Mbeya. Diwani wa Kata ya Mwakibete jijini hapa, Lucas Mwampiki (Chadema), ametangaza vita dhidi ya wazazi ama walezi watakaowapeleka watoto shuleni bila ya kuwanunulia mahitaji muhimu akisema watachukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu kwenye msiba wa Charles Mwangoka ambaye alikuwa mkazi wa Mtaa wa Ng’osi katika kata hiyo, Mwampiki aliwataka wazazi kuhakikisha wanakamilisha mahitaji ya wanafunzi kabla ya shule kufunguliwa Jumatatu ijayo.
“Ndugu wakazi wote wa Kata ya Mwakibete, napenda kuwakumbusha kwamba kamati ya maendeleo ya kata tulishakubaliana kwamba kuanzia sasa wanafunzi wote wakamilishiwe mahitaji kama sare, viatu, madaftari na pia lazima wawe wasafi kimwili wakati watakapoanza masomo,’’ amesema.
Mwampiki amesema hoja ya elimu bure haina maana ya wazazi wawapeleke watoto bila kuwanunulia sare, vifaa ama kutowapatia fedha za chakula.
No comments:
Post a Comment