DAWA NA TIBA
Faida za Kiafya za Kitunguu Swaumu (Garlic)
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen'genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika China mwaka 510 K.K na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Roma. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana.
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash) ingawa watumaiji wake wengi huilalamikia dawa hiyo kwa sababu ya harufu mbaya ya dawa hiyo inayowasababishia kunuka kwa mdomo.
Faida za vitunguu swaumu
Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na Ushahidi wa Kitafiti
Katika utafiti uliofanyika nchini Czech ilionekana kuwa matumizi ya vitunguu swaumu yalisaidia sana katika kupunguza kusanyiko la lijamu (cholesterol) pamoja na mafuta yasiyofaa mwilini (low density lipoproteins) katika mishipa ya damu. Aidha, mwaka 2007 BBC iliripoti matumizi ya vitunguu swaumu katika kusaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya aina fulani ya mafua iliyosababishwa na virusi. Mwaka 2010, ulifanyika utafiti mwingine ambao ulijumuisha wagonjwa 50 wenye shinikizo la damu sugu ambalo lilikuwa ni vigumu kudhibitiwa hata kwa matibabu yaliyozoeleka ya dawa na njia nyingine. Kama njia ya kuchunguza ufanisi wa vitunguu swaumu katika kutibu shinikizo la damu, baadhi ya wagonjwa hao walipewa vitunguu swaumu wakati wengine walipewa dawa isiyohusika na matibabu ya shinikizo la damu (au placebo). Ilionekana kuwa wale waliopewa vitunguu swaumu kama dawa ya shinikizo la damu walionesha maendeleo mazuri kwa vitunguu swaumu kuweza kushusha vizuri kiwango cha shinikizo la damu, hususani systolic pressure, tofauti na wale waliopewa placebo.
Nini siri ya kitunguu swaumu?
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo; Nini Madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;

No comments:
Post a Comment