Search This Blog

Tuesday, 31 January 2017

MGODI RZ WAFUNGWA

Mgodi wa RZ wafungwa, Kamishna aongoza uchunguzi

SERIKALI imeufunga Mgodi wa RZ Union uliopo mkoani Geita kwa siku tano ili kupisha ukaguzi maalumu wa timu ya watalaamu, nayoongozwa na Kamishna wa Madini, Alli Samaje.

Agizo hilo, limetolea na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani, juzi wakati akizungumza na wananchi, baada ya wachimbaji 15 kuokolewa kutoka shimoni wakiwa hai.

Alisema baada ya kutokea ajali hiyo, mlango wa mgodi huo ulifukuliwa na kuharibu sura yake ya awali, hivyo lazima mgodi huo ufanyiwe ukaguzi kabla ya kuruhusiwa kuendelea.

“Siku tano (kuanzia jana), Kamishna wa Madini na watalaamu wengine wahamie hapa kwa ajili ya ukaguzi wa kina kuhusu usalama kabla ya kuendelea na shughuli zao ili kujiridhisha kama utakuwa salama,” alisema.

Naibu waziri huyo aliagiza ukaguzi wa awali ufanyike, iwapo aliyeukagua alishauri vyema na ikibainika kama hakutimiza wajibu wake, hatua zichukuliwe dhidi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, msemaji wa mgodi huo, Francis Kiganga alisema wamesitisha uzalishaji wao kupisha ukaguzi na wako tayari kupokea maelekezo ya Serikali.

“Kamishna wa Madini, ataanza ukaguzi nadhani akikamilisha ukaguzi wake tutapewa maelekezo hivyo tunangoja katika kipindi hicho cha ukaguzi kupokea maelekezo hayo na kutekeleza,” alisema.

Ukaguzi waanza

Katika kutekeleza agizo hilo, Kamishna Samaje jana aliwasili mgodini hapo saa 7 mchana kwa ajili ya kuanza ukaguzi wake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Mkazi wa Madini wa Mkoa wa Geita, Ally Said alisema tayari Samaje alikuwa katika eneo la tukio.

“Nitazungumza naye baadae, sasa yupo kwenye ukaguzi na akikubali nitawafahamisha waandishi mkutane naye maana yeye ndiye anaweza kueleza suala la ukaguzi huu,” alisema.

Wachimbaji watoka Hospitali

Wakati huo huo, wachimbaji hao waliofukiwa na kifusi na kukaa siku nne wamerejea kazini kwao tayari kwa ajili ya kuanza kazi wakingoja ukaguzi wa Serikali kukamilika.

Hii ni baada ya madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Geita kuthibitisha kuwa wachimbaji hao wapo salama.

Akizungumza hospitalini baada ya kuruhusiwa, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga alisema afya za wachimbaji hao zimeimarika na wako salama na kuwataka warejee kwenye majukumu yao ya kila siku.

“Kilichowatokea ni ajali kazini, madaktari wanasema mpo salama sasa mnaruhusiwa leo kutoka hapa hospitalini na mtakwenda kuendelea na majukumu yenu hivyo niwatakie utendaji kazi mwema,” alisema.

Akizungumzia afya ya wachimbaji hao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita, Brian Mawala alisema watu hao wako katika hali nzuri, baada ya kukaguliwa kitabibu kwa siku ya juzi na jana na wameridhika kuwa hawana shida nyingine yoyote, hivyo wanaweza kuendelea na kazi.

DC ataka wapewe mikataba

Kutokana na hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi aliuagiza mgodi huo kuwapatia mikataba ya ajira wachimbaji hao waliofukiwa ili kuwapa uhakika wa ajira zao kutokana na kubaini kuwa wawakifanya kazi kwa mkataba wa miezi mitatu.

“Nimezungumza na wajiri wenu juu ya ajira yenu, tumekubaliana awapatie mkataba na wamekubali wote mtapata mkataba wa muda mrefu, hivyo zaidi ya hapo kuna fedha ambazo zilitolewa na wadau kwa ajili yenu sasa tutazungumza niwafahamishe ni kiasi gani na kesho nitawaletea wote kila mmoja asaini kupokea na kisha nitatangaza.

Mgodi

Katika hatua nyingine Msemaji wa Mgodi wa RZ Union, Francis Kiganga alisema mgodi huo ambao umeanzishwa Julai, 2013, ulikuwa ukichimbwa mawe kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya kuanza uzalishaji hapo Juni mwaka huu.

Alisema walikuwa katika hatua za ukamilishaji wa ujengaji wa kinu cha kusagia mawe, ikiwa ni pamoja na mtambo wa kuzalisha dhahabu (CP) ambao ulikuwa ukiendelea kujengwa.

Tathmini Matokeo IV 2016

Tathmini ya Jumla kuhusu matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016

Dkt. Charlse Msonde, Katibu Mtendaji NECTA

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.

Dkt. Charlse Msonde, Katibu Mtendaji NECTA

Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa watahiniwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya mtihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Aidha amesema baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa 126 waliobainika kufanya udanganyifu ikiwa ni pamoja na watahiniwa 58 wa shule, 58 wa kujitegemea na watahiniwa 10 wa QT. Pia baraza hilo limefuta matokeo ya mtahiniwa mmoja aliyebainika kuandika matusi kwenye karatasi yake ya majibu.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililoongoza kwa ufaulu ni Kiswahili ambapo asilimia 77.75 wamefaulu na somo la mwisho ni Basic Maths ambalo asilimia 18.12 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.

Kati ya wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 5 ni wasichana na 5 ni wavulana wakiongozwa na Alfred Shauri kutoka Feza Boys ya Dar es Salaam

Kati ya shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa, shule 6 zinatoka katika mkoa wa Dar es Salaam




WANAUME WALALAMIKIWA UTUNZAJI WATOTO

Wanaume washitakiwa matunzo ya watoto

MALALAMIKO yanayohusu huduma za utunzaji wa watoto yameongezeka zaidi kwa mwaka 2016 kutokana na sababu mbalimbali, mojawapo ikitajwa kuwa ni hali ya uchumi kubadilika nchini.

Kwa mwaka 2015, Mahakama ya Watoto Kisutu jijini Dar es Salaam, ilipokea malalamiko 17 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambao walipokea malalamiko yapatayo 154, hali ambayo si kawaida na miaka mingine.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Watoto Kisutu, Devotha Kisoka katika wiki ya utoaji wa elimu na msaada wa sheria inayofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja.

“Katika awamu hii ya tano ya serikali ya kubana matumizi malalamiko yamekuwa mengi sana kwani wanaume wengi ambao wana watoto wengi imewawia vigumu kuwatunza,” alisema Kisoka na kuongeza kuwa mashauri yanayohusu matunzo kwa watoto ni mengi, tangu ilipofutwa mianya ya ufisadi, wanawake wengi wameachwa na wamekuwa wakifika kwa kutokujua waende wapi na watoto.

Alisema kutokana na hali hiyo, wanaume wengi wameamua kuelekeza fedha zao kutunza watoto wao wa ndani ya ndoa pekee na kuwapa kidogo wale walionao nje ya ndoa, jambo ambalo halikuwa hivyo kwa miaka ya nyuma.

Aidha, aliwahimiza wanaume kukumbuka wajibu wa kuwatunza watoto wao bila kujali hali yao ya kiuchumi wakitambua kuwa mtoto ana haki ya kulelewa na kupata matunzo.

Alisema sheria imewapa haki wazazi, walezi au yoyote mwenye maslahi ya mtoto kupeleka kesi katika Mahakama za Watoto kama kudai matunzo, mamlaka ya kisheria juu ya uangalizi wa mtoto na uasili wa kambo kwa kuwa mtoto ana haki ya kulelewa au kuwajua wazazi ama walezi.

Alisema kwa mwaka huu mashauri ya aina hiyo yameendelea kufika kwa wingi na kwa kuwa bado ni mapema, bado wataendelea kuyapokea.

