
Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI ) ni maradhi ambayo huathiri mfumo wa mkojo yaani figo, mirija ya mkojo pamoja na kibofu cha mkojo.
Maradhi haya husababisha na vimelea wa aina mbalimbali . Bacteria ndio husababisha UTI mara nyingi zaidi kuliko vimelea wengine. Hata hivyo fangasi pia huweza kusababisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.
"Kibofu cha mkojo ndicho kiungo ambacho huathirika zaidi. Bacteria wanaweza kusambaa kutoka kwenye kibofu cha mkojo na kuathiri sehemu zingine kwenye mfumo wa mkojo"
Vimelea hawa huweza kuingia kwenye njia ya mkojo kwa njia mbalimbali. Mojawapo ni kutoka kwenye njia ya haja kubwa kwenda kwenye njia ya mkojo hasa wakati wa kutawaza. Hivyo ni vyema kutawaza toka mbele kurudi nyuma ili kuepuka kuingiza vimelea kwenye mrija wa mkojo. Wanawake wako katikahatari kubwa ya kupata maambukizi kwa sababu mirija yao ni mifupi ukilinganisha na wanaume.
Pia vimelea hawa huweza kuenezwa wakati wa tendo la ndoa,na pia kutawaza kwa wanawake
Dalili za UTI
Iwapo unapata dalili hizi ni dhahiri kuwa unaweza kuwa na UTI.
•Kuhisi maumivu kama kuungua wakati wa kukojoa
•Kuhisi haja ya kutaka kukojoa mara kwa mara na unapokwenda unapata mkojo kiduchu.
•Kuhisi maumivu chini ya tumbo na hata mgongoni
•kupata mkojo wenye rangi au damu
•Uchovu
•Kuhisi homa au baridi
Vipimo
Vipimo hutolewa katika mkojo. Mkojo unaweza kufanyiwa uchunguzi wa moja kwa moja au kuoteshwa kwa siku kadhaa.
Matibabu
Maambukizi ya kibofu cha mkojo hayana madhara makubwa kama yakitibiwa haraka. Mgonjwa huweza kuandikiwa dawa za kunywa au sindano kutegemea hali ya mgonjwa.
Maambukizi ya figo huweza kusababisha mgonjwa kupata maradhi sugu ya figo na hivyo figo kushindwa kufanya kazi vizuri.
Pia bacteria huweza kuenea katika sehemu mbalimbali za mwili hivyo kusababisha madhara zaidi na hata kifo.
Unashauriwa kufanya yafuatayo ili kupunguza kupata maambukizi mara kwa mara
•Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau lita 3
•Hakikisha unakojoa unapohisi haja. Epuka kubana mkojo.
•Kojoa kila baada ya tendo la ndoa
•Nawa kabla ya kukutana kimwili
•Tawaza toka mbele kurudi nyuma kila baada ya haja kubwa
•Kula matunda na vyakula vya protein
No comments:
Post a Comment