Search This Blog

Tuesday, 18 April 2017

Kisima cha maarifa

Kisima Cha Maarifa
Chota Maarifa Mbalimbali Uboreshe Maisha Yako Skip to content
KITABU; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.
By Makirita Amani | February 3, 2017

Habari za leo rafiki yangu?

Moja ya changamoto kubwa ambayo watu wengi wamekuwa wanasema inawazuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao ni muda. Watu wana mipango mikubwa na mizuri sana, lakini wanakosa muda wa kutekeleza mipango yao hiyo mizuri.

Watu wanapanga kuanza biashara zao ili kuweza kujitengenezea uhuru wa kifedha, lakini wanakosa muda wa kusimamia biashara zao vizuri.

Watu wanapanga kujifunza zaidi kwa kujisomea vitabu, lakini kila wakitaka kutekeleza hilo muda unakuwa hautoshi.

Wengi sana wanatamani kuwa karibu na familia zao, lakini kazi na biashara zao zinakuwa kikwazo kwao, wanakosa kabisa muda wa kuwa karibu na familia.

Na wengi wanapenda kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao, lakini siku inavyoanza na kuisha, wanajikuta hawana hata dakika chache za kufanya mazoezi.

Muda ni changamoto kwa wengi na watu wametafuta sana suluhisho la namna ya kupata muda wa ziada. Wengi wamekuwa wakisema nikipata muda nitafanya hivi, au vile. Lakini wamekuwa hawapati muda, kwa sababu hawaelewi vizuri muda unapatikanaje.

Kwa kuanza, huwezi kupata muda, bali unaweza kutenga muda. Kila siku yako ina masaa 24, huwezi kuongeza hata dakika moja, hata uwe na fedha kiasi gani. Hivyo kusema nikipata muda nitafanya, ni kusema sifanyi, kwa sababu huwezi kuja kupata muda zaidi ya ulionao sasa.

Ni changamoto hii ya muda imenifanya kukaa chini, kutafiti na kufanya majaribio ya kusimamia muda wangu vizuri na hatimaye nimeandika kitabu; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, Una muda wa kutosha kufanya chochote unachotaka kwenye maisha yako. Hichi ni kitabu ambacho kitakupa wewe maarifa sahihi ya kuweza kusimamia muda wako, kuweza kutenga masaa mawili kila siku kwenye maisha yako, bila ya kujali upo “bize” kiasi gani. Kupitia kitabu hichi nakwenda kukuonesha hatua kwa hatua maeneo unayoweza kupata muda zaidi kwenye maisha yako.

Kama ambavyo wote tunajua, hakuna mtu anaweza kuwa na zaidi ya masaa 24 kwa siku. Sasa ninaposema unaweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku je namaanisha unaweza kuwa na masaa 26? Jibu la swali hilo utalipata ndani ya kitabu hichi.

Hichi ni kitabu ambacho kila mtu ambaye yupo makini na maisha yake, ambaye kweli anataka kufanikiwa, ambaye ameshashika hatamu ya maisha yake na hayupo tayari kuwalalamikia wengine, anapaswa kukisoma. Siyo kitabu cha kuacha kwa sababu maarifa yake ni muhimu sana kwenye usimamizi na matumizi mazuri ya muda wetu.

Kitabu; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU kina sura zifuatazo;

WATU WOTE TUNA MASAA 24 KWA SIKU, MATUMIZI NI JUU YETU.
Hapa nimeonesha namna ambavyo tuna zawadi nzuri ya muda wa masaa 24 kila siku. Pia nimekuonesha jinsi ambavyo watu wanafanikiwa kwenye muda huu huu wakati watu wengine wanashindwa katika muda huu huu.

Muda ndiyo kitu pekee ambacho binadamu wote tumepewa kwa usawa, hakuna anayeweza kukudhulumu wewe muda wako, ila wewe mwenyewe unachagua kujidhulumu.

Kwenye sura hii utapata mwanga wa namna unavyotumia muda wako.

KIPIMO HALISI CHA THAMANI YA MAISHA YETU.
Kwenye sura hii nimekuonesha kwamba thamani ya maisha yako inapimwa kwa matumizi ya muda wako. Siku utakayoondoka hapa duniani, kitu cha kwanza watu watakachozungumzia ni namna ulivyoyagusa maisha yao, na wala siyo mali ulizokuwa nazo.

Hivyo kwenye kitu chochote unachofanya, hakikisha kutoa thamani kwa wengine ni kipaumbele cha kwanza.

TATIZO SIYO MUDA, TATIZO NI VIPAUMBELE.
Kwenye sura hii ninakuonesha namna ambavyo umekuwa unajidanganya kwamba huna muda. Nimekuonesha jinsi ambayo kwa kuchagua wewe mwenyewe, umekuwa unapoteza siku yako, unajikuta umefanya mambo mengi, lakini huoni matokeo makubwa.