Alisema asilimia kubwa ya wanaofika kufungua mashauri hayo ni wanawake wakidai kuachwa bila huduma kwa watoto, lakini pia hata wanaume hufika kwa madai ya kutaka kuruhusiwa kuwaona watoto ama kuwatembelea.

Kuhusu utendaji wa Mahakama hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Watoto, Kisutu, Victoria Nongwa alisema hupokea mashauri mbalimbali yanayohusu watoto kwa kuwa nao hufanya makosa mbalimbali kama ilivyo kwa watu wazima.

Alisema mtoto ana haki ya kupata dhamana katika mashitaka yote isipokuwa yale ambayo sheria imetamka bayana hayana dhamana na wanaweza kupata adhabu kama amri ya kuachiwa kwa masharti kwa kipindi fulani lakini kisizidi miaka mitatu.

Alizitaja adhabu nyingine ni kulipa faini, adhabu ya kuripoti kwa ofisa ustawi wa jamii kwa kipindi fulani na adhabu ya kupelewa katika shule maalumu.

Monday, 30 January 2017

Waziri mkuu apokea ugomvi wa DC na MBUNGE.

Waziri Mkuu apokea ugomvi wa DC ,Mkuu wa wilaya

Dodoma. Mgogoro baina ya Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia na mkuu wa wilaya hiyo, Saimon Odunga umechukua sura mpya, safari hii ukiibuka katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dodoma (RCC) ambayo imeamua ufikishwe kwa Waziri Mkuu.

Kikao hicho ambacho kilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kilifanyika  katika ukumbi wa Chuo cha Mipango.

Baada ya Odunga kupewa nafasi ya kuchangia ajenda mara baada ya Majaliwa kuondoka, aliomba ushirikiano kutoka kwa wabunge ilikutekeleza shughuli za maendeleo.

“Ninaomba waheshimiwa wabunge watusaidie kulisemea hili kwa sababu hali ni mbaya katika sekta nyingi,” alisema.

Akizungumza katika kikao hicho, Nkamia, ambaye aliwahi  kuwa naibu waziri, alianza kwa kumuomba Rugimbana kusaidia katika sekta ya ardhi akisema ina matatizo mengi na kutoa mfano wa Wilaya ya Chemba.

Alisema katika wilaya hiyo kuna tapeli wa ardhi ambaye amesaidiwa na viongozi kupata ardhi yenye ukubwa wa ekari 500 kinyume na sheria.

Alihoji sababu za mkuu huyo wa wilaya kutaka wabunge washiriki katika kusukuma hoja mbalimbali za maendeleo, wakati anadharau wabunge, mwenyekiti wa halmashauri na viongozi wengine wa chama wilayani humo.

“Huyu ni mkuu wa wilaya ambaye anaongoza kwa rekodi ya kuwakamata watu kwa kutumia madaraka yake. Nimesikia jana (juzi) kuwa na mimi nawindwa ili nikamatwe. Niko tayari kukamatwa,” alisema Nkamia, ambaye anaongoza Jimbo la Chemba kwa kipindi cha pili mfululizo.

“Nakuomba mkuu wa mkoa umuite huyu dogo (DC) umkanye kuhusu hii tabia yake ya kudhalilisha watu. Kwa kuwa bwana mkubwa (DC) hapo ameanzisha vita na sisi tunaomsaidia kazi. Sisi tuna busara zetu, hatuwezi kuingia vitani,” alisema.

Nkamia alimuomba Rugimbana kuwaita wote wawili-Odunga na yeye-wakae pamoja na kutafutia suluhu ya jambo hilo ambalo alisema linaweza kukwamisha maendeleo ya jimbo hilo.

Alimuonya mkuu huyo wa wilaya kuhusu tabia ya kuwatia mbaroni wananchi wanaouliza maswali wakati ni haki yao kufanya hivyo.

“Chemba tulikuwa tunaishi kwa amani sana lakini amekuja bwana huyu mdogo (Odunga) anataka kutuchafulia sifa sisi. Ameteuliwa na Rais amefanyiwa vetting (uhakiki) nzuri tu. Mambo ya kuwaita watu wapumbavu no (hapana),” alisema Nkamia.

KIKOMO USAJILI TIN

Usajili wa TIN wafikia kikomo.
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haitaongeza siku za kufanya uhakiki wa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) hapa jijini baada ya muda kumalizika leo, hivyo wote watakaokuwa hawajahakikiwa watafutiwa namba zao na watatakiwa kuomba upya.
Kwa mara ya kwanza TRA imepanga kufanya uhakiki wa TIN kwa siku 60 kati ya Agosti na Oktoba lakini baada ya kujitokeza watu wengi tarehe ya mwisho iliongezwa hadi Novemba na mara ya tatu ilisogezwa hadi Januari 31. Lengo la uhakiki huo ni kuondokana na mfumo wa kizamani wa usajili wa namba hiyo.
Kayombo alisema kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa wanahitaji kuhakikiwa namba, mamlaka iliamua kusogeza mbele muda wa kutoa huduma hiyo pamoja na kufungua vituo vya kutoa huduma ambako watumishi walifanya kazi hiyo hadi Jumamosi na Jumapili kuwapa nafasi wafanyakazi.
Alisema madhara kwa watakaofutiwa TIN ni makubwa kwani wafanyabiashara na madereva wa magari leseni zao zitakuwa batili na watachukuliwa hatua kwa kosa la kufanya biashara bila kuwa na namba ya utambulisho.
“Wale wote ambao watakuwa hawajahakikiwa watafutiwa namba zao za TIN, itawalazimu kuomba upya ingawa kuomba kwao upya hakutafuta madeni yao ya nyuma,” alisisitiza Kayombo.
Mmoja wa watu waliokwenda kuhakiki namba zao kituo cha Mwenge, Abdul Namwelesi alikosoa utaratibu huo akipendekeza uhakiki ungekuwa endelevu badala ya kuweka muda maalumu kutokana na ugumu wa watu wote kuhakikiwa kwa wakati mmoja.
Alisema kutokana na ratiba ya maisha hususani kwa wakazi wa Dar kuwa za kukimbizana, TRA wangeweka utaratibu maalumu kila dereva anapokwenda kuhuisha leseni yake ahakikiwe taarifa zake  na kila mfanyabiashara anapokwenda kulipa kodi hapohapo ahakikiwe taarifa zake.
Zulekha Kambi aliyekutwa kwenye kituo cha Uwanja wa Taifa alijilaumu kutokana na kutotumia muda mrefu uliokuwa umetolewa badala yake akasubiri hadi siku za mwisho zenye msongamano mkubwa.
“Najuta. Wee acha tu. Nilikuwa likizo nyumbani mwezi mzima. Jana ndiyo nimekumbuka kesho mwisho. Nimekuja na nimekuta umati kama huu. Hapa nilipo hata fomu sijui nitaipata saa ngapi,” alisikitika.

Usimkimbie mdeni wako.

