Magari yanayotumia umeme kuathiri biashara ya mafuta ndani ya miaka 10
Suala la magari yanayotumia umeme kuathiri biashara ya uchimbaji na uuzaji mafuta miaka 2-4 iliyopita lisingeonekana kama ni tishio sana, ila sasa watafiti wanasema hivyo.
Ndani ya miaka hii miwili teknolojia ya magari yanayotumia umeme imekua sana. Makampuni mengi yamewekeza katika teknolojia hiyo na hivyo kusababisha ata bei ya magari hayo kushuka kwa kiasi kikubwa.
Kituo la masuala la utafiti chini ya chuo kimoja nchini London – Carbon Tracker Initiative and Imperial College London, kimesema kutakuwa na upungufu wa uhitaji wa mafuta takribani mapipa milioni 2 kwa siku kufikia mwaka 2025.
Soko hilo litapotea kutokana na ukuaji wa ununuaji na utumiaji wa magari yanayotumia teknolojia ya kuendeshwa na umeme. Ripoti hiyo inasema hadi kufikia mwaka 2050 upungufu wa uhitaji utafikia mapipa milioni 25.
Hii inamaanisha mataifa yanayotegemea biashara ya mafuta yanayotumika katika uendeshaji wa injini za magari yataathirika sana. Na pia kutokana na ukuaji wa manunuzi ya magari haya basi tutazidi kuona bei ya mafuta ikizidi kushuka kutokana na ushindani.
Bei?
Bei ya magari yanayotumia umeme yamezidi imezidi kushuka katika mataifa kama Marekani na kila makampuni mengine mengi ya magari yakizidi kuwekeza kwenye magari hayo bei inazidi kuwa sambasamba na ya magari yanayotumia mafuta.
Inategemewa kufikia mwaka 2025 magari yanayotumia umeme yatakuwa asilimia 35 ya magari yanayotumika wakti hadi mwaka 2050 itafikia takribani asilimia 66 ya magari yote.
No comments:
Post a Comment