Ninakuonesha kwa nini vipaumbele ni muhimu zaidi kuliko kufanya kila ambacho unajisikia kufanya.

JINSI UNAVYOWEZA KUPATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.
Kwenye sura hii ndiyo naanza kukuonesha kwa mfano, hatua kwa hatua namna unavyoweza kupata masaa mawili ya ziada kila siku, kwenye siku yako ya masaa 24.

Kupitia sura hii, unakwenda kuiangalia siku yako kwa undani, na kuona mambo ambayo umekuwa unayafanya lakini siyo muhimu na kuacha kuyafanya au kuyapangia muda mwingine wa kuyafanya.

Kuna mambo matano ya kufanya ili uweze kupata masaa mawili ya ziada kila siku. Utajifunza mambo hayo matano kwenye sura hii.

MATUMIZI BORA YA MASAA MAWILI YA ZIADA ULIYOPATA KWENYE SIKU YAKO.
Ukishapata masaa mawili ya ziada, kwenye zoezi utakalojifunza kwenye sira ya nne, nimeona nisikuache na masaa hayo bila ya kukushauri kitu cha kufanya. Kwa sababu ukibaki nayo yakiwa matupu, utajikuta unapoteza muda zaidi.

Kwenye sura hii nimekushauri matumizi mazuri ya masaa yako mawili ya ziada ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako na uweze kufanikiwa.

Nimekushauri mambo matano unayoweza kuanza kuyafanya mara moja, ukayafanya kila siku na ukaweza kufanikiwa sana.

Pia nimekushirikisha maeneo kumi ambayo unaweza kujifunza kila siku na ukapata taarifa, maarifa na hamasa ya kufanikiwa.

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KULINDA MUDA WAKO.
Kupata masaa mawili ya ziada siyo kazi ngumu, utaona mwenyewe ukishafanya yale utakayojifunza kwenye kitabu hichi. Changamoto ni kwamba wapo maadui wanaokazana kuiba muda wako huu. Kuna watu au vitu ambavyo vinakuibia muda wako bila ya wewe mwenyewe kujua.

Kwenye sura hii nimekushirikisha mambo mawili muhimu ya kufanya ili kuweza kulinda muda wako. Ukifanya mambo haya mawili, kamwe hutakuja kupoteza tena muda wako.

JINSI UNAVYOWEZA KUONGEZA MUDA WAKO MARADUFU.
Baada ya kukuwezesha kupata masaa mawili ya ziada kwenye siku yako, nikakupa na mambo ya kufanya kwenye masaa yako mawili ya ziada, pamoja na namna unavyoweza kuyalinda, changamoto bado haijaisha, masaa mawili ni machache sana.

Ili ufanikiwe unahitaji kuwa na masaa kuanzia elfu moja na kuendelea kwa siku. Unahitaji kuwa na masaa elfu kumi, laki moja na hata masaa milioni moja kwa siku.

Kwenye sura hii nakushirikisha jinsi unavyoweza kupata muda maradufu, yaani kupata muda mwingi zaidi kila siku ili kuweza kufanya makubwa. Hakuna mtu amewahi kufanikiwa duniani kwa kufanya kazi masaa nane au kumi kwa siku, unahitaji masaa mengi zaidi ya hayo, na nitakuonesha namna unavyoweza kuyapata kwenye sura hii.

Nirudie tena kukusisitiza rafiki yangu, hichi siyo kitabu unachopaswa kukikosa, kisome na fanyia kazi yale ambayo umeyapata, maisha yako yatakuwa bora zaidi.

JINSI YA KUPATA KITABU; PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

Kitabu hichi kinapatikana kwenye mfumo wa nakala tete (yaani softcopy, pdf) hivyo unaweza kukisomea kwenye simu yako, tablet au hata kompyuta.

Kitabu hichi kinatumwa kwa njia ya email, hivyo unaweza kutumiwa popote pale ulipo Duniani.

Gharama ya kitabu ni tsh elfu tano (5,000/=).

Kukipata kitabu tuma fedha kwa namba zifuatazo; 0755 953 887 au 0717 396 253 (namba zote jina ni Amani Makirita). Ukishatuma fedha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye email yako na jina la kitabu MASAA MAWILI kisha utatumiwa kitabu kwenye email yako.