Usimkimbie anaye kudai, hii ndio namna ya kudili na madeni
Ngoja nikumegee kidogo, hivi unajua kama Kukimbia madeni ni hatari kuliko kuyakabili? Unapokuwa na deni au madeni siku zote ni mzigo, ambao unatamani siku moja ungepata nafasi ya kuutua. Hivyo basi ni vizuri kuangalia namna ya kuutua huo mzigo.
Mimi na wewe tunakubaliana kwamba huwa tunakopa kwasababu ya kutatua shida zetu sio vinginevyo, na mara zote kama kweli uko sawa ukiwa unakopa nia na madhumi ni kuja kurudisha hicho kiasi siku moja. Hivyo basi endapo umeshindwa kurudisha kwa wakati zipo namna za kukabiliana na mdeni wako nazo ni hizi hapa:
Dumisha mawasiliano na mdeni wako, mueleze wakati na hali uliyo nao. Usimfiche jaribu kueleza kiundani kwanini umeshindwa kulipa kwa wakati na pia muonyeshe masikitiko yako juu ya hilo.
Toa ahadi itakayo kuweka huru, Kwa mfano Unampa mtu ahadi kuwa nitakulipa tarehe kumi na mbili, wakati wewe ni mfanya kazi na unategemea mwisho wa mwezi na huna namna yoyote ya kupata pesa hapo katikati. Wakati mwengine unaweza kutoa ahadi ilikumpa moyo mdeni wako lakini ujue unajiweka kwenye matatizo makubwa Zaidi. Kumbuka kwamba unapo mpa mtu ahadi naye anaweka mipango yake, ukitoa ahadi nyingi zisizotimia kumbuka pia unapunguza uamini kwake.
Hakikisha unajipa muda wa kutosha, na kuwa na uhakika na ahadi unazotoa, hakuna kitu kinacho kera wadai kama ahadi nyingi zisizo na mwisho
Punguza deni kidogo kidogo, wakati mwengine labda ni ngumu kupata pesa yote na kulipa kwa wakati lakini unaweza kuwa unapata kidogo kidogo. Nivizuri kupunguza kwani inajenga uamini Zaidi na pia huonyesha nia ya kweli ya kulipa deni.
Usisuburi hadi mdeni wako kukupigia simu kukuuliza kuhusu “ unalipa lini”. Piga simu kabla yake na eleza maendeleo ya marejesho.
Onana na mdeni wako uso kwa uso kama inawezeka, kuonana na mdeni wako physically inasaidia kuonyesha emotions au hisia. Hata ukimueleza jambo au kwanini umekwama kulipa deni inakuwa rahisi kukamata hisia zake pia. Pia inajenga ukaribu na heshima kwamba umeamua kumtafuta na kuongea nae.
Pia kumbuka kwamba mdeni ni mtu, Wakati mwengine mtu baada tu ya kukopa na simu hapigi tena hata yale mahusiano ya kawaida yanapungua. Hii inaharibu sana, nayeye siku pia akija kukudai atakudai kama hakujui na hatakusiliza shida zako.
Kwakumalizia: Hizi ni namna tu za kudili na madeni mambo yanapokuwa magumu, ila dawa kubwa ya deni ni kulipa au kutokopa.
Nakutakia kila la heri kwenye Pilika za Maisha, kwa nafasi za kazi na scholarships tembelea>> Jobs in Tanzania-Stuffzoom..

Matunzo ya mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa

Matunzo ya mtoto aliyezaliwa nje ya Ndoa
Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni nani?
Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ni yule ambaye amezaliwa na mwanamke ambaye hajafunga ndoa na mwanaume aliyezaa naye.
Aidha kama mwanamke  ambaye ameolewa lakini anakaa mbali na na mume wake, akizaa na mwanaume mwingine mtoto atakayezaliwa atahesabiwa kuwa ni mtoto wanje ya ndoa.
Vilevile mjane akijifungua mtoto ambaye si ya marehemu mume wake atahesabiwa kuwa ni mtoto wan je ya ndoa.
Watoto wanaozaliwa katika mazingira haya matunzo yao yanasimamiwa na sheria ya matunzo ya watoto wa nje ya ndoa Sura 278 ya mwaka 1964.
Kufuatana na sheria tajwa hapo juu, mama wa mtoto huyo anaweza kupeleka maombi mahakamani akiomba mahakama imtangaze mwanaume fulani kuwa baba halali wa mtoto.
Matunzo ya mtoto, baada ya baba wa mtoto kutangazwa au kuthibitishwa na mahakama, na mama wa mtoto kuomba atoe matunzo au gharama za elimu ya mtoto na baba akikataa au kutoa kiasi cha fedha ambazo hazitoshi.
Mahakama baada ya kupokea maombi  inaweza kumwita baba huyo na kutoa amri kuwa atoe gharama za matunzo kwa mama kwa mama wa mtoto au mlezi kulingana na kipato chake.
Maombi haya yatapelekwa katika mahakama ya Wilaya kwa kuwasilisha hati ya maombi ikiambatana na hati ya kiapo.
Endapo amri ya matunzo na gharama za elimu zinatafutwa mahakamani na mama wa mtoto, itakuwa ni kosa kwa mtoto huyo kuondolewa chini ya malezi ya mama yake.
Iwapo mtu yeyote atakiuka amri ya mahakama inayotaka malezi kuwa chini ya ya mama na inayokataza kumchukua mtoto anayelelewa na mama yake mzazi.
Mtu huyo anaweza kushitakiwa na akipatikana na hatia anaweza kufungwa.
Matunzo ya mtoto yanapotolewa inabidi yatumike kwa kumtunza mtoto na wala si vinginevyo, na mtu anayefuja fedha za mtoto anaweza kushitakiwa na akipatikana na hatia anaweza kufungwa jela.
Angalizo, endapo wakati wa kupeleka maombi mahakamani, mwombaji akiolewa au kama mwombaji alikuwa ni mwanamke aliyeolewa lakini akiishi mbali na mumewe, na katika kipindi cha maombi amerudiana na kuishi na mumewe mahakama haitaweza kutoa amri ya matunzo kwa mtoto husika.
Fedha zote kwa ajili ya matunzo ya mtoto zinaweza kulipwa kwa mama au mlezi wa mtoto. Hata hivyo fedha zinaweza kulipwa mahakamani na baadaye mahakama kuzituma kwa mama au mlezi wa mtoto.
Uteuzi wa mlezi, baada ya mama wa mtoto kutakiwa kulipwa  matunzo na ikaonekana kuwa mama wa mtoto hawezi kumlea mtoto, mahakama inaweza kumteua mtu mwingine kwa ajili ya kumlea mtoto kama mtu huyo amekubaliana na uteuzi huo kwa hiari yake mwenyewe.
Baadhi ya vigezo vinavyosababisha mlezi kuteuliwa ni mama kufariki, kutokuwa na akili timamu au kufungwa gerezani.
Maombi ya kuteuliwa mlezi yanaweza kuwasilishwa mahakamani na baba wa mtoto, mama wa mtoto au Afisa Ustawi wa Jamii.
Hata hivyo baba wa mtoto anaweza kupeleka maombi kuomba mtoto husika awe chini ya uangalizi pale mtoto anapotimiza umri wa miaka saba.

Dalili za vidonda vya tumbo

Dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo

Dalili zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na;

Kuchoka choka sana bila sababu maalum
Kuuma mgongo au kiuno
Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
Kizunguzungu
Kukosa usingizi
Usingizi wa mara kwa mara
Maumivu makali sehemu ya mwili
Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
Kichefuchefu
Kiungulia
Tumbo kujaa gesi
Tumbo kuwaka moto
Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
Kutapika nyongo
Kutapika damu au kuharisha
Sehemu za mwili kupata ganzi
Kukosa hamu ya kula
Kula kupita kiasi
Kusahahu sahau na
Hasira bila sababu.

Kwa kweli ni vigumu kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.

Ufugaji kuku wakienyeji kama mradi

Ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi.

MAHITAJI

Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01
Banda bora
Vyombo vya chakula na maji
Chakula bora
Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
Chanzo cha nishati joto na mwanga
Elimu na ujuzi wa malezi bora
Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)
Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu
KUKU 10

Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.

Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja pia.

JOGOO 01
Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi. Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.

BANDA BORA
Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04. Yani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana. Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika. Mfano katika maeneo ambayo fitoKuku zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo. Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi. Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-

Sakafu: Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
Kuta: Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu
Paa: Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
Wigo: Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na mabati
Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.
Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala.
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa. Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.

JINSI YA KUFANYA
Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga. Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.

Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuetamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.

Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti. Kuku anapotaga mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumwandaa kwa kazi ya kuetamia. Kwa kufanya hivi, kuku atataga mayai 15 au zaidi na ikiwa atataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri utafute mayai mengine ujazilizie ili kufikisha mayai 20 kwa kila kuku. Zingatia kwamba mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yanatunzwa sehemu salama, mahali pakavu, pasafi na penye joto la wastani.

Kuku wote wanapaswa kuanza kuetamia kwa siku moja. Ili kufanikisha hili inapasa uwe karibu na kuku wako. Kuku mmoja akianza kuetamia mwekee mayai ya kuku wa kisasa au mayai mabovu ya kuku wa kienyeji. Utafanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuetamia mayai. Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku yaliyotumika humfanya kuku aendelee kuetamia akijua ni mayai yake.

