Ukurasa huu unakupa dondoo mbalimbali za namna ya kuitunza afya yako na hatimaye kuishi maisha ambayo siyo hatarishi kwa afya yako. Kutunza afya ni moja kati ya majukumu muhimu sana kwa kila binadamu. Afya njema hutusaidia kuishi maisha marefu kwa raha bila kusumbuliwa na maradhi ya hapa na pale. Healthline wanaonyesha kuna faida lukuki pale unapoamua kuitunza afya yako nazo ni:
Husaidia kuwa na uzito mzuri
Husaidia kupambana na maradhi
Hurefusha maisha
Hufanya ujisikie vizuri
Ukurasa huu utakuwa unakupa dondoo mbalimbali za kukusaidia kujua namna ya kutunza afya yako vilevile kufahamu namna ya kujiepusha na magonjwa mbalimbali. Jim Rohn aliwahi kusema; “Tunza mwili mwako, kwani ndiyo sehemu pekee uliyonayo ya kuishi”
No comments:
Post a Comment