Search This Blog

Wednesday, 11 January 2017

Njia ya Uzazi wa Mpango kwa Kutumia Kalenda

Njia ya Uzazi wa Mpango kwa Kutumia Kalenda
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKy4r8GZ7rlv_yMVvEqYcSuKhMJ-zp3xOBPqaXuq2MiWcQHAXh28ImtkT1TXfwIxk8JF4_NFlzAs7xer70Ka41DqDCU9OJaTqjP6WpFAdLOXAZGNw-SKVUTz7oyEeg0eCGZm-cG483yAQB/s1600/



Hii ni njia ambayo mwanamke anaweza kutumia kupanga uzazi bila kutumia dawa au kitu cha aina yoyote.  Njia hii inategemea kuchagua kwa makini siku za kufanya mapenzi kutegemeana na ufahamu wa kipindi chote cha hedhi cha mwanamke.  Njia hii ina faida yake, lakini yeyote anayeitumia lazima awe makini sana, kwa sababu lazima ajue lini anategemea kupata damu ya hedhi tena.  Ni rahisi sana kufanya makosa kwa kutumia njia hii.
Nani anaweza kutumia njia ya kalenda
Wanawake walioko tayari kuchukua miezi 3 hadi 6 kupima vipindi vyao vya hedhi kabla ya kutumia njia hiyo.
Wanawake walio na mzunguko wa hedhi ambayo urefu wake haubadiliki. Wanawake wanaojua hisabati vizuri .

MAKALA: NJIA ZA UZAZI WA MPANGO.

Kwa hiyo, kabla ya kutumia njia hiyo, ni vyema kwa mwanamke kuandaa kalenda inayoonesha siku yake ya kwanza kutoa damu ya hedhi kila mwezi kwa kipindi cha miezi 3 hadi 6.  Hii itamsaidia kujua lini mayai yake yalipevuka.

Njia hii inamsaidia zaidi mwanamke aliye na mzunguko wa hedhi wa siku 28, na hutegemea kufahamu kuwa yai la mwanamke hupevuka siku 14 kabla hajaingina kwenye hedhi.

Kwa mfano;  1)  Kama unaanza kuingia katika hedhi tarehe 1 Juni (na una mzunguko wa hedhi wa siku 28), basi kuna uwezekano mkubwa utaingia kwenye kipindi kipya cha hedhi tarehe 29 Juni.  Kwa hiyo yai lako litapevuka siku 14 kabla kwenye tarehe 15 Juni.  Kwa hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kwako wewe kupata mimba kama unafanya mapenzi karibu na tarehe hii, kuanzia tarehe 14 Juni hadi 16 Juni.  Kwa hiyo kuepukana na kupata mimba, usifanye mapenzi kati ya tarehe hizo.  Lakini lazima ukumbuke kuwa mbegu za kiume zinaweza kuishi ndani ya mwili wa mwanamke kwa siku 7, kwa hiyo ili kuwa na uhakika zaidiya kuepukana na kupata mimba, unatakiwa kutokufanya mapenzi kuanzia tarehe 8 hadi 16 Juni.

No comments:

Post a Comment