Baada ya kuona kwamba kuku wako wote wapo tayari kwa kuetamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuetamia yani chumba kimoja katika lile banda letu. Ninashauri kwamba chumba kwajili ya kuetamia kiwe chumba cha kwanza au cha mwisho katika mfuatano wa vyumba vya banda lako. Andaa viota bora vya kuetamia, weka mayai 20 kwa kila kiota, ikiwa hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi yako.

Waamishe kuku kutoka wanapotagia na kuwaweka katika chumba ulichokiandaa kwajili ya kuetamia. Ili ufanikiwe katika zoezi hili inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza. Mweke kuku katika kila kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake. Wahudumie kwa chakula na maji ya kutosha. Wakati wa usiku waongezee joto la ziada kwa kuweka jiko au ndoo ya chuma yenye chengachenga za mkaa au kama una umeme weka taa za joto.

Baada ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua vifaranga. Huu ndio wakati unaotakiwa kuwa karibu sana na kuku wako kuliko wakati wote. Watenge vifaranga mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba chao maalumu mbali na kuku. Kama chumba cha kuetamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawe chumba cha mwisho n.k

Ukishawatenga vifaranga mbali na matetea wako, wawekee tena mayai mengine 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua kwa wafigaji wenzako. Hakikisha kuku waliotaga hayo mayai ni wazuri, hawana magonjwa na wanauzito/ukubwa unaofaa. Mayai yote yakaguliwe vizuri ili kujua kwamba yameharibika, yana nyufa au mabovu. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba chako ni kisafi na viota vimesafishwa, havina wadudu na uchafu wowote. Kuku wako bila kujijua wataanza kuetamia upya mayai uliowawekea.

Ukiwawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyokwambia awali. Baada ya siku 21 hadi 25 tena utapata vifaranga wako wengine tena. Fuata kila hatua kama nilivyokwambia hapo awali. Lakini kwa awamu hii nashauri waache matetea wako wapumzike wala usiwapatie mayai mengine tena.

JINSI YA KULEA VIFARANGA
Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuetamia, andaa chumba kwa ajili ya kulea vifaranga. Safisha kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.

Washa taa ya joto au weka chombo cha kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla huja anza kuingiza vifaranga wako. Weka pia chakula na maji ya kutosha katika vyombo vyenye umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia. Tandaza magazeti, maboksi, makaratasi n.k katika sakafu ya chumba hicho. Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao watakufa ili ufanikiwe katika jambo hili, banda lako liwe la mduara katika kona zake.

Weka joto la kutosha. Joto la kutosha ni lile linalowafanya vifaranga watawanyike chini ya chanzo cha joto wakati kama joto limezidi vifaranya kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujukusanya chini ya chanzo cha joto.

Baada ya siku 3 utawapatia chanjo ya Gumboro na siku 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa chanjo hii baada ya mwezi mmoja kisha utafanya hivi kila baada ya miezi mitatu mitatu.

MAPATO YA MRADI WAKO
Katika uzazi wa kwanza utapata vifaranga 150 kwa wastani wa vifaranga 15 kwa kila kuku. Tuseme haujazingatia kanuni za ufugaji za makala hii ukapata vifaranga 100 yani wastani wa vifaranga 10 kwa kila kuku. Kisha baadaye wakakua wakafa kuku 50 yani watano kwa kila kuku utakuwa na jumla ya kuku 50.

Baada ya wiki 3 utapata tena kuku tufanye kwa mahesabu kama hayo hapo juu kwa hasara utakuwa na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa kuku wako baada ya uzao wa pili uliwapumzisha kwa miezi miwili basi mwezi wa 3 utapata tena kuku vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata wengine 100. Kwa mahesabu kama hayo awali wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa.

Baada ya miezi 6 utakuwa na kuku wakubwa wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili kuku 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.

Katika kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Ikiwa kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwishoni utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku wengine 900 toka katika kutoka kwa uzao wa kwanza, wapili na watatu. Hivyo mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.

Ukiuza majogoo yote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujenga miundombinu bora maana sasa utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana kwa kasi utapata pesa kiasi cha TZS 7,200,000/=. Sasa ongeza kuku wako wa kutaga hadi wafikie kuku 4,000 maana sasa utakuwa na pesa za kutosha kuendesha mradi wako.

Sasa ukiwa na kuku 4000 wa kienyeji wa kutaga mayai, ikiwa kuku 3000 tu watataga ukauza yai moja kwa bei ya haraka haraka ya TZS 250 tu, utapata TZS 750,000/= kwa siku ambayo sawa na TZS 22,500,000/= kwa mwezi na TZS 270,000,000/= kwa mwaka sawa sawa na 128,572 USD. Kumbuka mwamba makadilio haya niya chini sana. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukimtanguliza Mungu utafikia hata TZS 500,000,000/= kwa mwaka.

Kumbuka unapofanikiwa kupata mapato ya kila aina, umtolee Mungu zaka(x10%) ya mapato yako, pia ukatoe sadaka ambayo ni kubwa kuliko zaka na uwasaidie masikini na wahitaji.

Tunza kumbukumbu zako zote za fedha katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi ya mradi wako. Pia hali ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo ya mwisho, siku walipoanza kuetamia, magonjwa yanayowasumbua mara kwa mara n.k

Sifa za mwanamke asiyefaa kuolewa

Fahamu sifa za mwanamke asiyefaa Kuolewa asilani

SUALA la kuoa lipo tu licha ya kwamba wapo wanaochelewa kuingia kwenye maisha hayo wakihisi inaweza kusitisha furaha ya maisha yao. Nasema hivyo kwa kuwa najua wapo wanaoamini kuoa ama kuolewa ni kujiingiza kwenye matatizo.

Dhana hiyo haina mashiko kiviile, asikuambie mtu unapoingia kwenye ndoa na mtu anayekupenda na wewe unampenda kwa dhati, karaha hakuna licha ya kwamba kugombana kwa hapa na pale hakuwezi kukosekana.

Hata hivyo, nikiri tu kwamba, zipo ndoa ambazo ni ndoano. Yaani unakuta mtu kaingia kwenye ndoa na mtu ambaye hakuwa amedhamiria, matokeo yake kadiri siku zinavyokwenda anahisi ameingia chaka na anaishia kuomba ndoa isiwepo.

Leo nataka kuwazungumzia wanawake ambao ni majanga na ukijichanganya ukaingia nao kwenye maisha ya ndoa, utakiona cha mtemakuni.

10. Asiyeridhika na penzi unalompa
Wapo wanawake ambao wewe unaweza kujitahidi kumpatia mapenzi kadiri unavyoweza lakini yeye hatosheki. Anakuchukulia wewe ni dhaifu sana na wakati mwingine kuhisi yupo mwingine anayeweza kumpa zaidi ya kile unachompa, huyu ni tatizo.

9. Wivu kupindukia
Hatukatai, wivu ni muhimu sana kwenye suala la mapenzi lakini kuna ule wivu uliopindukia kiasi cha kuwa kero. Walio kwenye ndoa wananielewa namaanisha nini.

Kwa kifupi mtu mwenye mapenzi ya dhati na mwenziye lazima awe na wivu lakini ukiwa na ule wa kupinduki ni tatizo linaloweza kuitibua ndoa.

8. Anaona unamsaliti kila mara
Huku kunatokana na kutokujiamini tu. Ukioa mwanamke ambaye kila wakati unapokuwa mbali naye anahisi unamsaliti, huyo hakuamini na kamwe hamuwezi kudumu. Mara kadhaa mtakuwa mkigombana akihisi una mwingine kumbe hakuna ukweli katika hilo.

