Search This Blog

Wednesday, 11 January 2017

Mbunge wa Kilombero Morogoro (CHADEMA ) ahukumiwa miezi 6 jela Bila Faini





Na, Jackson Monela – Star TV
Mahakama ya Wilaya ya Kilombero imemuhukumu kifungo cha miezi Sita mbunge wa Jimbo Kilombero mkoani Morogoro Peter Lijualikali (30) mara baada ya kumkuta na hatia ya kufanya fujo na kusababisha taharuki katika uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Machi Mosi mwaka 2016.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Timothy Lyon na imemuhusisha mbunge wa Jimbo hilo Peter Lijualikali pamoja na mwenzake Stephano Mgata (35) ambaye  yeye amehukumiwa kifungo cha nje cha Miezi sita.
Lijualikali amekutwa na hatia kutokana na kuonekana kutiwa hatiani zaidi ya mara tatu kupitia kesi namba 338 ya mwaka 2014, kesi namba 220 ya mwaka 2014 na kesi namba 340 ya mwaka 2014, hivyo kutokana na kuonekana ni mzoefu mahakama imeona mtuhumiwa ana hatia ya kutumikia kifungo hicho cha miezi sita.

No comments:

Post a Comment