Mtumishi aliye katika likizo ndefu ya maradhi atapaswa kuangaliwa afya yake na Daktari wa Serikali angalau mara moja kwa mwezi na pale atakapoonekana Likizo ya Maradhi. 86 amepata nafuu kiasi cha kuweza kuendelea na kazi atapaswa kuendelea na kazi tarehe ambayo Daktari ataidhinisha hata kama muda wake wa likizo ya maradhi haujamalizika. (6) Mtumishi hatostahiki kuchuma likizo katika kipindi cha likizo ndefu ya ugonjwa. (7) Ikiwa hata baada ya likizo ndefu ya ugonjwa ya siku 300 kwa malipo ya mshahara kamili mtumishi atakuwa hajapata nafuu kiasi ya kuendelea na kazi anaweza iwapo Daktari wa Serikali ataona kuwa kuna uwezekano wa mtumishi anaehusika kupata nafuu kiasi cha kumuezesha kuendelea na kazi, kuomba likizo bila ya malipo kwa muda usiopungua miezi sita. (8) Ikiwa hata baada ya kumalizika muda uliotajwa hapo juu wa likizo ya maradhi, mtumishi anayehusika atakuwa bado anaendelea kuumwa kiasi ya kutozimudu kazi zake, mtumishi huyo hatostahiki muda wowote zaidi wa likizo ya maradhi. Inapotokezea hali hiyo Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi atapaswa kuchukua hatua za kuitaka Bodi ya Uchunguzi wa Afya za Watumishi iidhinishe mtumishi huyo kustaafishwa kwa sababu ya maradhi. (9) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni hizi, Mtumishi aliyekuwemo katika kipindi cha majaribio anastahiki kupata likizo ya maradhi. (10) Ni jukumu la Katibu Mkuu au Mkuu wa Taasisi kufuatilia taarifa za ugonjwa za mtumishi aliyekuwepo katika likizo ya maradhi.

No comments:

Post a Comment