7. Anahisi amekosea kuwa na wewe
Wapo wanawake ambao wanapoingia kwenye ndoa baada ya muda wanahisi wamekosea kuolewa na mwanaume huyo. Unakuta mke wa mtu anahisi fulani ambaye zamani alikuwa kwenye uhusiano naye angekuwa sahihi zaidi baada ya kuona upungufu fulani kwa huyo aliyemuoa.

6. Yuko kimasilahi zaidi
Kuna wanawake ambao ukiwaoa wanakuwa na furaha na wewe ukiwa unazo tu, ukiishiwa wanaanza kununa na kuleta visirani vya hapa na pale. Hawa ni tatizo, mwanamke wa kweli ni yule anayeridhika kuwa na wewe kwenye shida na raha

5. Yuko tayari kuachana na wewe
Hivi hujawahi kumsikia mke wa mtu akimwambia mumewe; ‘Kama vipi tuachane, kwanza kwetu sijafukuzwa na nilikuwa nakula, nalala, navaa.” Mwanamke anayeweza kumtamkia mume wake maneno haya, huyo si mke na kamwe hawezi kukufanya uwe na furaha.

4. Hapendi ndugu zako
Waswahili wanasema ukipenda boga, penda na ua lake. Kama utatokea kuoa mwanamke ambaye anakupenda wewe tu lakini akija ndugu, rafiki au mtu mwingine wa karibu yako anabadilika, huyo ana matatizo kwani atakufanya utengwe na jamii yako.

3. Anajali mafanikio binafsi
Siku zote wawili waliotokea kupendana wakioana wanakuwa mwili mmoja hivyo lazima watakuwa wanawaza na kufanya maamuzi pamoja.

Ogopa sana mwanamke anayependa kutumia kipato chake kufanya mambo binafsi tena kwa siri. Kwa mfano kusaidia kwao, kujenga nyumba kwao, kuanzisha miradi yake bila kukushirikisha.

2. Eti akizaa utamzeesha
Hili kwa wale wanaopenda kuoa masistaduu. Wapo ambao wakitajiwa suala la kuzaa mara baada ya kuingia kwenye ndoa wanagoma wakidai eti watazeeshwa hivyo waachwe kwanza wale ujana. Wakati huo unaweza kukuta mwanaume anataka mtoto ili apate ile heshima, mke anagoma kwa sababu hiyo isiyo na msingi, hili ni tatizo.

1. Anataka awe na sauti
Mwanaume siku zote atabaki kuwa kiongozi wa familia lakini wapo baadhi ya wanawake hawataki kukubaliana katika hilo. Wengi wanalazimisha usawa na wengine wakitaka wao ndiyo wawe na sauti kuliko wanaume zao.

MAJALIWA:WATUMISHI WAZEMBE HAWATAKIWI HALMASHAURI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema wakati umefika wa kuwa na watumishi wenye weledi wa kutosha kwenye Halmashauri zote nchini na pia hazitakiwi kuwa pango la wezi, wazembe au jalala la kutupa wabadhilifu walioshindikana kwingineko.
Aidha, Waziri Mkuu amesemma Serikali za Mitaa na Halmashauri zote nchini zinatakiwa zianze kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi kuona ni kwa namna gani zitakuwa chachu ya maendeleo ya viwanda vinavyotarajiwa.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati akifungua Kikao cha Baraza la Mashauriano (RCC) mkoani Dodoma. amesema kikao ni chombo muhimu na endapo kitatumika vizuri kitaweza kusaidia kusukuma maendeleo ya Mkoa na kupunguza migogoro kwenye Halmashauri.

Aidha, Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuongeza kiwango cha ruzuku kwa Halmashauri zote nchini kwa kadiri uwezo utakavyoruhusu na kusisitiza kwamba fedha hizo lazima zisimamiwe vizuri na zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo inayowagusa wananchi.

“Endapo itabainika kwamba kuna baadhi ya Sheria zinazokwamisha utendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hatutasita kuzifanyia mapitio na hatimaye kuzibadili ili ziendane na azma yetu ya kutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema Majaliwa.

 

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema vyanzo vingi vya mapato ya Serikali vinapatikana kwenye Halmashauri huku changamoto kubwa ikiwa ni kulegalega kwa  Halmashauri nyingi katika ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya kodi jambo linalozorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi.

 

MWANAHALISI LIOMBE RADHI

Gazeti La Mwanahalisi Lapewa Saa 24 Liombe Radhi

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA KATIBU WA UNO

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mataifa (UN)




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.

PICHA NA IKULU

Mkutano wa 6 kuanza leo DODOMA

Mkutano Wa 6 Wa Bunge Kuanza Kesho.....Wabunge 4 Kula Kiapo, Maswali 125 Kuulizwa Na 16 Ya Papo Kwa Papo Kwa Waziri Mkuu

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Masiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akizungumza na wanahabi mjini Dodoma leo akitoa taarifa ya yale yatakayojiri katika Mkutano wa sita wa Bunge la 11 unaotaraji kuanza kesho Januari 31 hadi Februari 10 mwaka huu mjini Dodoma.

***************
Mkutano wa Sita wa Bunge unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 31 Januari 2017 na kumalizika tarehe 10 Februari 2017 Mjini Dodoma. 

Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-
 
1.0         KIAPO CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-
(i)         Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo
(ii)       Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi
(iii)      Mhe. Anne Kilango Malecela
(iv)    Mhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)
 
2.0         MASWALI
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi. 
 
3.0       KAULI ZA MAWAZIRI
Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa  kama ifuatavyo:-
(i)     Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
(ii)   Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
 
4.0       MISWADA YA SHERIA
Katika Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika mwezi Novemba, 2016 Miswada mitatu (3) ya Sheria ilisomwa  kwa mara ya Kwanza Bungeni na kupelekwa kwenye Kamati husika ili ifanyiwe kazi. 
 
Hivyo katika Mkutano huu wa Sita Miswada hiyo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni kwa mara ya Pili, kujadiliwa na kupitishwa na Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 91. Miswada hiyo ni:-
Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).
Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)
Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA
30 Januari, 2017.

MWENYEKITI MPYA UMOJA WA AFRIKA

Rais wa Guinea achaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika (AU)

Rais wa Guinea, Alpha Conde amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika (AU), uchaguzi uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi wanachama vinavyoendelea katika Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Rais Conde anapokea uongozi kwa Rais wa Chad Idris Deby ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa umoja wa hadi.

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ni kiongozi asiye na maamuzi (ceremonial head of the Union). Mwenyekiti huyu huchaguliwa  na Marais wa Nchi wanachama wa AU ambaye hushika wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu. Uongozi huu huenda wa zamu katika Kanda tano za bara la Afrika (Kaskazini, Kusini, Mashariki, Magharibi, na Afrika ya Kati).

Nafasi hii ilianzishwa mwaka 2002 ambayo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza.

Rais wa Chad,  Idriss Deby (kushoto) akikabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Rais Alpha Conde wa Guinea (kulia).

PONGEZI KWA MKUU WA MKOA GEITA KWA KUWAOKOA WACHIMBAJI

Makamu wa Rais atuma salamu za pole na pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa Kuwaokoa Wachimbaji Waliofukiwa na Kifusi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za pole na pongezi Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa kazi nzuri na kubwa waliyoifanya ya kuwaokoa wachimbaji wadogo 15 waliofukiwa na maporomoko ya udongo kwenye Mgodi wa Dhahabu wa RZU uliopo katika Kijiji cha Nyarugusu, wilaya ya Geita katika mkoa wa Geita.

Tukio hilo la kufukiwa wachimbaji hao wadogo 15 wakiwemo Watanzania 14 na raia Mmoja wa China lilitokea usiku wa Tarehe 26 Januari mwaka 2016.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa furaha taarifa za kuokolewa kwa wachimbaji hao wadogo na amesifu na kupongeza jitihada za kuwaokoa wachimbaji hao  zilizofanywa na Serikali ya Mkoa wa Geita, Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa mkoa wa Geita, Wamiliki wa Migodi ya Dhahabu na wananchi kwa ujumla kwa kutoa vifaa mbalimbali vya uokoaji jitihada ambazo zimepelekea kuokolewa kwa wachimbaji hao wakiwa hai.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa “jitihada ,Umoja na Mshikamano ulioonyeshwa na makundi mbalimbali katika kuwaokoa ndugu zetu waliofukiwa na maporomoko ya Udongo wakiwa kazini huko Geita ni mfano mzuri na wakuigwa na wananchi na taasisi nyingine nchini katika kujitolea kwa hali na mali hasa vifaa vya uokoaji kwa ajili ya kusaidia watu wanaopatwa na majanga ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama walivyofanya ndugu zetu wa mkoa wa Geita nawapongeza Sana”.

