Mahakama kuu nchini Ethiopia imewatia hatiani waumini wa dini ya kiislamu wapatao ishirini na kuwahukumu kifungo gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kueneza msimamo mkali wa kidini na kupenyeza kundi la Islamic State nchini humo.
Watu hao wamehukumiwa chini ya sheria sheria mpya tata ya kupambana na ugaidi.kwa pamoja isipokuwa mmoja wao wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano unusu gerezani naye wakili wao amesema kwamba watakata rufaa dhidi ya kifungo kwa wateja wake.
Miongoni mwa watuhumiwa hao ni waandishi habari wawili ambao walikuwa waajiriwa wa kituo kimoja cha redio ya kiislamu.
Upande wa mashitaka ulisema watuhumiwa walijaribu kuchochea vurugu na kusambaza vipeperushi katika misikiti katika mji mkuu, Addis Ababa, na miji mingine.
Waandishi wa habari wamekuwa na mitizamo tofauti tofauti na kutoa maoni kwamba Waislamu kwa muda mrefu wanajiona wanyonge nchini Ethiopia.
No comments:
Post a Comment