Yajue Madawa ya kulevya aina na athari zake kwa mtumiaji
Tatizo la madawa ya kulevya limetokea kuwa janga kubwa duniani kote, watu wengi wameathirika na janga hili. jinsia zote wanaume, wanawake, na vilevile rika zote vijana na wazee pia.
Hapa tutaongelea aina mbili za madawa ya kulevya yaani Cocaine na Heroin.
Cocaine
Hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamuErythroxylum coca bush.

Aina hii ya dawa ya kulevya hutolewa kwa mifumo ifuatayo;
Unga ambapo mitaani hujulikana kama coke na hutumika kwa kuvutwa puani kama unga, au kuyeyushwa na maji na kuchomwa kwenye mshipa wa damu.
Crack ambapo mitaani hujulikana kwa jina hilohilo crack au rock, na hutengenezwa kwa kuchanganywa na kemikali. Na hutumika kwa kuvutwa kama sigara.

Cocaine pindi inapoingia kwenye damu huenda kwenye ubongo na kuzuia ufyonzwaji wa vihisishi vifuatavyo: dopamine, norepinephrine na serotonin, kutoka kwenye ubongo. Hivyo ubakia kwenye ubongo. Na vihisishi hivi husababisha ile hali ya furaha, mchangamfu na kujisikia mwenye nguvu kitaalamu euphoria. Na huweza kuwa kwenye hali hii kwa nusu saa tu.
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili zifuatazo hutokea

Mishipa ya damu husinyaa (constricted blood vessels)
Joto la mwili huongezeka
Mapigo ya moyo huongezeka
Shinikizo la damu
Dilated pupils
Joto la mwili huongezeka
Mapigo ya moyo huongezeka
Shinikizo la damu
Dilated pupils
Matumizi ya muda mrefu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara yafuatayo; Pamoja na kwenda kwenye ubongo husambaa sehemu nyingine za mwili na mzunguko wa damu
Moyo - Kwenye moyo huweza kuleta Shambulizi la moyo (heart attack) na vilevile mapigo ya moyo yasiyo na mpangilio (Arrhythmia) hivyo unaweza kufa ghafla tu.
Ubongo - Mishipa ya damu kwenye ubongo inaweza kusinyaa na kupelekea kupata Kiharusi, hata kwa kijana. Vilevile unaweza kupata ugonjwa wa akili (substance abuse pyschosis).
Mapafu na mfumo wa hewa - Uvutaji kupitia pua huweza kupelekea tatizo sugu la kutokwa damu puani kila wakati na mafua yasiyo pona, kupoteza mfumo wa harufu, na ikivutwa kama sigara kuharibu mapafu moja kwa moja.
Mfumo wa chakula - Cocaine husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu kwenye tumbo na utumbo hivyo kusababisha vidonda na kuweza kuharibu kabisa mfumo huu kwa utumbo kuoza.
Mafigo - kutokana na shinikizo la damu mafigo yanaweza kushindwa kufanya kazi vizuri, vilevile cocaine inaweza kuleta madahara moja kwa moja kwenye mafigo kitaalamu Rhabdomyolysis.
Ngono - ingawa cocaine huweza kutumika kama njia ya kuongeza hamu ya ngono huweza kusababisha kushindwa kumaliza kile ulichokianza. Matumizi sugu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara kwa jinsia zote yani kwa wanaume na wanawake.
Na vilevile huweza kufanya kuwa tegemezi wa dawa hii.
Kwa wanaotumia sindano na kushea wanaweza kupata maambukizi ya virusi ya hepatitis na vya ukimwi.

Nini hutokea baada ya matumizi ya muda mrefu ya kokeni?
Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;

Unyogovu
Uchovu
Kushindwa kuzingatia na kutokuwa makini
Kukosa uwezo wa kuwa na furaha au kusikia raha
Kuongezeka kwa tama zaidi ya kutumia cocaine
Kujisikia kuumwa, maumivu, baridi na kutetemeka.

Ikitokea mtu akitumia zaidi ya kiwango kinachotakiwa kwa muda mfupi yaani overdose, kifo cha ghafla huweza kutokea kutokana na madhara yafuatayo;
Moyo kushindwa kufanya kazi
Kiharusi
Degedege mara kwa mara
Mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi
Kiharusi
Degedege mara kwa mara
Mfumo wa hewa kushindwa kufanya kazi
Heroin
Hujulikana vilevile kama diamorphine, hutokana na mmea huitwao kitaalamu opium poppy. Heroin kwa mfumo wa Morphine hutumiwa hospitalini kama dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu kwenye kansa. Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa.

Aina hii ya dawa ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa kuchoma kwenye mshipa. Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na kwenye uke, ambapo kuta hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya sekunde arobaini.
Heroin mara tu baada ya kuingia kwenye damu kuenda kwenye mfumo wa neva na kukandamiza ufanyaji kazi wake, ndio huweza kutumika kupunguza maumivu.
Dalili za mtu aliyetumia heroin
Dalili ambazo hutokea mara tu anapotumia Heroin:

Kujisikia mwenye furaha na raha
Kupishana Kusikia hali usingizi na tahadhari
Midomo kuwa mikavu
Misuli kuishiwa nguvu
Kuhema polepole
Warm skin flushing
Mikono na miguu kuwa mizito
kope za macho kulegea

Nini madhara ya matumizi ya muda mrefu ya heroin?
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama

Maambukizi kwenye kuta na milango ya moyo
Maambukizi ya ini na virusi (kama hepatitis C na HIV),
Maambukizi ya figo
Maambukizi ya mfumo wa hewa
Maambukizi ya ngozi na majipu
Dalili ambazo hutokea mara tu unapoacha kutumia heroin;

Kutotulia
Maumivu ya misuli na mifupa
Kutapika
Dalili hizi hufikia kilele ndani ya masaa 48 hadi 72 na hufika kikomo baada ya wiki.

No comments:
Post a Comment