Usikose kitabu hichi kizuri rafiki yangu, ni njia ya uhakika ya kununua uhuru wako wa muda na kuweza kufanikiwa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Washirikishe Wengine:
FacebookTwitterGoogleLinkedIn1Email
Related
Jinsi ya kutengeneza bajeti ya matumizi mazuri ya muda wako kama mjasiriamali.
August 31, 2015
In "BIASHARA/UJASIRIAMALI"
UKURASA WA 624; Hatua Iliyo Ngumu Zaidi Kwenye Safari Ya Mafanikio...
September 15, 2016
In "KURASA ZA MAISHA"
Mambo Matano(5) Muhimu ya kuzingatia kama umepanga kuanza biashara 2016.
January 5, 2016
In "BIASHARA/UJASIRIAMALI"
Category: VITABU
Post navigation← UKURASA WA 764; Samaki Huanza Kuozea Kichwani…UKURASA WA 765; Weka Macho Yako Fedha Zako Zilipo… →
You must log in to post a comment.
TAFUTA HAPA

Search for: 
Ingia Hapa (LOG IN)

You are not logged in.
Username

Password

Forgot?  Register
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kujiunga unapata yafuatayo;
1. Makala za ujasiriamali na biashara.
2. Makala za kujijengea tabia za mafanikio.
3. Makala za uchambuzi wa vitabu.
4. Makala zinazohusu mafanikio ya kiwango kikubwa(WORLD CLASS)
5. Kuingia kwenye KUNDI LA WHATSAPP lenye watu wengi waliofikia mafanikio.
Kupata maelezo ya kujiunga BONYEZA MAANDISHI HAYA KUJIUNGA NA KISIMA

JIUNGE NA KUPOKEA MAKALA KWENYE EMAIL

Weka email yako hapa na bonyeza NIUNGE na kila makala inapotoka utatumiwa moja kwa moja kwenye email yako.
Karibu sana.

Join 524 other subscribers

W

MAKALA MPYA

UKURASA WA 840; Chochote Usichokijua Ni Kigumu… April 19, 2017
UKURASA WA 839; Haijalishi Hali Ya Uchumi Ikoje, Fursa Za Kutengeneza Fedha Bado Ni Nyingi… April 18, 2017
UKURASA WA 838; Mmoja Kati Ya Wengi Na Mmoja Kati Ya Wachache… April 17, 2017
UKURASA WA 837; Kitu Kimoja Cha Kuboresha Chenye Matokeo Makubwa Kwenye Maisha Yako Ya Mafanikio… April 16, 2017
UKURASA WA 836; Fukuza Nusu Ya Wateja Wako… April 15, 2017
MAKUNDI YA MAKALA

AUDIO BOOKS (1)
BIASHARA LEO (129)
BIASHARA/UJASIRIAMALI (100)
BLOGGER (9)
DARASA LA JUMAPILI (3)
FALSAFA MPYA YA MAISHA (81)
FALSAFA YA USTOA (23)
FURSA (3)
KURASA ZA MAISHA (839)
MAKALA KWA WOTE (765)
NENO LA LEO (236)
ONGEA NA COACH MAKIRITA (24)
USHAIRI WA KOCHA MAKIRITA (1)
TABIA ZA MAFANIKIO (57)
UCHAMBUZI VITABU (110)
EAT THAT FROG (1)
KITABU; A Guide to the Good Life The Ancient Art of Stoic Joy (23)
KITABU; RICH DAD, POOR DAD (17)
THE RICHEST MAN IN BABYLON (19)
THINK AND GROW RICH (15)
UJUMBE WA LEO (125)
VITABU (8)
VITABU VYA MAFANIKIO (1)
WORLD CLASS (101)
SIKU 30 ZA MAFANIKIO (31)
SIRI 50 ZA MAFANIKIO (48)
MAKALA ZA ZAMANI

MAKALA ZA ZAMANI
MAKALA ZILIZOSOMWA SANA

VITABU
UKURASA WA 839; Haijalishi Hali Ya Uchumi Ikoje, Fursa Za Kutengeneza Fedha Bado Ni Nyingi...
KARIBU KISIMA CHA MAARIFA
Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.
JE WAJUA; Nchi Ya Kwanza Africa Kupata Uhuru.
UKURASA WA 836; Fukuza Nusu Ya Wateja Wako...
UKURASA WA 838; Mmoja Kati Ya Wengi Na Mmoja Kati Ya Wachache...
Utaratibu Wa Kupata Kitabu Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.
UKURASA WA 835; Kudanganya Na Kutosema Ukweli Wote...
MEDITATION(TAJUHUDI); Maana Yake, Jinsi ya Kufanya na Faida Zake.

Sunday, 16 April 2017

Mambo 39 Yanayovunja Mahusiano Ya Kimapenzi Au Ndoa

Mambo 39 Yanayovunja Mahusiano Ya Kimapenzi Au Ndoa
Muungwana Blog · 2 days ago

Mambo 39 Yanayovunja Mahusiano Ya Kimapenzi Au Ndoa

1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.
17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika                maisha yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara anapokuwa katika msongo wa mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako [kutoendeshwa na watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa kumtunza na kumjali mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.

Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata ndoa kuharibika maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku atachoka, maana hana moyo wa jiwe bali ana moyo wa nyama. Kuvumilia nako kunamwisho wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu, vidonda vya mapenzi, vifo vya watu wengi na kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda na kupendwa katika maisha yao