 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wamiliki wa migodi kote nchini wahakikishe wanafanya kazi zao za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria kama hatua ya kuepuka madhara yanayoweza kutokea wakiwa wanafanya shughuli zao za uchimbaji wa madini.

Kupitia kwako Mkuu wa mkoa wa Geita napenda kutuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kutokea kwa tukio hilo na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wachimbaji hao ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu Katika Hospitali ya Serikali ya mkoa wa GEITA matibabu mema ili waweze kupona haraka na kurejea kwenye kazi zao za kujitafutia riziki.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Kudhibiti Maafa nchini, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita na kupekelea kuchukuliwa hatua za haraka katika kushughulikia ajali hiyo.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dar es Salaam           

29-Jan-2017

DAKTARI AJIUZURU BAADA YA MKUU WA MKOA KUMUWEKA RUMANDE

Daktari Aandika Barua ya Kuacha Kazi Baada ya Mkuu wa Mkoa Kumuweka Rumande Kwa Kosa la Kipindupindu
MPEKUZI / 9 hours ago

Mganga  Mkuu wa Wilaya ya Singida Vijijini, Dk. Erick Bakuza ameandika barua ya kuacha kazi

Dk. Bakuza amechukua uamuzi huo ikiwa ni siku chache tangu alipopewa adhabu ya kuwekwa mahabusu na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Rehema Nchimbi.

Dk. Nchimbi alitoa amri ya kukamatwa kwa daktari huyo kutokana na kuzuka ugonjwa wa kipindupindu ambao ulisababisha vifo vya watu wawili mwishoni mwa mwaka jana.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Rashid Mandoa jana alithibitisha kuacha kazi kwa Dk. Bakuza.

“Ni kweli amewasilisha barua ya kuacha kazi lakini ninavyojua mimi si kweli kwamba ameacha kazi kutokana na adhabu aliyopewa na Mkuu wa Mkoa ya kuwekwa ndani.

“Kwanza ujue hakuwekwa ndani, na ameamua kuacha kazi kwa sababu amepata sehemu nyingine ambayo anaona ina maslahi anayohitaji yeye,” alisema.

Juhudi za kumpata Dk. Bakuza kuzungumzia hatua yake hiyo hazikuzaa matunda.

Kauli ya Mkuu wa Mkoa
Wakati Mkurugenzi huyo akisema kwamba Dk. Bakuza hakuwekwa ndani, Mkuu wa Mkoa huyo, Dk. Nchimbi alithibitisha kwamba aliwekwa ndani kwa   saa tatu.

“Mimi nilitoa amri ya kukamatwa Daktari huyu na aliwekwa chini ya ulinzi kwa saa tatu.Nilimuweka ndani kwa sababu ya mazingira ambayo niliyakuta nilipokuja kuanza kuitumikia nafasi niliyoteuliwa ya ukuu wa mkoa, na nitatetea uamuzi wangu huo.

“Niliamuru akamatwe kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, kesi ya kwanza ya kuwapo kwa mgonjwa wa kipindupindu iliripotiwa Novemba 26, mwaka jana.

“Utaratibu unajulikana wazi kwamba ikifika kesi tano DMO (Mganga Mkuu wa Wilaya) anatakiwa atoe taarifa kwa MRO (Mganga Mkuu wa Mkoa).

“Desemba 4   hakutoa taarifa, ilipofika Desemba 16 vikatokea vifo viwili hakutoa taarifa hadi Desemba 18 ndipo akatangaza.

“Nikaona hakuwa makini katika kazi yake kwa sababu alipaswa kutangaza mapema ili tuchukue hatua za kudhibiti ugonjwa huo na naamini hata hivyo vifo visingetokea,” alisema.

Dk. Nchimbi alisema suala la kipindupindu halipaswi kuchukuliwa kisiasa na kwamba lenyewe lipo kitaalamu zaidi.

“Kuna taratibu ambazo hufuatwa lazima tupate evidence ya kutosha, watu wachukuliwe vipimo, yeye alinyamaza kimya. Wataalamu walipokwenda kuchunguza wakagundua kuna kipindupindu kwenye wilaya yake,” alisema.

Aliongeza: “Kwa hali hiyo niliona hakuwa makini katika kazi yake, hivyo nilitaka kumshtua tu awe makini, hakuwa makini.

“Katika hali ya kawaida angesema mapema tungechukua hatua mapema, tungetibu maji, tungesafisha visima na hata vifo visingetokea,” alisema.

Maalim Seif afunguka.

Maalim Seif Afunguka Mambo Mazito.......,Adai Muda si Mrefu Atakuwa Rais wa Zanziba, Asema Yupo Tayari Kwa Maridhiano
MPEKUZI / 8 hours ago

Aliyekuwa  mgombea urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema yupo tayari kufanya tena maridhiano endapo pande zote mbili zitakubali kwamba Zanzibar kuna matatizo.

Maalim Seif aliyasema hayo jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni ya AZAM na kuongozwa na mtangazaji nguli nchini, Tido Mhando.

Alisema maridhiano yaliyofanyika akiwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume,  yalikuwa na manufaa makubwa kwa kuwa Zanzibar ilikuwa na amani na utulivu.

Maalim Seif alisema CUF iliamua kukaa na Karume baada ya kuona uchaguzi ulikuwa unakaribia kufanyika hivyo ikaamua kufanya kikao cha muafaka wa maridhiano na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iliyozaa matunda.

Alisema baada ya kufanyika maridhiano na kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais alikuwa na nafasi kubwa ya kumshauri Rais mambo mbalimbali.

 “Hata kulipokuwa na SUK (Serikali ya Umoja wa Kitaifa),  mambo yalikuwa mazuri na maelewano na hata ilikuwa ikitokea mtu akifika ofisini anashindwa kufahamu CUF ni nani na CCM ni nani,’’ alisema Maalim Seif.

Alisema  hata sasa kama kuna nia njema ya kufanyika mazungumzo yafanyike kwa sababu  kwa sasa Zanzibar kuna matatizo na uhasama unazidi kupamba moto.

Maalim Seif pia alizungumzia suala la kufutwa  Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka 2015 na marudio yake Machi 20 mwaka jana.

Alisema yeye alishinda kwa kura nyingi na hivyo kama uchaguzi ungekuwa huru na haki yeye ndiyo alistahili kutangazwa kuwa Rais wa Zanzibar na si vinginevyo.

Alisistiza kwamba hatambui uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka jana  kwa kuwa hakushiriki na wala hakuwa na sababu ya kushiriki kwa kuwa mshindi alishapatikana Oktoba 25, mwaka juzi.

“Nisingeweza kukubali kurudia uchaguzi ule kwa kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC) alifuta matokeo yale ili CCM kwa njia zozote zile ishinde kwenye uchaguzi wa marudio.

“Hawakuweka mpira  uwanjani urudiwe eti kwa sababu washindwe  si kweli, hivyo wangetumia mbinu zozote ili washinde ,’’alisema Maalim Seif.

Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema ni kosa kukaa kimya wakati bado suala   la uchaguzi linafanyiwa kazi ili ufumbuzi upatikane.

Alisema  hilo  ni kama bomu ambalo likiripuka  hali itakuwa mbaya.

Mtangazaji alimuuliza MaalimSeif kama hakuona kuwa ni kosa kujitangazia   ushindi?

Alisema alifanya hivyo baada ya kuona kwamba ZEC ilikuwa anataka kumtangaza Dk. Shein (Ali Mohamed Rais wa Zanzibar) kuwa ni mshindi  huku hakushinda.

