Donald Trump na atakayekuwa makamu wake Mike Pence
wameidhinishwa na baraza hilo kwa ushindi wa kura zaidi ya 270 ikiwa ni
wiki sita baada ya kupita uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo
November 8, 2016 japokuwa kwenye upande wa kura za wananchi wa kawaida
bado Hillary Clinton ameendelea kuongoza baada ya kuongeza kura zaidi ya
milioni 3 baada ya matokeo kutangazwa.
Kupitia
kurasa zao za Twitter, Donald Trump na makamu wake Mike Pence wameonesha
furaha yao baada ya kuthibitishwa kwa ushindi wao.

No comments:
Post a Comment