Hata hivyo alisema kama waliona amefanya makosa basi wangemkamata na kumpeleka mahakamani.

Alisema bado ana matarajio ya kuwa Rais wa Zanzibar katika   muda mfupi ujao.

Kuhusu uchaguzi wa 2020, alisema  ataangalia hali ya siasa ijayo.

 Mgogoro ndani ya CUF
Akizungumzia mgogoro ndani ya chama hicho, alisema  unachangiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Alisema Profesa Ibrahimu Lipumba aliamua kuondoka yeye mwenyewe.  “Lakini cha kushangaza baada ya miezi 10 akarudi sijui ni kwa misingi gani?” alihoji.

Alisema Katiba iko wazi kwa mtu anayejiuzuru, ni kwamba anaandika barua kwa Katibu Mkuu na Katibu anapeleka barua kwenye Mkutano Mkuu.

Alipoulizwa mbona alipokabdhiwa barua hakuitisha mkutano wa kumridhia Lipumba kujiuzulu, alisema hawakuweza kuitisha mkutano ghafla kwa kuwa chama hicho ni kidogo na hakikuwa na fedha.

‘’Lakini tuliitisha Mkutano Mkuu akajadiliwa, cha kushangaza yeye anang’ang’ania kuwa ni mwenyekiti, hii inashangaza haiwezekani katika hili!’’ alisema.

Alisema hata Msajili anafahamu kurudi kwa Lipumba ni lazima akubaliwe na Mkutano Mkuu.

Hata hivyo, alisema katiba ya chama haisemi mtu anayeondoka akae na baadaye aamue kurudi kwa sababu  hawafahamu kama ana nia njema na chama au la ikizingatiwa  pia alikiacha chama  katika kipindi kigumu cha uchaguzi mkuu.

Seif alisema kutokana na Msajili wa Vyama vya Siasa kuendelea kumtambua Profesa Lipumba licha ya kujiuzuru yeye mwenyewe, CUF kimeamua kwenda mahakamani  kuweza kupata tafsiri ya sheria.

“Mgogoro huu ulipandikizwa kwa wazi kabisa na Lipumba wakati anajiuzuru  tulimfuata na viongozi mbalimbali, wa dini wa chama wazee na vijana asitoke lakini alikataa kuendelea kubaki kwenye nafasi hiyo,’’ alisema.

Maalim Seif alisema kwa kufanya hivyo imeonekana kuwa Lipumba hakuwa na msimamo kwa kuwa yeye ndiye aliyewaletea aliyekuwa mgombea urais akiwakilisha Ukawa, Edward Lowassa, huku akisema kuwa kila alipokuwa akipita vijiweni, Lowassa alikuwa akitajwa tajwa sana na wananchi.

Alisema  yeye na wenyeviti wenzake wa   Ukawa walimtangaza Lowassa, hivyo Lipumba kubadili msimamo kulionyesha dhahiri kwamba tayari kulikuwa na nguvu nyuma yake iliyokuwa ikimshawishi  na hata baada ya kujiuzuru iliendelea kufanya hivyo.

Maalim  alisema baada ya Lipumba kukaa pembeni CUF kilipata mafanikio makubwa kwa vile kilipata viti vya ubunge 10 upande wa Bara na halmashauri nne ambazo ziliundwa na chama hicho  peke yake.

Alisema  hata katika uchaguzi mdogo wa marudio wa hivi karibuni, Lipumba alisimamisha wagombea katika kata 11 lakini hakuambulia kiti hata kimoja zaidi ya wagombea kupata kura 10 ,11,12.

Alipoulizwa hatima ya CUF kwa sasa,   alisema hiyo si mara ya kwanza kwa vile  kuna migogoro mikubwa ilipita huko awali ukiwamo wa Hamad Rashid Mohamed lakini ulikwisha.

Kuhusu kama ana mpango wa kuunda chama kingine, alisema ni hisia za watu tu na kwamba hana mpango huo.

Alisema  yeye ni mmoja wa waanzilishi wa CUF akiunda chama kingine ataonekana kuwa ni msaliti.

“Siwezi kuunda chama kingine nikaachana na CUF, mimi ni CUF kindakindaki na nitaendelea kuwa CUF kindakindaki  ndani ya chama ,’’alisema.

Alisema CUF kimeamua  kupeleka mahakamani  mgogoro huo na hata kama mahakama itampa Lipumba ushindi  watakata rufaa ingawa hawatarajii hilo.

Maalim Seif  alikiri kwamba bila vyama vya upinzani kuungana ni vigumu kukiondoa  CCM madarakani na ndiyo sababu ya kufanya hivyo.

Mgogoro wa ruzuku
Alimshangaa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kutoa ruzuku kwa Profesa Lipumba   kupitia akaunti nyingine ambayo si ya chama makao makuu.

Alisema Msajili aliwaandikia barua kusema kuwa  ruzuku isingetolewa kutokana na chama hicho kuwa na mgogoro, lakini  baada ya muda wakashangaa imepitishiwa katika akaunti ya wilaya ya Temeke.

Kuhusu kushindwa uchaguzi wa marudio, Dimani alisema siyo kwamba wameshindwa bali   Dimani ni jimbo la CCM  na hata hivyo kama   demokrasi CCM ingetumika isingeshinda.

Maisha baada ya kustaafu
Maalim Seif alisema licha ya kustaafu anapata haki zake zote kisheria siyo kuomba.

Haki hizo ni pamoja na gari, walinzi na posho kila mwezi ingawa alisema matibabu anajigharamia mwenyewe   kwa kuwa akiomba ananyanyaswa.

Meli kubwa ya lisasa ya Azam

Picha: Meli kubwa ya kisasa ya Azam yatia nanga Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza
MPEKUZI / 7 hours ago

Meli mpya na ya kisasa iitwayo AZAM SEALINK 2 aina ya RORO yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na magari 150 imetia nanga
Bandari ya Tanga leo.

Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki.





Visit website

Friday, 27 January 2017

Magazeti ya Tanzania January 28, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo



January 28 2016 naanza kukusogezea post zote kubwa kwenye zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye,Hardnews na Michezo ili uje kinachoendelea Mtu wangu usiache kukaa karibu yangu 




























Tuesday, 24 January 2017

MBINU YAKUFANYA WASOMAJI WAKO WAVUTIWE NA HABARI ZAKO

“Je! Unaandika post lakini hazivutii wasomaji kuzisoma? Tazama mambo ya kuzingatia ili itie mshawasha” 

Wateja wa blog yako hawasomi post zako kwa sababu tu zina ujumbe mzuri, la hasha! Ila pia kwa kuwa zinavutia machoni na zinawafanya wajihisi wepesi kuanza kuzisoma. Kama post yako itakuwa ni maneno tu yamejaa kurasa yote humfanya msomaji ahisi kuwa atachukua muda mrefu kusoma na kuchanganua kilichoandikwa. Lakini kama itakuwa imepangiliwa vizuri basi hatoona wingi wa maneno na ataanza kuelewa kinachozungumziwa kabla hajamaliza kusoma.

Vifuatavyo ni vitu vitakavyomtamanisha msomaji asome post yako

1. Vichwa vya habari vya chapisho

Kazi iliyopangiliwa kwa kuwa na vichwa vya habari vinavyotambulisha kila wazo katika post yako humfanya msomaji aelewe anachokisoma baada tu ya kuona kichwa hicho. Mfano ukiandika post kisha baada ya kichwa cha post yakajaa maelezo tu hadi mwisho itamlazimu msomaji aisome kazi yote ndio apate picha ya kinachozungumziwa. Lakini kama baada ya kichwa cha habari kikuu ukaandika aya moja kisha kikafata kichwa cha habari kidogo kisha maelezo yake, kisha vivyo hivyo mpaka mwisho, kutamfanya msomaji aelewe habari nzima kwa kusoma vichwa vya habari tu na hivyo huwa mwepesi kuisoma kazi nzima. 

2. Picha katika blog

Picha hutoa ujumbe kwa wepesi zaidi kuliko maneno elfu moja. Matumizi ya picha hupunguza mlundikano wa maneno pamoja na humpa msomaji kitu cha kujiburudisha akiwa katika post yako. Humfanya msomaji apate ujumbe wa kinachozungumziwa na kukumbuka kwa wepesi zaidi ujumbe ule. Picha inaweza ikawa ni ya kupiga kwa kamera, mchoro, chati ama jedwali. Ni muhimu tu kuzingatia masuala ya haki miliki unapotumia picha.

3. Listi/orodha katika blog

Kutumia listi ni kujaribu kuyapanga mawazo yako katika mtiriliko ambao utakuwa na vichwa vya habari na namba ama nukta. Listi hufanya post ionekane nyepesi na yenye kusomeka. Jitahidi kutumia listi katika post zako ambazo zinaruhusu listi. Post hii ni mfano mzuri wa matumizi ya list.

4. Rangi za blog

Si kila post itakuwa na rangi yake, la hasha! Ila mpangilio mzuri wa rangi katika post zako hupendezesha post na kuonekana ni za maana hata kama yaliyomo hayafikii kiwango hicho cha umaana. Jaribu kutumia rangi tofauti katika kichwa cha habari kikuu, vichwa vidogo, linki na maneno yaliyobaki. Kwa kawaida kuseti rangi huwa kunafanyika wakati wa kudizaini blog yako.

5. Video katika blog

Video zina faida kama ilivyo picha ila kwa video ni zaidi. Kuna aina ya watu ambao huwa wanauwezo mkubwa wa kujifunza kwa kusikia kuliko kusoma hivyo kwa video na sauti watavutiwa zaidi na blog yako. Zipo tovuti ambazo unaweza kuweka video zako bure kisha ukaziunganisha katika blog yako.

NJIA ADIMU ZA KUONGEZA WATEMBELEAJI KWENYE BLOG YAKO

Kama tayari umeshafungua Blog yako, basi hongera kwa hilo kwani hiyo ni hatua kubwa ambayo kila Blogger aliyefanikiwa amepitia. Sasa kinachofuata ni nini cha kufanya ili kuhakikisha watu wanaokuja kutembelea Blog yako hawakauki na wanaongezeka kila leo. Lazima tuwe na dhamira ya kufika mbali na kwamba tumeamua ku blog ili tupate kipato na si vinginevyo, japokuwa tunaweza kufungua blog kama sehemu ya Kujifurahisha lakini furaha hiyo italeta tija kama una kipato kinapatika ndani ya kujifurahisha huko.
Zifuatazo ni Miongoni mwa mbinu Unaweza zitumia Blogger ili kujihakikishia watembeleaji wa kudumu na wapya kuongezeka kila leo:-
1.Kuandika Mada/Topic nzuri zenye kuvuta hisia.
Hii ni muhimu sana kwani baada ya kutambua wasomaji/wafutiliaji wako basi yafaa kutambua ni mada gani zinawagusa zaidi na zitawafanya warudi kila leo.


2.Kuchangia katika blog nyingine za kufanana na yako
Pia uwe na tabia ya kutoa comment au kutoa mada katika blog nyingine zenye muingiliano na yako huku ukiacha link ya mada zako katika blog hizo.
3.Kutumia vizuri SEO Tools ili kupatikana kirahisi mtandaoni
Zipo SEO Tools nyingi za bure ambazo husaidia blog yako kupatikana kirahisi mtandaoni kupitia keywords katika search engines mfano Google, miongoni mwa hizo ni Attracta.
4.Kujitanua ki network kupitia Mitandao ya kijamii mfano Facebook.


Kupitia mitandao hii unaweza kupata wafuatiliaji wa kutosha kwani wengi tayari huwa ni marafiki au jamaa zako, pia huwa na element ya kutaka kuona ni jinsi gani mwenzao unafanya.
5.Uwe na ratiba nzuri yak u post, usikae kimya muda mrefu.


Ikiwa umefungua Entertainment Blog, News Blog au Gossip Blog basi zisipite siku mbili bila ku post vitu vipya katika blog yako ili watu wawe na imani ya kupata kile wanachokitarajia katika blog hiyo, lakini ikiwa ni education au informative blog basi hata siku nne si mbaya.
6.Topic zako zisiwe nje ya Muonekano wa blog yako (Niche)
Kama ni taarifa basi ziwe taarifa za kweli, si za kutunga na ziwe zina uhusiano na Dira ya Blog yako, usitoke nje ya mada na uwe na Dira yenye tija.
7.Usiweke “MAVITU” Mengi Katika Blog yako kwani Huweka uzito wa Ku load.
Si kila Plugin ni nzuri kwa blog yako, nyingine hufanya pages zako ku load taratibu mno, hii huwakera wanaokuja kutembelea blog yako.

Jinsi Ya Kutengeneza Fedha Kwenye Mtandao Kwa Kutumia Blog.

Wiki chache zilizopita AMKA MTANZANIA iliendesha mafunzo mafupi ya jinsi ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog. Mafunzo haya yalikuwa na mafanikio makubwa sana kwani washiriki walijifunza mbinu mbalimbali za kuweza kukuza blog zao na kuzibadilisha kuwa biashara.
Pamoja na kutoa muda mrefu wa kujiunga na mafunzo haya, bado kuna watu wengi sana ambao waliyakosa mafunzo haya. Baada ya mafunzo kuisha kila siku kumekuwa na watu ambao wanahitaji kupata mafunzo haya. Ni vigumu kurudia kuendesha tena mafunzo haya kwa sababu kuna vitu vingi vya kufanya wakati wa kuendesha mafunzo ndio maana kuna ratiba maalumu za kuendesha mafunzo.
Kwa kuwa elimu hii ni muhimu sana na inaweza kumkomboa mtanzania yeyote anayetaka kutengeneza kipato kikubwa nimeona sio busara kwa watu wengi kuikosa elimu hii. Hivyo nimetoa kitabu kinachoitwa JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Kitabu hiki kimejaa mbinu muhimu za kutengeneza fedha ambazo ainafanya kazi kwenye mazingira yetu ya kitanzania na ndio huwa nazitumia kila siku.
Katika kitabu hiki utajifunza jinsi ya kutengeneza blog hata kama hujui kabisa na jinsi ya kuikuza na kuifanya kuwa biashara kubwa.
Kitabu hiki kina mafunzo yafuatayo;
1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.
2. Jinsi ya kutengeneza blog
3. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.
4. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.
5. Uandishi wa makala zenye mvuto.
6. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).
7. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.
8. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.
9. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.
10. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.
11. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.
Masomo hayo yameelezewa kwa lugha rahisi na wakati mwingine kwa kutumia picha ili kuweza kukurahisishia wewe kuelewa.
COVER
Pata kitabu hiki mara moja ili uweze kutengeneza misingi yako ya kuweza KUTENGENEZA KIPATO KISICHO NA KIKOMO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.
Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa PDF na kinatumwa kwa njia ya EMAIL.
Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi(10,000/=) unatuma fedha hiyo kwa MPESA-0755953887 AU TIGO PESA-0717396253 kisha unatuma email adress yako kwa meseji kwenye moja ya namba hizo na unatumiwa kitabu mara moja.
Pata kitabu hiki na uanze kujenga misingi ya kutengeneza pesa kupitia mtandao. Uzuri wa kutengeneza pesa kwenye mtandao ni kwamba hakuna kikomo na unaweza kufanya kazi popote ulipo. Kikomo cha kiwango cha fedha unachoweza kutengeneza unaweka mwenyewe, ukiwa na juhudi na maarifa kipato kinakuwa kikubwa. Unaweza kufanyia kazi zako ofisini, nyumbani au sehemu yoyote unayoona ni nzuri kwako.
Kupitia kitabu hiki unapata nafasi kubwa ya kuyaboresha maisha yako.
Karibu sana upate kitabu hiki ambacho kitaboresha maisha yako kwa kiasi kikubwa sana.